PAP isingeweza kununua hisa za IPTL kutokana na kesi ya Rugemalira dhidi ya IPTL. Na aliyezuia hilo ni MAHAKAMA. Kwa hiyo hata kama sing sethi angekuwa na hela kiasi gani ingebidi kwanza amalizane na rugemalira. Na ndicho kilichofanyika, rugemalira alilipwa ndio akaondoa kesi.
zile pesa ni za tanesco na iptl lakini iptl wamechukua wao zote.
FACTS:
1. James rugemalira alikuwa anamiliki 30% ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP. Asingeziuza hizo hisa, mpaka leo angekuwa bado anamiliki 30% ya IPTL KIHALALI kabisa, hivyo kuwa mbia mwenza wa PAP.
2. James rugemalira aliuza hizo share zake kwa kampuni ya PAP kwa dola milioni 75. Uuzaji wa hizi hisa ulifuata taratibu zote kisheria including ulipaji kodi.
MASWALI:
1. Huyu ndugu anaitwa mwizi kivipi? Amelipwa fedha kutokana na kuuza hisa, tatizo liko wapi hapo? Kisheria angeweza kumuuzia yoyote yule tofauti na PAP hizo hisa kama wangeafikiana bei! PAP wamefikia dau na yeye kawauzia, where is the problem hapo? IPTL sio kampuni ya umma, PAP sio kampuni ya umma, VIP sio kampuni ya umma. This is purely a private sector transaction. Mbona Rostam aliuza share zake vodacom kwa mabilioni tena kupitia nje ya nchi lakini hakuitwa mwizi (kwa kukwepa kodi among other things), badala yake akasherehekewa kwa front-page news? Naomba kufahamishwa kwa hoja tafadhali, uharamia wa James Rugemalira upo wapi.
kuwahonga kwa nini? yeye anamiliki 30% ambazo zina thamani hiyo ya 75mi USD. Sasa hapo ahonge ili iweje? kwani singasinga asingenunua yeye angeumia kivipi? Na je, hao majaji na mawaziri wanahusika vipi na ununuzi wa hisa wa PAP from VIP?
Mkuu inabidi utulie na kuwaza kwa umakini sana ndio utaelewa kilichofanyika hapa. Ruge ameitahadharisha serikali kuhusu utapeli unaotaka kufanyika katika IPTL kwa kuandika barua kibao, ameenda mbali zaidi amefungua amaefungua kesi ili IPTL ifilisiwe. Wakati huo huo mahakama ya kimataifa imeshatoa hukumu IPTL imekuwa ikiicharge TANESCO hela zaidi hivyo inatakiwa ilipwe. Wahusika kwa upande wa serikali hawafanyi hivyo, Sigh (Tapeli) anakuja anataka kuichukua IPTL (ambayo Ruge bado ana hisa 30%, kumbuka Ruge anajua kabisa TANESCO ikilipwa hela iliyokuwa overcharged Ruge naye inakula kwake). Ruge, Sethi na viongozi wala rushwa wakijua hili, wanachelewesha kwa makusudi kutekeleza waliyoamriwa na mahakama ya kimataifa.
Ruge akijua kabisa IPTL inataka kuchukuliwa na Sethi kiujanja ujanja (ameshaitahadharisha serikali, amefungua kesi na anataka ifilisiwe through RITA), akiwa kama mkurungenzi na akijua pia IPTL inatakiwa iilipe TANESCO anaamua kutumia maujanja (kumbuka Ruge ana connections na viongozi na wafanyabiashara, Sethi hana). Anapewa 7milioni ya kianzio kwa kumuuzia TAPELI hisa zake 30%(wewe ni mkurugenzi kampuni yako (IPTL) inatakiwa ilipe pesa kwa TANESCO). Hapa utaona kuwa Ruge akiwakilisha IPTL amekiuka hukumu ya mahakama na ili kujiweka mbali anauza hisa zake fasta kwa kuamua kupokea kianzio kutoka kwa TAPELI.
Naweza kusema with confidence kuwa makubaliano ya kuuziana na Seth yalikuwa influenced na pesa iliyopo account ya ESCROW. Alichofanya Ruge ni kuuza kwa Seth ili yeye asiwe front (kujificha), ndio maana hela ilipokwapuliwa tu Ruge kalipwa. You dont need to be a Professor to see this. Nina uhakika kama TAKUKURU wamefanya kazi yao vizuri ni rahisi sana kumuipmplicate Ruge hapa. Lazima makubaliano ya kuuziana walionyesha hilo salio baada ya kutanguliziwa dola 7m zitalipwa lini. Sasa hapa ndio patamu maana wale wote waliotakiwa kuhakikisha IPTL inailipa TANESCO kama ilivyoamriwa ndio hao hao Ruge amewalipa pesa nyingi. Ruge hawezi kupona hapa. Proper investigation lazima ita uncover deal lote na kama Sethi pia aliwalipa hawa viongozi which is unlikely maana wanyemjua hapa ni Ruge.
Lawyer mzuri anamkamata Ruge kirahisi sana, saaaaaana tu. Kiufupi Ruge ni muhumjumu uchumi na akijua kama mkurungenzi wa IPTL anatakiwa ailipe TANESCO na akijua IPTL inataka kununuliwa kitapeli ameshiriki kufanya uhalifu ndani ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
mimi sio mwenzako mimi ni "interahamwe, FDLR, ideology, RNC, traitor, divisionist, revisionist. A.K.A. BBC!"
1.Ndugu, hiyo IPTL iliwekwa chini ya mufilisi kutokana na kesi ya RUGEMALIRA HUYU HUYU! Ruge alitaka IPTL ifilisiwe ili alipwe fedha zake 30% ya assets. Hivyo hata singasinga asingetokea, bado IPTL ingepigwa mnada Ruge angekula chake pale pale! Mitambo ya IPTL ubungo pale inakubalika kuwa na thamani around $250mil usd. so unaweza kuona bado angekula vijisenti vingi tu. Sasa hapo kuna rushwa gani mpaka eti ahonge watu wa serikali?
2. VIP iliuza hisa zake kwa PAP mwezi september, na deal nzima ilikuwa concluded then! Rugemalira alitoa press statement around August akielezea dili nzima ilivyokwenda. From then onwards, ndipo PAP ikapata uhalali wa kuingilia fedha za escrow. So you see by the time PAP inashughulika na escrow, James Rugemalira alikuwa hayupo!
3. kuhusu escrow account, hii dili ilikuwa kati ya PAP na Tanesco, wote wakakubaliana kuhamisha fedha kwenda PAP. Sasa hapo James rugemalira anahusika vipi tena? Kama kuna ubatili wowote wanatakiwa kufuatiliwa watu wa serikali na PAP sio JR! c'mon; tanesco kuna bodi nzima, wakurugenzi, mameneja, serikalini kuna waziri, naibu waziri, katibu, AG, BOT, Mbona wote hawa hawafuatiliwi anafuatiliwa mtu ambaye kosa lake ni kuuza mali yake kihalali?
Vile vile swali rahisi tu: fedha za escrow ni malipo ya umeme toka IPTL kwenda Tanesco, sasa leo watu wanapodai kuwa actually fedha zote ni za Tanesco na bado Tanesco inadai, maana yake ni nini? kuwa IPTL muda wote huo toka 2006 ilikuwa inazalisha umeme bure?
4. Kuhusu fedha kampa nani, rejea namba 2. Kuwa fedha zake ni halali na ana uwezo wa kumpa yoyote yule. Na zaidi ya hapo kuna USHAHIDI GANI KUWA hivi vielelezo vilivyosambaa humu JF ni vya kweli? Kilichopo ni karatasi reeefu lenye majina ya watu, aliyelitoa hajulikani! Lakini zaidi ya yote hata kama tukifanya wamepewa fedha na JR, je wanahusika vipi katika transaction ya VIP na PAP mwezi september? Kumbuka orodha ina majina kama ya askofu kilaini, watoto na mkwe wa rugemalira, etc, how on earth do these people fit in on all this?
mbona habari zanasema mahakama ya usuluhishi ilitoa majibu kuwa kulikuwa na overcharge mwezi january/february mwaka huu na pesa zilitolewa november/december?. hiyo inaeleza pia kwanini ruge kahonga pesa mwezi february mara baada majibu ya mahakama kuwa mabaya upande wake. hakuwa na intetion ya kugawa pesa kabisa.tanesco hakuwa na chake pale.kumbuka gharama zilishashushwa kutoka 3.6 mil dola kwa mwezi hadi 2.6 mil dola kwa mwezi.na hyo ilikuwa amri ya mahakama ya migogoro ya kibiashara ya kimataifa.tanesco walikata rufaa wakitaka ishuke zaidi ya hapo lakini haijawa hvyo.na hzo hela zimewekwa escrow ikiwa ni tanesco anamlipa iptl kila mwezi.tanesco hana chake pale mpaka iwe vingnevyo.
1. Bado sioni shida iko wapi, hizo 70% ya IPTL ambazo unasema sing sethi kanunua kimagumashi zilikuwa za serikali? Bado masuala yote ya ndani ya IPTL, Mechmar etc, ni mambo ya private sector! Rugemalira hajadeal na serikali yeye ame-deal na PAP! vile vile kwenye suala la Rugemalira kumpinga sethi ni hivi: Rugemalira alikuwa na kesi na IPTL akitaka IPTL ifilisiwe na yeye apate haki zake i.e 30% ya value ya IPTL. Singh sethi alivyokuja hakuweza kununua zilie 70% kwa sababu ya kesi ya rugemalira mahakamani, ikabidi kwanza sethi aelewane na Rugemalira kwa kumpa advance ya 7Mil USD, na ndipo Rugemalira akaondoa kesi mahakamani iliyomuwezesha sethi (and for that matter anyone else) kununua hisa za Mechmar/PiperLink, hata ukiangalia timeline of events unaweza kuona kuwa hata deal yenyewe kati ya sethi na Rugemalira ilifanyika BEFORE hii mambo ya escrow account.
2. Afadhali tunakubaliana kuwa hakuna msingi wowote wa kuchunguza fedha binafsi za mtu zinakwenda wapi. Pili, hakuna taarifa yoyote rasmi inayothibitisha kuwa Rugemalira amewalipa watu gani fedha isipokuwa hizi picha picha za JF. Mtu pekee ambaye inajulikana kuwa kapokea fedha toka kwa Rugemalira ni taasisi ya elimu inayoendeshwa na mama tibaijuka, ingawa baadhi ya watu wanataka ieleweke kuwa zimeingia mfukoni mwa mama Tibaijuka personally! Na sababu pekee inayofanya tujue ni kuwa FEDHA HIZI ZILITOLEWA WAZI WAZI! Hii inaonyesha kuwa mtoaji na mpokeaji wote hawana la kuficha.
tatu, hao watu wanaodaiwa kupewa fedha mbona haionekani kivipi wanaweza kuwa part of escrow account transaction? Hivi mama tibaijuka alipwe bilioni ili afanye nini? Askofu kilaini? Andrew chenge? Roles zao ni zipi kwenye hili sakata? Rejea tena: Rugemalira had 30% of IPTL na hizo ndizo alizouza, na angeweza kuuza kokote kule kwa bei hiyo hiyo, mitambo ya IPTL ubungo pale ni zaidi ya 250mil USD, hivyo hata IPTL ingefilisiwa rugemalira angepata roughly the same amount. Sasa hawa watu wote tunaoambiwa wamehongwa na rugemalira, wamehongwaje?
mbona habari zanasema mahakama ya usuluhishi ilitoa majibu kuwa kulikuwa na overcharge mwezi january/february mwaka huu na pesa zilitolewa november/december?. hiyo inaeleza pia kwanini ruge kahonga pesa mwezi february mara baada majibu ya mahakama kuwa mabaya upande wake. hakuwa na intetion ya kugawa pesa kabisa.
Kosa lake kubwa ni hata hio 30% ownership ni uwizi hajawahi kuweka mtaji hapo
Kwakuwa kazoea kuiba, kudanganya na kutapeli ndio 40 zake zimefika
Hapo umemaliza utata mkuu.Wizi wa Rugemalila ni kupewa pesa kutoka ESCROW TEGETA account ya uma badala ya kulipwa kutoka kwa singasinga upo hapo???
the citizen wanasema mwanzoni mwa mwaka huu mahakama ya usuluhishi ilisema kulikuwa na shida kwenye charges hivyo iptl na tanesco wapige hesabu nani apate nini. jambo baya ni kuwa pesa zilishatolewa disemba. ruge akaanza kuhonga iili kunyamazisha watu. ndiyo maana uhongaji mwingi umefanyika februari baada ya uamuzi wa mahakama.Ruge aliuza hisa zake september. Fedha za escrow zilitolewa December. Mtu kashapata chake ahonge ili iweje?
the citizen wanasema mwanzoni mwa mwaka huu mahakama ya usuluhishi ilisema kulikuwa na shida kwenye charges hivyo iptl na tanesco wapige hesabu nani apate nini. jambo baya ni kuwa pesa zilishatolewa disemba. ruge akaanza kuhonga iili kunyamazisha watu. ndiyo maana uhongaji mwingi umefanyika februari baada ya uamuzi wa mahakama.