Je, ni kosa kisheria kutumia VPN?

Ghaysh

Member
Feb 12, 2015
24
43
TCRA vs VPN:
Moja, TCRA haina mamlaka kisheria kumtaka raia kwa LAZIMA atoe "IP Address" yake. Hata KUOMBA raia atoe "IP Address" ni kosa. Hili la VPN nalo linapotoshwa tu. Matumizi ya VPN hayajazuiwa na sheria yoyote ile kama wengi wanavyoaminishwa.

Pili, Kanuni za 2020 zinazotumika KUDHIBITI raia ni BATILI kwa msimamo wa Ibara 64(5) ya Katiba ya nchi kwa sababu Kanuni hizo zinavunja Ibara 16(1) ya Katiba yenyewe, inayotoa HAKI YA FARAGHA ya mawakiliano binafsi. Pia, kanuni hizi za TCRA zinavunja Ibara ya 6(d) & 7(2) za Mkataba wa Afrika Mashariki, ambazo zinataka shughuli za kiraia kuongozwa KIDEMOKRASIA chini ya misingi ya UTAWALA BORA.

Tatu, kwa upande mwingine, Sheria ya Makosa ya Mtandao (Cybercrimes Act, 2015) kifungu cha 31 & 32 vinaeleza UTARATIBU wa askari polisi kupata USHAHIDI ulio ndani ya "computer device" ya mtuhumiwa. Ambapo, mtuhumiwa HALAZIMISHWI kutoa "IP Address" au VPN access kwa askari, na katika hatua hii, raia anaweza kukataa kutoa ushirikiano ili kulinda haki zake. Hapo ndipo askari polisi (mpelelezi) hutakiwa kisheria kuomba KIBALI MAALUM toka kwa mahakama, huku akitoa SABABU YA MSINGI ili apewe access na mtuhumiwa (sio mara zote hupata kibali). Huu ndio utaratibu unaopaswa kutumika kama mtu amevunja sheria za TCRA na sio hiki ambacho TCRA inataka kuaminisha raia kuwa ndio utaratibu!

Nne, TCRA kutumia utaratibu wake binafsi (ambao haupo kisheria) inakuwa ni kuingilia utaratibu ulioko kisheria hapo juu . Nasisitiza, wakati pekee ambapo raia atalazimika kutoa "IP Address" ni kwenye hatua ya UPELELEZI wa kosa la mtuhumiwa (kama anasadikiwa kutenda kosa) na si vinginevyo.

Tano, kama mtu hajatenda kosa lolote, TCRA haitakiwi kisheria hata KUOMBA "IP Address" yako, na hii si kazi ya TCRA bali ni kazi ya polisi mpelelezi wakati wa UPELELEZI tu. Hivyo, TCRA kuhitaji "IP Address" za raia, ni kitendo cha kutaka KUDUKUA mawasiliano ya watu ambapo ni kosa kisheria. TCRA iache KUPOTOSHA sheria & kanuni zinazoipa miongozo kwayo, maana kanuni hazisemi kama ambavyo raia wanaaminishwa.

Sita, narudia tena, kwa msimamo wa sheria ya sasa, mtu anaweza ombwa "IP Address" na ASKARI POLISI tu wakati wa UPELELEZI wa kosa linalosadikiwa kufanyika na si wakati mwingine wowote. TCRA kuomba "IPA" za raia kabla ya KOSA ni kutaka kufanya UDUKUZI, maana TCRA wakiwa na "IP Address" ya mtu, wanaweza kuona kila kitu mtu huyo anachokifanya mtandaoni.

ANGALIZO:
Huu waraka wa TCRA unavunja sheria & kanuni za TCRA lakini pia unaingilia taratibu za sheria nyingine. Lakini pia, kanuni zenyewe zinavunja Katiba ya nchi, hivyo ni BATILI. Hili la VPN pia ni USANII tu na halipo kisheria, bali limebuniwa tu. Sitaki kupoteza muda kulizungumzia.

Mwisho, binafsi, napuuza waraka wa TCRA na nitawakata wakasome sheria & kanuni vizuri kabla ya kuja kwa wananchi. Hiki kinachofanyika ni SIASA.

NB: Nimeikuta mahali
 
Ukataze vpn eti kilinda maadili,harafu mloganzila wanafanya operesheni ya kuongeza
 
Back
Top Bottom