Man, are you serious? Suala la rushwa tangu lini likawa ni private matter? Hivi wewe (achilia mbali kampuni) leo hii ukienda hospitali kasha ukampa rushwa daktari ili uhudumiwe hiyo itakuwa ni private matter? RITA yenyewe ni serikali… kuna sheria zinazoongoza RITA na pia kuna sheria pale kampuni inapowekwa chini ya mufilisi wa RITA… si kwamba kwavile ni kampuni binafsi then wenye nayo wanaweza tu kwenda RITA na kusema "we want our company back, itoe kwenye kundi la mufilisi coz' we already have a buyer…!" Hakunakitu kama hicho. Sasa je, sheria zilifuatwa katika kuiondoa IPTL kwenye faili ya mufilisi na kuiuza? Je, ikithibitika kwamba zile statements ni genuine bado huwezi kujiuliza ni namna gani Yule Yule ambae IPTL ilikuwa chini yake amelipwa millions of shillings na wenye kampuni yao!! Hii haiwezi kuwa issue private ya wana-hisa coz' hao wanahisa ni associates kwa maana ikiwa kuna maofisa wa serikali wamehongwa basi hao wanahisa wote watakuwa wamehusika! Hakuna private matter hapo… rushwa ni rushwa tu!
Kwanini amlipe kwanza? Sidhani kama ndicho nilichosema! Nilichosema ni kwamba, hisa za IPTL ambazo ni 70%, Seith alizinunua kwa few thousand dollars wakati 30% ya VIP ziliuzwa kwa millions of dollar… does it make it any sense? Sasa basi nilichosema ni kwamba, kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna ukwepaji wa kodi… nadhani unafahamu kwamba panapotokea mauziano kuna kodi ya capital gain. Hivyo basi, assume kodi halali ambayo Seith alitakiwa kulipa TRA ni 50 billion lakini akalipa 5 million, hapo maana yake ni kwamba, kiasi alicho-save kwenye kulipa kodi halali ndicho hicho ambacho ametumia kulipa some of 30% shares za VIP! Na kwavile huwezi kukwepa kodi kama hii pasipo kuishirikisha TRA, ndipo pale haishangazi kuona kwenye list ya Ruge kuna maofisa wa TRA!
Labda mtu anaweza kujiuiza: Ikiwa hapo muhongaji ni PAP, kwanini basi majina ya maofisa wa TRA yatokee kwenye list ya Ruge! Kuna various possibilities, moja inawekana kabisa kwamba Seith na Ruge walishakubaliana nani a-deal na nani? Ruge yeye alikuwa tayari kwa lolote ili pesa yake aipate, na huwezi juwa… inawekena vile vile kwamba, pesa ambayo Seith aliipata kwa kukwepa kulipa kodi aligawana na Ruge, huku role ya Ruge katika kupata mgao wa ukwepaji kodi huo ikiwa ni kufanya biashara na maofisa wa TRA!
Hukumu ipi? Hii ambayo ilipelekea account ya Escrow kuwa freezed, au? Kama ndiyo, tunafahamu IPTL ilikuwa 70% Mechmar… je, hiyo 30% ilikuwa ya nani kama haikuwa ya VIP? Kama hazikuwa za VIP, sasa kwanini PAP ilitaka ku-settle na VIP? Kwahiyo unataka kusema VIP walikuwa wameshauza 30% ya hisa zake wakati kulikuwa na kesi mahakaman?
Kuhusu kwamba hizo ni tetesi nimeshasema mara kadhaa kwamba, ikishathibitika statements zinazoonekana kwenye mitandao ni genuine then there MUST be something! Kila mtu anafahamu kwamba haijakuwa confirmed! Lakini ikishakuwa confirmed, huwezi kusema kwamba hakuna connection yoyote na PAP… hao walio chini ya tetesi ni government officials ambao moja kwa moja wanahusika kwenye sakata hili! Sion sababu ya kurudia rudia role ya watu wa TRA, sioni sababu ya kurudia rudia role ya watu wa RITA, sioni sababu ya kurudia rudia role ya mawaziri wa zamani wa wizara ya nishati, sioni sababu ya kurudia rudia role ya mtu kama Chenge ambae kama kumbukumbu zangu zipo sawa, wakati Escrow account inafunguliwa yeye alikuwa ndie Mwanasheria Mkuu wa serikali! Sitaki kuamini kwamba bado hapo huoni connection yoyote kati ya hao maofisa wa serikali na PAP!
Mwisho unasema si busara kujadili tetesi lakini sitakii kuamini eti unachomaanisha ni kwamba hakuna maofisa wa serikali waliohongwa unless kama unataka kusema kwamba hata kauli za
Zitto kwamba kuna maofisa kadhaa wamehongwa nazo no tetesi! Je, Zitto nae anaongelea tetesi? Kama sio tetesi na kweli kuna watu wamehongwa, ni ajabu gani miongoni mwa hao waliohongwa kuwa ni hao wanaoonekana kwenye statement ya Ruge? Good enough, majority ya wale wanaoonekana ni wale wale ambao they have some roles in this whole thing! Kwamba humu JF kuna mtu alishapewa ubalozi na baadae kugundulika kwamba si kweli haiwezi kuwa sababu tosha kuhalalisha kwamba kila kisemwacho JF uongo kwavile kuna mambo mengi ambayo yalianzia hapa hapa JF na watu wakabisha lakini hatimae ikabainika kwamba ni KWELI, UKWELI MTUPU!