Kosa la Rugemalira ni nini ?

Kosa na dhambi ya mauti ya Rugemalira ni Kula njama na kusaidia wizi wa mabilioni ya pesa za umma, and to add salt to injury; anazigawa kama njugu, bila uchungu na mamilioni ya watanzania maskini.

pesa za umma zipi?
 

Mkuu inabidi utulie na kuwaza kwa umakini sana ndio utaelewa kilichofanyika hapa. Ruge ameitahadharisha serikali kuhusu utapeli unaotaka kufanyika katika IPTL kwa kuandika barua kibao, ameenda mbali zaidi amefungua amaefungua kesi ili IPTL ifilisiwe. Wakati huo huo mahakama ya kimataifa imeshatoa hukumu IPTL imekuwa ikiicharge TANESCO hela zaidi hivyo inatakiwa ilipwe. Wahusika kwa upande wa serikali hawafanyi hivyo, Sigh (Tapeli) anakuja anataka kuichukua IPTL (ambayo Ruge bado ana hisa 30%, kumbuka Ruge anajua kabisa TANESCO ikilipwa hela iliyokuwa overcharged Ruge naye inakula kwake). Ruge, Sethi na viongozi wala rushwa wakijua hili, wanachelewesha kwa makusudi kutekeleza waliyoamriwa na mahakama ya kimataifa.

Ruge akijua kabisa IPTL inataka kuchukuliwa na Sethi kiujanja ujanja (ameshaitahadharisha serikali, amefungua kesi na anataka ifilisiwe through RITA), akiwa kama mkurungenzi na akijua pia IPTL inatakiwa iilipe TANESCO anaamua kutumia maujanja (kumbuka Ruge ana connections na viongozi na wafanyabiashara, Sethi hana). Anapewa 7milioni ya kianzio kwa kumuuzia TAPELI hisa zake 30%(wewe ni mkurugenzi kampuni yako (IPTL) inatakiwa ilipe pesa kwa TANESCO). Hapa utaona kuwa Ruge akiwakilisha IPTL amekiuka hukumu ya mahakama na ili kujiweka mbali anauza hisa zake fasta kwa kuamua kupokea kianzio kutoka kwa TAPELI.

Naweza kusema with confidence kuwa makubaliano ya kuuziana na Seth yalikuwa influenced na pesa iliyopo account ya ESCROW. Alichofanya Ruge ni kuuza kwa Seth ili yeye asiwe front (kujificha), ndio maana hela ilipokwapuliwa tu Ruge kalipwa. You dont need to be a Professor to see this. Nina uhakika kama TAKUKURU wamefanya kazi yao vizuri ni rahisi sana kumuipmplicate Ruge hapa. Lazima makubaliano ya kuuziana walionyesha hilo salio baada ya kutanguliziwa dola 7m zitalipwa lini. Sasa hapa ndio patamu maana wale wote waliotakiwa kuhakikisha IPTL inailipa TANESCO kama ilivyoamriwa ndio hao hao Ruge amewalipa pesa nyingi. Ruge hawezi kupona hapa. Proper investigation lazima ita uncover deal lote na kama Sethi pia aliwalipa hawa viongozi which is unlikely maana wanyemjua hapa ni Ruge.

Lawyer mzuri anamkamata Ruge kirahisi sana, saaaaaana tu. Kiufupi Ruge ni muhumjumu uchumi na akijua kama mkurungenzi wa IPTL anatakiwa ailipe TANESCO na akijua IPTL inataka kununuliwa kitapeli ameshiriki kufanya uhalifu ndani ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
zile pesa ni za tanesco na iptl lakini iptl wamechukua wao zote.

tanesco hakuwa na chake pale.kumbuka gharama zilishashushwa kutoka 3.6 mil dola kwa mwezi hadi 2.6 mil dola kwa mwezi.na hyo ilikuwa amri ya mahakama ya migogoro ya kibiashara ya kimataifa.tanesco walikata rufaa wakitaka ishuke zaidi ya hapo lakini haijawa hvyo.na hzo hela zimewekwa escrow ikiwa ni tanesco anamlipa iptl kila mwezi.tanesco hana chake pale mpaka iwe vingnevyo.
 
Kosa lake kubwa ni hata hio 30% ownership ni uwizi hajawahi kuweka mtaji hapo

Kwakuwa kazoea kuiba, kudanganya na kutapeli ndio 40 zake zimefika
 

safi mkuu namm nilkuwa nashangaa sana tatzo la watz ni hear say sana.mzee wawatu anapiga kaz mchana na usiku kujiimalisha kiujasilia mali tatizo lingine hawapend jisomea kujua background ya mtu.kati ya madon wanaokwenda smart na mambo yao ni huyu mzee huwez kuta anapata fedha kiujanja ujanga kwake legal terms applies always ila wanaomshutumu wawe makini sana watamlipa pesa nyingi sana
 
kuwahonga kwa nini? yeye anamiliki 30% ambazo zina thamani hiyo ya 75mi USD. Sasa hapo ahonge ili iweje? kwani singasinga asingenunua yeye angeumia kivipi? Na je, hao majaji na mawaziri wanahusika vipi na ununuzi wa hisa wa PAP from VIP?

hear and say hao usipoteze muda wako wanasema wasichokijua mkuu
 

Ruge alilipwa kwanza mwezi september, escrow akaunti fedha zilitolewa december!
 
mimi sio mwenzako mimi ni "interahamwe, FDLR, ideology, RNC, traitor, divisionist, revisionist. A.K.A. BBC!"

meaning mnyarwanda. Huwezi kuwa yote hayo halafu ukajiita Mtanzania.
 

Mkuu hap umeelezea vizuri sana.kma kuna watu hawaelewi basi watakua na matatizo.nionavyo hapa kuna mnyukano Wa kisiasa.ruge maelezo yake yapo clear San.sema kiushabiki kuna watu wamejitoa ufahamu kbisaa na kuamini wanakiamini bila kufany utafiti.big up bro.ukwil siku zote utakuweka huru
 
mbona habari zanasema mahakama ya usuluhishi ilitoa majibu kuwa kulikuwa na overcharge mwezi january/february mwaka huu na pesa zilitolewa november/december?. hiyo inaeleza pia kwanini ruge kahonga pesa mwezi february mara baada majibu ya mahakama kuwa mabaya upande wake. hakuwa na intetion ya kugawa pesa kabisa.
 

Hapo namba mbili hata me nashangaa.kwa hadhi ya rugemalila sijui watu walitaka awape pesa wauza karanga au wauza nyanya ndo mngerizika.hao watu aliowap pesa rugemalila ndio watu Wa class zake.huwez jua wanasaidianje kibiashara na kifamilia.ivi kwa akili timamu inaeweza kw nini ruge kampa hela jaji au akina chenge..kumbuka ye ni mfanyabiashara na ana hadhi ya watu Wa class fulan ktk jamii
 
meaning mnyarwanda. Huwezi kuwa yote hayo halafu ukajiita Mtanzania.

acha hizo wewe...ingia PM kwa malumbano binafsi, hapa tunazungumzia ishu serious. Wewe unaionaje? kama mtanzania half-cast?
 

Ruge aliuza hisa zake september. Fedha za escrow zilitolewa December. Mtu kashapata chake ahonge ili iweje?
 
Kosa lake kubwa ni hata hio 30% ownership ni uwizi hajawahi kuweka mtaji hapo

Kwakuwa kazoea kuiba, kudanganya na kutapeli ndio 40 zake zimefika

actually aliweka mtaji, na hata asingeweka, umma wa watanzania unaingiaje hapo? kwani IPTL ni kampuni ya umma?
 
Ruge aliuza hisa zake september. Fedha za escrow zilitolewa December. Mtu kashapata chake ahonge ili iweje?
the citizen wanasema mwanzoni mwa mwaka huu mahakama ya usuluhishi ilisema kulikuwa na shida kwenye charges hivyo iptl na tanesco wapige hesabu nani apate nini. jambo baya ni kuwa pesa zilishatolewa disemba. ruge akaanza kuhonga iili kunyamazisha watu. ndiyo maana uhongaji mwingi umefanyika februari baada ya uamuzi wa mahakama.
 

jamaa ni mdini

anawapa pesa watu wa dini moja tuu

inamaana hana hata shamba boi wa dini yetu?
 

ruge yeye amelipwa september, sasa ahonge watu mwaka huu ili iweje? Isitoshe yeye ameuza hisa, ingekuwa bado ni mwanahisa wa IPTL hapo sawa, kwani angepata mgawo wa escrow kwa asilimia zake 30, lakini yeye aliuza hisa kabla ya mambo ya escrow december.
 

jamaa ni mdini

anawapa pesa watu wa dini moja tuu

inamaana hana hata shamba boi wa dini yetu?

shamba boi wa mhaya anatakiwa awe na digrii tatu kama Le shatiz bin kufunika kitensa, dini yenu si mnajijua mlivyo "wasomi"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…