Kosa la Rugemalira ni nini ?

Kosa la Rugemalira ni nini ?

JMali mbona jina lako kama James rugeMALIla?



Na mimi naombeni mgao nikaezeke kibanda changu kule kikongo.
 
FACTS:

1. James rugemalira alikuwa anamiliki 30% ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP. Asingeziuza hizo hisa, mpaka leo angekuwa bado anamiliki 30% ya IPTL KIHALALI kabisa, hivyo kuwa mbia mwenza wa PAP.
2. James rugemalira aliuza hizo share zake kwa kampuni ya PAP kwa dola milioni 75. Uuzaji wa hizi hisa ulifuata taratibu zote kisheria including ulipaji kodi.

MASWALI:
1. Huyu ndugu anaitwa mwizi kivipi? Amelipwa fedha kutokana na kuuza hisa, tatizo liko wapi hapo? Kisheria angeweza kumuuzia yoyote yule tofauti na PAP hizo hisa kama wangeafikiana bei! PAP wamefikia dau na yeye kawauzia, where is the problem hapo? IPTL sio kampuni ya umma, PAP sio kampuni ya umma, VIP sio kampuni ya umma. This is purely a private sector transaction. Mbona Rostam aliuza share zake vodacom kwa mabilioni tena kupitia nje ya nchi lakini hakuitwa mwizi (kwa kukwepa kodi among other things), badala yake akasherehekewa kwa front-page news? Naomba kufahamishwa kwa hoja tafadhali, uharamia wa James Rugemalira upo wapi.
jamaa hakuiba directly, alitumia mbinu ili watu kama wewe msiweze kuelewa. alijua pesa za escrow zinaenda tanesco na hisa zake zingeshuka sana thamani. ndiyo akaanza michakato ya kutoa hela kwa kushirikiana na aliowalipa ili anunuliwe. PAP wasingenunua hisa zake kama asingewahakikishia kwa kupata pesa. ni kama mwanamke aliyejitolea mahari sema hapa hiyo mahari anakuwa kaiba.
 
ni njama ya wizi mkubwa kati ya maofisa wakuu serikalini wawekezaji wanasiasa na wanasheria. makosa ya ruge yanahitaji kubainishwa wazi ili ashtakiwe. upo ushahidi tele wa kutoa rushwa na taarifa za uongo.

Msiwa na hamaki isiyo na mashiko ndugu,hela za Escrow hakuzichukua
Ruge.Isitoshe hzo hela hazikuwa tayari mali ya TANESCO,mbona tu wazito wa kuelewa??Nitawaelewa kama hoja itakuwa ni ukwepaji kodi wakati wa mauziano ya hisa au kufufua hoja kwamba IPTL mkataba wake na TANESCO haukuwa fair.MAMBO YA ESCROW NI POLITICS TU,HAKUNA LA MAANA,HASA KUMHUSU RUGE.
 
jamaa hakuiba directly, alitumia mbinu ili watu kama wewe msiweze kuelewa. alijua pesa za escrow zinaenda tanesco na hisa zake zingeshuka sana thamani. ndiyo akaanza michakato ya kutoa hela kwa kushirikiana na aliowalipa ili anunuliwe. PAP wasingenunua hisa zake kama asingewahakikishia kwa kupata pesa. ni kama mwanamke aliyejitolea mahari sema hapa hiyo mahari anakuwa kaiba.

Ebu tujuzeni, ni kwa mapana gani hela kwenye akaunti ya Escrow haikuwa mali ya IPTL.Na kama haikuwa ni nani kati ya serikali na STANDARD CHARTERED BANK atakuwa mmiliki halali?
 
Mkuu jMali,
Braza Ruge tunambana hapa!
  • Mosi, yeye ni mtu anayeifahamu IPTL in and out kwa sababu amekuwa nao kwenye biashara kwa muda mrefu. Ushahidi unaonesha wazi kwamba PAP imepata 70% ya hisa za IPTL kwa magumashi. Inasemekana baada ya Singh kuingia nchini, Ruge alimpinga huyu bwana... Aidha, kuna kila dalili kwamba hata hiyo PAP yenyewe ni ghost company. Pamoja na yote hayo, bado Braza Ruge akawauzia PAP hisa zake 30%. Sasa ikiwa Ruge alikuwa anaifahamu IPTL na Menchmar in and out to the point kwamba ilikuwa ni rahisi kwake kama kufumba na kufumbua kufahamu ikiwa kweli PAP waliuziwa 70% za Menchmar ambazo inaonesha kwamba hawakuuziwa ama wameuziwa kimagumashi.... sasa je, huoni Ruge nae ameuza hisa zake kwa mtu ambae bila shaka alifahamu kwamba ni mwizi tu na bado akawa tayari kufunika kombe... PAP wachukue pesa zetu zilizokuwa Escrow wakati anafahamu haikuwa sahihi?
  • Umwagaji wake pesa kwa viongozi na watendaji wa serikali na wale ambao walipata kuitumikia serikali ni jambo ambalo halipaswi kuachwa hivi hivi. Ni kweli, pesa ni zake na ana haki za kutumia apendavyo lakini inapoonekana kwamba wengi wa waliolipwa wanatoka sekta ile ile ya nishati huku wengine wakiwa hawapo tena kwenye system, lakini ile tu kuwa walipata kuwamo MEM, tayari nao anawapa mamilioni ya pesa... hili si jambo dogo... Si hivyo tu, hata wale ambao ni wahusika katika mikataba ya serikali, AGs... Chenge ambae ameshastaafu kwenye hiyo nafasi long time ago lakini nae kamegewa mzigo wa kutosha! Kuna yule wa RITA ambae RITA ndio wanahusika kwenye masuala mazima ya ufilisi huku Braza Ruge nae alipeleka kesi mahakamani kutaka IPTL ifilisiwe... hili ni jambo ambalo hutakiwi kulipuuza hata kidogo! Kama nilivyosema hapo awali, pesa ni zake na ana haki ya kutumia apendavyo lakini anapomwaga mamilioni kwa watendaji wa serikali ambao kwa kiasi kikubwa wanahusika na IPTL in one way or another... NO PLEASE, tunahitaji maelezo yasiyopinda pinda na atuambie amefanya nao biashara gani! ALWAY, I repeat, ALWAYS, there's only one money related business between government officials and business executives especially if such transaction isn't done on public... what's the business? The answer is simple: CORRUPTION! Here's the Theory: "To Every Corrupt Government Official, There's a Corrupt Business Executive Behind Him!"

1. Bado sioni shida iko wapi, hizo 70% ya IPTL ambazo unasema sing sethi kanunua kimagumashi zilikuwa za serikali? Bado masuala yote ya ndani ya IPTL, Mechmar etc, ni mambo ya private sector! Rugemalira hajadeal na serikali yeye ame-deal na PAP! vile vile kwenye suala la Rugemalira kumpinga sethi ni hivi: Rugemalira alikuwa na kesi na IPTL akitaka IPTL ifilisiwe na yeye apate haki zake i.e 30% ya value ya IPTL. Singh sethi alivyokuja hakuweza kununua zilie 70% kwa sababu ya kesi ya rugemalira mahakamani, ikabidi kwanza sethi aelewane na Rugemalira kwa kumpa advance ya 7Mil USD, na ndipo Rugemalira akaondoa kesi mahakamani iliyomuwezesha sethi (and for that matter anyone else) kununua hisa za Mechmar/PiperLink, hata ukiangalia timeline of events unaweza kuona kuwa hata deal yenyewe kati ya sethi na Rugemalira ilifanyika BEFORE hii mambo ya escrow account.

2. Afadhali tunakubaliana kuwa hakuna msingi wowote wa kuchunguza fedha binafsi za mtu zinakwenda wapi. Pili, hakuna taarifa yoyote rasmi inayothibitisha kuwa Rugemalira amewalipa watu gani fedha isipokuwa hizi picha picha za JF. Mtu pekee ambaye inajulikana kuwa kapokea fedha toka kwa Rugemalira ni taasisi ya elimu inayoendeshwa na mama tibaijuka, ingawa baadhi ya watu wanataka ieleweke kuwa zimeingia mfukoni mwa mama Tibaijuka personally! Na sababu pekee inayofanya tujue ni kuwa FEDHA HIZI ZILITOLEWA WAZI WAZI! Hii inaonyesha kuwa mtoaji na mpokeaji wote hawana la kuficha.
tatu, hao watu wanaodaiwa kupewa fedha mbona haionekani kivipi wanaweza kuwa part of escrow account transaction? Hivi mama tibaijuka alipwe bilioni ili afanye nini? Askofu kilaini? Andrew chenge? Roles zao ni zipi kwenye hili sakata? Rejea tena: Rugemalira had 30% of IPTL na hizo ndizo alizouza, na angeweza kuuza kokote kule kwa bei hiyo hiyo, mitambo ya IPTL ubungo pale ni zaidi ya 250mil USD, hivyo hata IPTL ingefilisiwa rugemalira angepata roughly the same amount. Sasa hawa watu wote tunaoambiwa wamehongwa na rugemalira, wamehongwaje?
 
jamaa hakuiba directly, alitumia mbinu ili watu kama wewe msiweze kuelewa. alijua pesa za escrow zinaenda tanesco na hisa zake zingeshuka sana thamani. ndiyo akaanza michakato ya kutoa hela kwa kushirikiana na aliowalipa ili anunuliwe. PAP wasingenunua hisa zake kama asingewahakikishia kwa kupata pesa. ni kama mwanamke aliyejitolea mahari sema hapa hiyo mahari anakuwa kaiba.

1. Not true, PAP wasingeweza kununua IPTL kutokana na kesi ya Rugemalira mahakamani. PAP walimlipa Rugemalira kwanza kabla ya escrow. Walianza kwanza na advance ya mil 7 USD, Rugemalira akaondoa kesi yake mahakamani halafu ndio wakamalizia zile zilizobaki.
2. kesi ya rugemalira dhidi ya IPTL ilikuwa ni kutaka IPTL ifilisiwe ili yeye apate thamani ya asilimia zake 30. Thamani ya hisa zake ilikuwa pale pale siku zote.
 

kutokana na link yako, naomba upitie yafuatayo:

1. A joint venture known as Independent Power Tanzania Ltd is set up between Mechmar Corporation of Malaysia (70 per cent) and VIPEM of Tanzania (30 per cent).

2. March 1, 2002 – VIPEM petitions the High Court of Tanzania to wind up IPTL.

3. 2009 – The High Court of Tanzania places IPTL under a receiver manager (RITA) following the 2002 winding up petition filed by Mr Rugemalira.

4. 2010 – Mr Sethi comes to Tanzania, and claims that he had bought 70 per cent of IPTL from the Malaysian company. He attempts to take over the management of the company, but fails because of the winding up petition filed by Mr Rugemalira, the minority shareholder, who owns 30 per cent of IPTL

5. September 2013 – Mr Rugemalira finally agrees to sell his 30 per cent stake to Mr Sethi's company called PAP for $75 million. He is paid an advance of $7 million on the condition that he withdraws his winding up petition filed at the High Court of Tanzania. Mr Rugemalira withdraw the petition, which paves the way for the consent judgment issued by Mr Justice John Utamwa in September.

Mbona kila kitu kipo wazi? Sethi ali-deal kwanza na Rugemalira kwa kumpa stahiki yake na ndipo akaingia kwenye mambo ya escrow. James rugemalira hapa hana kosa lolote! vinginevyo labda unionyeshe ni wapi ambapo James Rugemalira ana kosa.
 
Ndugu usishangae sana kuhusu sisi Watanzania na mimi nikiwemo. Na tunadhihirisha na tafiti zilizofanywa tukaonekana Tanzania tuna watu wa IQ ndogo sana na ndio maana badala ya kujadili issue tunajadili watu . Badala ya kujiuliza zile 70% of shares zilikuwa halali kuuzwa TZS6m? Was due process followed to the letter? Badala yake tunaletelwa list ndefu ya majina tena tunashupalia yale ambayo tunayajua kwa maana ya judges na mawaziri. Inakuwaje mmiliki wa 30% aliyeuza share kuahalali mchana kweupe katika jua la utosi na kulipa kodi ndio tunataka kumsulibisha. Tumeruka toka kwenye fedha kuchukuliwa na singasinga sasa tunataka kutundika wa 30%. Tumeama badala ya kuagnalia due process tunajadili majina kuwa wamegawiwa pesa kama njugu. Is this really our concern? Do we have a process that governs monetary transactions. is it viable? Does it need improvement? Is the country protected? Are our local investors protected by laws and policies? Watanzania lets think bigger. Wakati wa Richmond tudanganywa na wanasiasa kwa sababu ya chuki zao za kukosa vyeo. Bwana Lowasa wakati anakubali kujiuzuru alitoa speech lakini hatukuagalia context yake kuwa " shida ni uwaziri mkuu" . Sote ni mashahidi baaada ya kumtosa yuleyule aliyeliazisha Samwel Ssita kasema mjadala umefungwa yeye akaja kuuendeleza nje ya bunge baada ya jinamizi la Dowans na kuamuliwa kuwa lazima tuwalipe. Haya yote yanatokea na kwa hii Escrow yatatokea maana we are discussing people and not the process neither the issue

spot on mkuu, unajua mpaka imebidi niangalie ulijiunga JF lini ndio nikaelewa. Siku hizi JF imebadilika sana watoto wamekuwa wengin kuliko watu wazima, hoja kama zako ni nadra sana kuziona JF nowadays.
 
Go deep you are trying to ask light questions for serious problem.issue si kuuza share.hicho ni kitu cha kawaida kabisa kwa wale wanaojua mambo fedha.Tatizo linaanzia tanesco ambalo ni shirika la umma.tanesco na iptl wana mkataba wa kuuziana umeme.Regemalila yuko ndani ya iptl na akaunti yake imetumika ktk kukwapua pesa benki kwenye account ya escrow.sasa basi ebu jiongeze mwenyewe kuanzia hapo au fuatilia vizuri huo mjadala bungeni utajua nn kimefanyika

naomba wewe ndio ujiongeze kwani facts ni hizi:
1. Ni kweli Tanesco na IPTL wana mkataba wa kuuziana umeme, na Rugemalira alikuwa ndani ya IPTL kupitia VIP. Lakini Rugemalira alikuwa na mgogoro na wanahisa wenzake Mechmar humo ndani ya IPTL ambao wao ndio walikuwa wanaendesha IPTL kwa vile rugemalira alikuwa minority shareholder. Rugemalira aliweka kesi mahakamani ili IPTL IFILISIWE ili yeye apate ku-cashout his 30%! Si kweli kwamba akaunti yake imetumika kukwapua fedha za escrow.
2. Fedha za escrow au hizo zinazodaiwa kutoka tanesco zimetolewa na serikali sio rugemalira, mhusika hapo ni serikali.
 
Umejipanga kuja kuongeza hasira za watu! bila shaka ni sababu ya nguvu ya hiyo hela vinginevyo tutakuja na version ya Rugemalira baada tu yahili la watumisi wetu kukaa sawa.

hasira zisizo na msingi ni upu.mbavu! Huwezi kuwa na hasira halafu ukiulizwa umekasirika nini ushindwe kusema, badala yake ukasirike zaidi!
 
Only the court of law can give best answers to your questions! Again , is Tanzania judiciary credible?

on what basis would one take rugemalira to court? He owned 30% of IPTL legally, He sold them legally, He paid taxes! on what basis i ask you!
 
...




Acha uzembe cag na wengine hawakuliona hilooo.

Mzembe ni wewe kwa kutokujua kuwa CAG anachunguza mali za umma sio binafsi, CAG amechunguza uhamishaji wa fedha za escow, sio uuzaji hisa kati ya PAP na Rugemalira (VIP) ambao ni private sector.
 
Tusijibu juu juu hii hoja. Hata mimi niliposoma katika gazeti la The Citizen mtiririko wa matukio yote ya hili sakata, niliona kama vile JR hana kosa, kwani aliuza hisa zake kabla hata fedha za ESCROW hazijaruhusiwa kugawiwa IPTL. Naomba tujibu hoja kwa hoja, sio kusema tu kuwa mleta mada ametumwa bila ya kujenga au kujibu hoja
 
Mkuu unaonekana upo mbali na ukweli na hata haufuatilii issue nzima ilivyo. Kwa taarifa yako JR aliwahi kuiandikia Wizara ya Nishati na kupeleka nakala kwa taasisi 23 ikiwemo BoT, kwamba PAP imlipe pesa zake kwanza kabla ya kupewa fedha za ESCROW.Ajabu PAP wakalipwa ndiyo JR ndiyo akapewa chake. Huhitaji kwenda shule kujua kuwa JR alilipwa pesa za ESCROW. Hizo fedha kuna kodi ndani yake, lakini inasemekana ni haki ya Tanesco. Kosa la JR ni kupokea malipo ya fedha zenye utata ambazo yeye mwenyewe alitahadharisha kabla ya kulipwa. Lakini baada ya kulipwa inatia shaka kwa hao wanaogaiwa. Ni wateule Fulani hivi. Ni sawa JR kauza hisa zake, lakini namna alivyouza, source ya fedha na hao anaowagaia ndiyo tatizo

sio kweli, taarifa zako haziko sahihi. JR alilipwa kwanza na PAP ndipo PAP wakachukua fedha za escrow. JR alikuwa na kesi na IPTL, IPTL ikawekwa chini ya mufilisi, PAP haikuweza ku-take over IPTL mpaka kesi iondoke, ndio maana PAP wakaelewana na Rugemalira kwa kumlipa, na ndipo Rugemalira akaondoa kesi yake mahakamani na hivyo PAP kuruhusiwa kununua hisa za Mechamar/piperlink. PAP walideal na JR september, escrow ilikuwa december!

2010
– Mr Sethi comes to Tanzania, and claims that he had bought 70 per cent of IPTL from the Malaysian company. He attempts to take over the management of the company, but fails because of the winding up petition filed by Mr Rugemalira, the minority shareholder, who owns 30 per cent of IPTL.



September 2013 – Mr Rugemalira finally agrees to sell his 30 per cent stake to Mr Sethi’s company called PAP for $75 million. He is paid an advance of $7 million on the condition that he withdraws his winding up petition filed at the High Court of Tanzania. Mr Rugemalira withdraw the petition, which paves the way for the consent judgment issued by Mr Justice John Utamwa in September.



source: Facts on IPTL deal ahead of the tabling of escrow scam report - National - thecitizen.co.tz
 
Tusijibu juu juu hii hoja. Hata mimi niliposoma katika gazeti la The Citizen mtiririko wa matukio yote ya hili sakata, niliona kama vile JR hana kosa, kwani aliuza hisa zake kabla hata fedha za ESCROW hazijaruhusiwa kugawiwa IPTL. Naomba tujibu hoja kwa hoja, sio kusema tu kuwa mleta mada ametumwa bila ya kujenga au kujibu hoja

Uko sahihi. rugemalira alilipwa kabla ya fedha za escrow hazijatoka.
 
Kama nimelewa vyema, Regemalila alikwisha maliza biashara yake na PAP, kwani PAP walinunua IPTL yote ikiwa ni pamoja na hisa 30% za Rugemalila kupitia VIP Engineering, maana hata tranfer ilifanyika na caiptal gain Tax zililipwa.... sasa inakuwaje anapata mgao katika EScrow ambayo ilitolewa BOT kwa maana ni hela za PAP sio za IPTL ambayo Rugemalila ndio alikuwa na mslahi huko? maana yake Regemalila inawezekana alitumika kugawa rushwa na ndio litakuwa kosa lake

Rugemalira hajapata fedha za escrow, hiyo umeitoa wapi mkuu? PAP walivyokuja walianza kununua kwanza hisa za Rugemalira ili Rugemalira aondoe kesi yake dhidi ya IPTL. Walipomalizana naye ndio wakapiga escrow. James Rugemalira hahusiki na akaunti ya escrow kwa chochote kile.
 
Mkuu ukiangalia hizo hisa utakwama kwenye tope hawa jamaa wamegawana pesa siyo zao na bado wanadaiwa Bilioni 15 na Tanesco, sijui kama umenielewa ndiyo maana Takukuru na CAG wameingia kwenye ili sakata.

Rugemalira hajagawiwa pesa ameuza hisa!
 
Back
Top Bottom