Kosa la Rugemalira ni nini ?

Kosa la Rugemalira ni nini ?

NImeshakupa maelezo ya kutosha kuwa hata asipopelekwa mahakamani bado haiondoi ukweli kwamba alishrikiana na Seith kuuibia serikali na ku-corrupt gov official kama ambavyo haijafuta ukweli kwamba Chenge alikula rushwa kwenye radar deal ingawaje hadi sasa hajafikishwa mahamakani! Corrupt system ambayo nae imethibitika kwamba amei-corrupt inaweza isimfikishe mahakamani but the invisible system which stands for the interest of the people has already stamped him as a corrupt business person.

Asante mkuu. Tunakuhitaji mkuu kwenye jukwaa la kimataifa manake hizo ndio zake. Yeye husema eti kwa sababu mtu aliuua lakini mahakama ikamuachia basi yeye hana hatia ijapokuwa majirani walimuona na macho yao. Can you believe the logic of this man?
 
Man, are you serious? Suala la rushwa tangu lini likawa ni private matter? Hivi wewe (achilia mbali kampuni) leo hii ukienda hospitali kasha ukampa rushwa daktari ili uhudumiwe hiyo itakuwa ni private matter? RITA yenyewe ni serikali… kuna sheria zinazoongoza RITA na pia kuna sheria pale kampuni inapowekwa chini ya mufilisi wa RITA… si kwamba kwavile ni kampuni binafsi then wenye nayo wanaweza tu kwenda RITA na kusema “we want our company back, itoe kwenye kundi la mufilisi coz’ we already have a buyer…!” Hakunakitu kama hicho. Sasa je, sheria zilifuatwa katika kuiondoa IPTL kwenye faili ya mufilisi na kuiuza?
Kwa maelezo yako nahisi inawezekana hujui kazi ya RITA na jinsi inavyofanya kazi, naomba ufuatilie na kujiongezea ufahamu how RITA works. Kuna hatua za ufilisi na si kila kampuni inayowekwa chini ya RITA maana yake imefisilika au ndio inafilisiwa. IPTL iliwekwa RITA katika level ya uangalizi, hawakuwekwa katika hatua ya ufilisi. katika hatua iliyowekwa IPTL iliruhusu kuondolewa hadhi ya kuwa chini ya RITA na kurudishwa kwa wenyewe pale ambapo financial affairs zake zitatengemaa. Na ndicho hicho kilichofanyika. Amri ya mahakama kutokana na maombi ya James Rugemalira akidai haki yake, ndio yaliyoweka IPTL chini ya RITA, na amri ya mahakama kutokana na maombi ya James Rugemalira huyu huyu baada ya kulipwa chake na Sing sethi, ndio yaliyoondoa IPTL chini ya RITA. Mbona kila kitu kiko straight forward?



Again, kama hujui kazi ya RITA lazima utatuhumu rushwa, lakini once ukijua, utagundua kuwa there is ABSOLUTELY NOTHING OF THE SORT. kampuni zinawekwa chini ya RITA kwa amri ya mahakama na zinaondolewa kwa amri ya mahakama. kama kuna mtu wa RITA amelipwa amelipwa kwa ishu zingine, vinginevyo thibitisha (ukionyesha ni jambo gani ambalo ofisa wa RITA kafanya kumsaidia JR).


Mkuu unachanganya mambo, there is no doubt kuwa sethi kakwepa kodi kwenye transaction ya kununua 70% za IPTL. Lakini hoja yangu ni kuwa hilo HALIMHUSU Rugemalira. Sethi alianza kwanza kumnunua Rugemalira kwa 75mil usd mwezi september! By the time sethi ananegotiate hizo 70%, alikuwa tayari anamiliiki 30% aliyonunua kwa Ruge. Ukwepaji kodi wa Sethi unamhusisha vipi Rugemalira tena? Kama Ruge alitumwa na sethi kuwalipa TRA ili wafoji kodi ya sethi hilo ni jambo lingine, lakini huwezi tu kudai Ruge anahusika na ukwepaji kodi wa Sethi mpaka uonyeshe uhusiano. Na hilo litahitaji uchunguzi wa vyombo vya sheria sio conspiracies za JF! Lakini kwangu itakuwa ngumu kuamini hivyo kwa kuwa Rugemalira hakuwa na shida kiasi hicho. Hisa zake zilikuwa pale pale, na mitambo ya IPTL ilikuwa pale pale, haki yake angepata tu hata iweje! In fact ni sethi ndio alikuwa na shida ya IPTL sio Ruge alikuwa na shida ya fedha za sethi. Hivi unajua kuwa Ruge mbali na bei ya hisa za VIP pia alitoa masharti kwa yoyote atakayenunua juu ya bei ya umeme?


Hii ni conspiracy, tetesi, uvumi ambao kwa great thinkers hatupaswi ku-entertain. Viko vyombo vya sheria, na ripoti inasomwa leo, let's hear them. Sethi ni kweli amekwepa kodi na TRA wanawajibika, lakini kujifanya sisi ni wachunguzi kiasi cha kuchafua majina ya watu sio vizuri. Wacha sheria ichukue mkondo wake.

Kutokana na kesi ya VIP, IPTL iliwekwa chini ya mufilisi (RITA) katika mchakato wa kuanza kufilisiwa (ingawa haikufikia stage hiyo), ili PAP anunue IPTL ilibidi aanze kwanza ku-deal na VIP ili IPTL itoke kwenye status ya mufilisi, na ndipo iwe na uwezo wa kuuza hisa zake.



Mpaka sasa hakuna ushahidi, hivi nikikuuliza hayo majina yametoka wapi utanijibu nini? Huwezi kuanza kujenga hoja juu ya kitu ambacho hakijathibitishwa wala hakijulikani usahihi wake. Akaunti tunaambiwa ni ya rugemalira, je aliyetoa hiyo statement ni nani? Mwanae, mkewe? Majina yaliyoko sawa ni ya viongozi wa zamani wa serikali. so what? Msingi mzima wa hoja yako umejengwa kwenye assumption kuwa Ruge katumiwa na sigh sethi kukwepa kodi! msingi ambao kwangu hauwezekani. Orodha ina majina mengi zaidi ya raia wa kawaida kuliko hao viongozi wa serikali, je mtu kama waziri tibaijuka amehusikaje? wakati wa hiyo escrow yeye alikuwa nani?

Anyway naomba tusitishe mjadala mpaka baada ripoti itakapotolewa leo, tujue mengi zaidi.

Well said
 

Mod, naomba msiunganishe thread hii na nyingine ili nipate majibu kuhusiana na malipo ya fedha aliyopata Rugemalira kutokana na kuuza hisa zake 30% kihalali kabisa. Naomba ninukuu sehemu ya taarifa ya PAC, halafu wadau wakisoma wanijibu maswali haya:
i) Je, kosa la Rugemalira ni lipi, kuuza hisa zake?
ii) Si halali kwa mtu kupokea hela ya malipo bila ya kulazimika kujua ilikotoka?
iii) Si halali kwa mtu kutumia fedha yake halali kwa jinsi anavyotaka, ikiwa ni pamoja na kuchangia hela ktk harambee mbalimbali?

Naomba nijibiwe taratibu bila ushabiki, tena kwa hoja zenye ushahidi wa taarifa ya PAC au kutoka sehemu nyingine. Sina maslahi yoyote na upande wowote, ila nataka tujadiliane hapa.


Taarifa ya PAC said:
Mheshimiwa,

Kamati haina tatizo na watu wawili kuuziana makampuni yao kwa thamani wajuazo wenyewe, au jinsi ya kuzitumia fedha zao, ama kuwachagulia watu wa kuwagawia, lakini Kamati imejidhihirishia kuwa fedha iliyotumika kulipia manunuzi hayo ni fedha ambayo sehemu yake ni ya umma iliyochotwa bila huruma wala aibu, kutoka Benki Kuu. Hivyo, Kamati inazitaka mamlaka za uchunguzi kuhakikisha kuwa fedha hizo zinarudi Benki Kuu hata ikibidi kwa kufilisi mali za watu wote waliofaidika na fedha hizo kwa thamani ya fedha walizopewa na Bwana Rugemalira.
 
Hayo ni maneno yako wewe, sehemu ya Ripoti ya PAC hii hapa:Kwahiyo hapo Ruge si kwamba alikuwa amelipwa, bali ndipo alipeleka proposal yake ya kiasi gani cha fedha anahitaji kwa ajili ya hizo 30% Shares. Baada ya Ruge kupeleka hiyo proposal, PAC wanasema Na Je, hapo VIP walikuwa wameshalipwa kama unavyodai wewe, Gazeti la The Citizen ambao ndio waliibua hili sakata, February 09,2014 wakawasiliana na Braza Ruge na Ruge akatuma sms. Ruge huyu hapa: The Citizen wana-clarify Which means, ingawaje PAC wanasema Lakini Ruge alikuja kufanya share transfer on January 24, 2014 baada ya: Na The Citizen, waibuaji wa sakata hili wanahitimisha: MASWAAALI???!! The Citizen hawa hapa: www.thecitizen.co.tz/News/-270m-deal--Story-of-IPTL--PAP-and-High-Court/-/1840392/2228606/-/item/0/-/12h5eoqz/-/index.html

asante kwa hii info.
 
Tuombe Mungu mapendekezo ya PAC yatekelezwe ndio utaelewa role ya Rugemalila na ndio utajua kwanini Mkombozi bank imejikuta katikati ya Kashfa. Lakini ukisoma ukurasa wa 60 wa ripoti ya PAC unasema hivi nanukuu "Baada ya fedha kutolewa kwenye Akaunti ya Tegeta ESCROW Ndg. Rugemalira alipata mgao wake wa USD million 75, ambazo ndani yake kulikuwa na kodi ya Serikali ambayo haikukusanywa na gharama za uendeshaji wa Akaunti ya ESCROW, fedha hizo zote zilipelekwa katika Benki ya Mkombozi. Huko zilianza kugawiwa kwa watu binafsi."Kwa hiyo kwa ripoti hiyo utaona kuwa Rugemalila alichukua pesa ya ESCROW na ukiangalia utaona yeye kachukua USD million 75 kati ya 122 kwasababu amechukua pamoja na iliyokuwa kodi ya serikali na charge ya uendeshaji wa Account ya ESCROW ambayo alitakiwa ailipe BOT ila kwasababu yeye ndio alikuwa anaijua system ndio maana akawa anagawa pesa ili kuwapooza watu waliofanikisha na ili wasije wakalipua.

Asante kwa mchango wako, nimepata taarifa mpya ambazo zinahusisha fedha za escrow na VIP. Kilichonichanganyani kuwa mwezi september VIP walilipwa advance ya 7mil USD, na ndipo wakafuta kesi, na baadaye wakaja kumaliziwa balance kwa fedha za escrow.
 
...hajaonewa, nilitaka Jmali anijibu khs fedha alizolipwa Ruge kuwa zilitoka wapi, hata hivyo umefafanua vizuri
Inaelekea hata mimi nili-quote kimakosa... nimerejea mjadala nikakuta nilikusudia kum-quote jMali
 
Last edited by a moderator:
Jmali, ni imani yangu kuwa unaangalia bunge now, na unamsikiliza mbatia, kama sivyo naomba utafute mchango alioutoa mbatia, ili uweze kujua kuwa JR kama amesingiziwa au
 
Mtoaji rushwa na mpokeaji rushwa wote wana kesi ya kujibu,
Swali: Mbona Rugamalira apandishwi mahakamani??
 
Rugemalira ameiweka Serikali mfukoni, je nani ana ujasiri wa kumpeleka kwenye vyombo vya sheria? Takukuru na mahakama watawahangaisha vidagaa tu lakini Ruge No
 
Mimi nashangaa mtu mzima anamtetea Ragamalira kuwa yuko clean, ina maana hana uchungu na nchi yake
 
Kama rugamalira hana kosa basi hao wanaofunguliwa kesi bandia hawana sababu ya kufikishwa mahakamani
 
Mtoaji rushwa na mpokeaji rushwa wote wana kesi ya kujibu,
Swali: Mbona Rugemalira apandishwi mahakamani??

Mkuu Msembuzi
Jibu la swali lako lipo Cristal clear kuwa Takukuru wamehongwa na Ruge kama ilivyoandikwa katika ripoti ya utafiti wa Afroberometer.
Rugonzibwa kabadilishiwa mashitaka na Takukuru sasa anashitakiwa kwa kupokea RUSHWA mtoaji hiyo Rushwa hajashitakiwa kulikoni?
 
Kama rugamalira hana kosa basi hao wanaofunguliwa kesi bandia hawana sababu ya kufikishwa mahakamani

Mkuu hili ni Movie ya kawaida kama nyingine tulizozizowea kuziona hapa Tanzania,Steering wa Movie hii ni Dr mkuu wa TKKR.
 
Rugemalira ameiweka Serikali mfukoni, je nani ana ujasiri wa kumpeleka kwenye vyombo vya sheria? Takukuru na mahakama watawahangaisha vidagaa Ruge No
Huyu raisi mkuu Jk ni makamu wake Rugemalira akipelekwa mahakamani nchi itatisika
 
Back
Top Bottom