Kosa la Rugemalira ni nini ?

Kosa la Rugemalira ni nini ?

maana kwenye report ni kuwa Singh alitumia fedha kutoka kwenye Acc ya Escrow kulipia hizo shares
 
maana kwenye report ni kuwa Singh alitumia fedha kutoka kwenye Acc ya Escrow kulipia hizo shares

kazitumiaje wakati alikuwa hajapewa, na kisheria hakuweza kupewa, wewe hiyo ripoti umeisoma kinyumenyume. VIP ilikuwa na kesi na IPTL hivyo Singh hakuweza kudai fedha za escrow. Ndio maana ikabidi anunue kwanza hisa za VIP ndani ya IPTL ndipo akaenda sasa kudeal na escrow account.
 
FACTS:

1. James rugemalira alikuwa anamiliki 30% ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP. Asingeziuza hizo hisa, mpaka leo angekuwa bado anamiliki 30% ya IPTL KIHALALI kabisa, hivyo kuwa mbia mwenza wa PAP.
2. James rugemalira aliuza hizo share zake kwa kampuni ya PAP kwa dola milioni 75. Uuzaji wa hizi hisa ulifuata taratibu zote kisheria including ulipaji kodi.

MASWALI:
1. Huyu ndugu anaitwa mwizi kivipi? Amelipwa fedha kutokana na kuuza hisa, tatizo liko wapi hapo? Kisheria angeweza kumuuzia yoyote yule tofauti na PAP hizo hisa kama wangeafikiana bei! PAP wamefikia dau na yeye kawauzia, where is the problem hapo? IPTL sio kampuni ya umma, PAP sio kampuni ya umma, VIP sio kampuni ya umma. This is purely a private sector transaction. Mbona Rostam aliuza share zake vodacom kwa mabilioni tena kupitia nje ya nchi lakini hakuitwa mwizi (kwa kukwepa kodi among other things), badala yake akasherehekewa kwa front-page news? Naomba kufahamishwa kwa hoja tafadhali, uharamia wa James Rugemalira upo wapi.
Jmali tatizo la Rugemalila ni kuwa amepata fungu kutoka pesa za Escrow. Maana Pesa ya Escrow ni malipo ambayo Tanesco ilikuwa inailipa IPTL huku VIP ikiwa ni moja ya share holders, ina maana baada ya kimagumashi kuonekana pesa ni ya IPTL ina maana kulikuwa na fungu la VIP kwasababu muda wote tangu ESCROW account inafunguliwa mpaka VIP wanauza share kulikuwa kuna percent ya hela ya Escrow ambayo ni mali ya VIP.
 
Jmali tatizo la Rugemalila ni kuwa amepata fungu kutoka pesa za Escrow.

Mbona Rugemalira alilipwa mwezi september kabla fedha za escrow hazijaguswa?
 
Mbona Rugemalira alilipwa mwezi september kabla fedha za escrow hazijaguswa?
Septemba alilipwa gharama ya shares alizouza, lakini kumbuka kabla hajauza kwenye ile hela ya ESCROW kulikuwa na percent yake kama share holder, sasa baada ya hela kuonekana ni za IPTL na zimekuwa zikikusanywa toka 2006 ina maana ktk muda wa 2006 mpaka alipouza shares, 30% ya hela iliyoingia ktk kipindi hicho ilikuwa ni yake.
 
Septemba alilipwa gharama ya shares alizouza, lakini kumbuka kabla hajauza kwenye ile hela ya ESCROW kulikuwa na percent yake kama share holder, sasa baada ya hela kuonekana ni za IPTL na zimekuwa zikikusanywa toka 2006 ina maana ktk muda wa 2006 mpaka alipouza shares, 30% ya hela iliyoingia ktk kipindi hicho ilikuwa ni yake.

si kweli. 75mil usd alizolipwa september ndio kila kitu. Hakulipwa tena fedha nyingine yoyote toka escrow. Unless kama una ushahidi juu ya hilo...
 
si kweli. 75mil usd alizolipwa september ndio kila kitu. Hakulipwa tena fedha nyingine yoyote toka escrow. Unless kama una ushahidi juu ya hilo...
Tuombe Mungu mapendekezo ya PAC yatekelezwe ndio utaelewa role ya Rugemalila na ndio utajua kwanini Mkombozi bank imejikuta katikati ya Kashfa. Lakini ukisoma ukurasa wa 60 wa ripoti ya PAC unasema hivi nanukuu "Baada ya fedha kutolewa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW Ndg. Rugemalira alipata mgao wake wa USD million 75, ambazo ndani yake kulikuwa na kodi ya Serikali ambayo haikukusanywa na gharama za uendeshaji wa Akaunti ya ESCROW, fedha hizo zote zilipelekwa katika Benki ya Mkombozi. Huko zilianza kugawiwa kwa watu binafsi."Kwa hiyo kwa ripoti hiyo utaona kuwa Rugemalila alichukua pesa ya ESCROW na ukiangalia utaona yeye kachukua USD million 75 kati ya 122 kwasababu amechukua pamoja na iliyokuwa kodi ya serikali na charge ya uendeshaji wa Account ya ESCROW ambayo alitakiwa ailipe BOT ila kwasababu yeye ndio alikuwa anaijua system ndio maana akawa anagawa pesa ili kuwapooza watu waliofanikisha na ili wasije wakalipua.
 
si kweli, at this point, ruge hawezi kupelekwa mahakamani, hata huko takuru kwenyewe nahisi faili watalikalia tu kama mafaili mengine. You see, hata ile kumhoji tu mtu unatakiwa kuwa na reasonable doubts. tukirudi kwenye ule mfano wangu wa mimi kukuhoji umepata wapi fedha ya kununua gari wakati kazi yako muuza karanga. Unadhani usiponijibu nikaenda kukushitaki takuru utakamatwa? JR anaweza akaamua kutumia haki yake ya kisheria ya kutojibu chochote huko takuru (kama hata akihojiwa) mpaka pale takuru watakapokwenda mahakamani. Sasa swali linakuja Takuru watamtuhumu JR kwa kitu gani? Sawa kawapa fedha kina chenge, mahakama itauliza so? shida yenu? watajibu nini?
Hakuna sehemu yoyote ile ambapo mtu analazimishwa kusema kwa nini kampa fedha fulani MPAKA PALE swali hilo likiwa ndani ya tuhuma kubwa zaidi, ambazo mpaka sasa hivi HAKUNA!
NImeshakupa maelezo ya kutosha kuwa hata asipopelekwa mahakamani bado haiondoi ukweli kwamba alishrikiana na Seith kuuibia serikali na ku-corrupt gov official kama ambavyo haijafuta ukweli kwamba Chenge alikula rushwa kwenye radar deal ingawaje hadi sasa hajafikishwa mahamakani! Corrupt system ambayo nae imethibitika kwamba amei-corrupt inaweza isimfikishe mahakamani but the invisible system which stands for the interest of the people has already stamped him as a corrupt business person.
 
si kweli. 75mil usd alizolipwa september ndio kila kitu. Hakulipwa tena fedha nyingine yoyote toka escrow. Unless kama una ushahidi juu ya hilo...
Hebu tujuze, ni kwanini moja ya mapendekezo ya PAC ni kuitangaza Mkombozi Bank na Stanbic kwamba zinajihusisha na utakasaji fedha?
 
hapo ndipo ninapopataka, corruption! enhee, mujulizi kapewa fedha ya nini? chenge? Ngeleja? hawa wamemsaidia vipi rugemalira?
Ina maana hujui kwamba Ngeleja alikuwa waziri wa nishati na madini kama ilivyokuwa kwa Yonah huku ikionesha kwamba mawaziri wote waliopitia Wizara ile walilipwa na Ruge? Ina maana hujui kwamba Escrow ilifunguliwa wakati Chenge akiwa AG?
 
FACTS:

1. James rugemalira alikuwa anamiliki 30% ya IPTL kupitia kampuni yake ya VIP. Asingeziuza hizo hisa, mpaka leo angekuwa bado anamiliki 30% ya IPTL KIHALALI kabisa, hivyo kuwa mbia mwenza wa PAP.
2. James rugemalira aliuza hizo share zake kwa kampuni ya PAP kwa dola milioni 75. Uuzaji wa hizi hisa ulifuata taratibu zote kisheria including ulipaji kodi.

MASWALI:
1. Huyu ndugu anaitwa mwizi kivipi? Amelipwa fedha kutokana na kuuza hisa, tatizo liko wapi hapo? Kisheria angeweza kumuuzia yoyote yule tofauti na PAP hizo hisa kama wangeafikiana bei! PAP wamefikia dau na yeye kawauzia, where is the problem hapo? IPTL sio kampuni ya umma, PAP sio kampuni ya umma, VIP sio kampuni ya umma. This is purely a private sector transaction. Mbona Rostam aliuza share zake vodacom kwa mabilioni tena kupitia nje ya nchi lakini hakuitwa mwizi (kwa kukwepa kodi among other things), badala yake akasherehekewa kwa front-page news? Naomba kufahamishwa kwa hoja tafadhali, uharamia wa James Rugemalira upo wapi.




Kwenye payroll nawewe umepata Mgawo wako?
 
hawawezi kujenga kesi kwa kutumia hiyo bank statement kirahisi rahisi hivyo mpaka wathibitishe kuwa waliolipwa pia waliprovide service fulani katika uhalifu. Vinginevyo akisema zilikuwa ni zawadi na wewe huna tuhuma mbadala utamkataliaje?
NIna wasiwasi na uelewa wako kuhusu haya mambo! Yaani bank statement inaonesha kabisa kwamba kuna transactions kutoka PAP hadi a/c ya Ruge na kutoka kwenye a/c ya Ruge hadi kwa gov officials halafu unasena hawawezi kujenga kesi kupitia bank statements wakati hiyo bank statement peke yake inatosha kabisa kumtia Ruge hatiani? Hivi kabisa kwa ufahamu wako Ruge anaweza kabisa kutoa logical explanation ya kuhalalisha malipo ya mabilioni ya shilingi kwa gov and ex-gov officials ambao walikuwa na role kwa namna moja au nyingine kuhusu suala zima la IPTL? Hapo hapo tunakuta staff wa bank hiyo hiyo iliyopitisha hizo transaction nao wamelipwa mamilioni ya TZS?

Trust me, ama teller au bank official ambae alifanya zile transaction alipitiwa au neno sahihi niseme Mungu aliamua kumuumbua Ruge...!! Nasema bank official alipitiwa coz' I can bet, alipewa karatasi lenye majina ya beneficiaries/payees na "kwa bahati mbaya" aka-include haya majina kwenye description! This's was a technical mistake ambayo walikuja kugundua wakati wameshafanya blanda! Mwanzoni mwa miaka ya 2000 kulikuwa na banking system moja ilikuwa inaitwa Easy Bank... am very certain, kama Mkombozi Bank ingekuwa wanatumia Easy Bank, lazima wangefanya data restoration na kuanza ku-run upya from the day Ruge alipofanya hizi corrupting transactions ili ku-clean up the mess!
 
hawawezi kujenga kesi kwa kutumia hiyo bank statement kirahisi rahisi hivyo mpaka wathibitishe kuwa waliolipwa pia waliprovide service fulani katika uhalifu. Vinginevyo akisema zilikuwa ni zawadi na wewe huna tuhuma mbadala utamkataliaje?
Sehemu ya Ripoti ya PAC hii hapa:
Kamati inajiuliza ni nini mahusiano ya moja kwa moja kati ya Viongozi hawa na malipo yaliyotokana na Akaunti ya Tegeta ESCROW. Mfano kwa upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb), ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi bilioni 1.6; Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6; Mhe. William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4 na Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4; Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4 na Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.

Upande wa Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu Methodius Kilaini shilingi 80.9, Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4

Kamati ilithibitishiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuwa baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa. Kutokana na muamala uliofanyika tarehe 6 Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi kiasi cha shilingi bilioni 3.3 na muamala wa Benki ya Stanbic wa tarehe 23 Januari 2014 ambapo fedha taslimu (cash) kiasi cha shilingi bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006
Kamati pia inaendelea:
Kamati imejiridhisha kwamba, suala la akaunti ya Escrow ni jambo la utakatishaji wa fedha (Money Laundering), kama alivyosema Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU katika mahojiano yake na Kamati. Kamati inazitaka mamlaka zinazohusika, ikiwemo Benki Kuu kuzitangaza benki za Stanbic na Mkombozi Commercial Bank kama asasi za utakatishaji fedha (Institutions of Money Laundering Concern).
Sasa wakati Kamati imethibitisha kwamba Mkombozi Benki imehusika kwenye utakatishaji wa fedha haramu,bado unataka kutuambia muhusika mkuu katika utakatishaji huo kwa upande wa Mkombozi Bank ambae ni Ruge yeye ni Clean Guy!!!!
 
Hivi Singasinga ye hajagawa kwa watu binafsi au ye yupo kiprofeshno zaidi? huko kwa Singh ndo kwaweza kuwa kuna madudu ya hatari
 
PAP walimlipa Ruge KABLA hawajaiba fedha za escrow! Fedha za PAP kwenda VIP hazikutoka escrow account.
Hayo ni maneno yako wewe, sehemu ya Ripoti ya PAC hii hapa:
Rugemalila alithibitisha kuwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo alimwomba kuwasilisha kiasi cha fedha ambacho angependa kulipwa na IPTL ili kumaliza Shauri lililokuwepo mahakamani. Aidha, Bw. Sethi aliwasilisha kwa Bw. Rugemalira ushahidi kwamba PAP imenunua Hisa 7 za Mechmar katika IPTL.
Kwahiyo hapo Ruge si kwamba alikuwa amelipwa, bali ndipo alipeleka proposal yake ya kiasi gani cha fedha anahitaji kwa ajili ya hizo 30% Shares. Baada ya Ruge kupeleka hiyo proposal, PAC wanasema
Mchakato wote wa kutoa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW ndipo ulipoanza
Na
baadaye kuhitimishwa na maamuzi ya Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013 ambayo ndiyo yaliyotumika kuhalalisha utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba, 2013.
Je, hapo VIP walikuwa wameshalipwa kama unavyodai wewe, Gazeti la The Citizen ambao ndio waliibua hili sakata, February 09,2014 wakawasiliana na Braza Ruge na Ruge akatuma sms. Ruge huyu hapa:
Lucas, since 24th January 14 VIP transferred its 30% shares in IPTL to PAP (Pan Africa Power Solutions (Tanzania) Ltd. I advise you to contact Mr Singh (+255767xxxx) on all questions concerning IPTL. James. Cc. Dr Singh.
The Citizen wana-clarify
Lucas is a reporter with The Citizen.
Which means, ingawaje PAC wanasema
maamuzi ya Mahakama Kuu ya tarehe 5 Septemba, 2013 ambayo ndiyo yaliyotumika kuhalalisha utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba, 2013.
Lakini Ruge alikuja kufanya share transfer on January 24, 2014 baada ya:
utoaji wa fedha katika Akaunti ya Tegeta ESCROW tarehe 28 Novemba hadi 5 Desemba, 2013.
Na The Citizen, waibuaji wa sakata hili wanahitimisha:
The Citizen has reliably established that the money used to pay VIP Ltd to wholly acquire IPTL plants came from the Escrow account established at the BoT.
MASWAAALI???!! The Citizen hawa hapa:
www.thecitizen.co.tz/News/-270m-deal--Story-of-IPTL--PAP-and-High-Court/-/1840392/2228606/-/item/0/-/12h5eoqz/-/index.html
 
matanzania mengine mabishi sana.fedha alizogawa rugemalila ni haramu ni mali ya wananchi.waliogawiwa pia ni wezi ikiwemo askofu kilain.majizi.dunia ya leo unapokea mamilion bila kuyafanyia kazi na huulizi.kilain kayadhalilisha makanisa afukuzwe
 
Hee! Hii sasa kali… baada ya kutubishia sasa umeamua kujibishia hata wewe mwenyewe!!!! We si uliniambia sifahamu utendaji kazi wa RITA na kwamba IPTL haikuwa chini ya mufilisi Hebu jikumbushe:
Ukarudia tena kuonesha msisitizo:
Mara eh, saa chache baadae wewe yule yule:

Afanalek wallah, nchi ina viroja hii!!!

Spot on mkuu. Huku kwetu rwanda jaamaa anajiitaga "intellectual". Leo amekutana na watanzania walioenda shule. Usishangae kumuona akitoweka na kurudi kwenye jukwaa lake "international forum"
 
Back
Top Bottom