Korogwe, Tanga: Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa

Inatisha... Kwa anayefahamu.
View attachment 1897131

Waliomburuza Jamaa Kwenye Bodaboda Mpaka Kumuua Wakamatwa​

Global Publishers Aug 11, 2021
article_image_1628677907280.jpeg

JESHI la Polisi mkoa wa Tanga linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kumshambulia na kumuua mtu mmoja aliyetuhumiwa kuiba pikipiki huko Korogwe.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga amesema marehemu alituhumiwa kuiba pikipiki Korogwe Tanga, Julai 27, mwaka huu na kutokomea nayo kusikojulikana.

Baada ya kufanya tukio hilo, Madereva bodaboda wa eneo aliloiba pikipiki hiyo wakaanza kumsaka ambapo baada ya siku chache walimkamata akiwa na pikipiki hiyo.

“Baada ya kumkamata walianza kumshambulia kwa vipigo kisha kumfunga kamba kwenye pikipiki na kuanza kumburuza barabarani (barabara ya vumbi). Hata hivyo, kutokana na majeraha makubwa aliyoyapa, mtu huyo alifariki dunia.

“Mpaka sasa tumewakamata watu 11 kwa kwa ajili ya uchunguzi na kuhusika na tukio hilo la kinyama. Uchuguzi ukikamilika tutawafikisha mahakamani,” amesema Chatanda.

Aidha, RPC Chatanda amewataka wananchi kutojichukulia hatua za kisheria mikononi kwani ni kuvunja sheria, hivyo iwapo kuna uhalifu basi waripoti katika vyombo vya sheria.
Wapewe onyo na kuachiwa huru ukatili wa wezi wa bodaboda unatisha jinsi wanavyowafanyia wanaowapora

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Usisahau wakitaka kukuibia watakuchoma hata kwa bisibisi. Acha wafe tu.

Tofauti yako na wao inakua wapi hapo?
Nimeshaibiwa sana na wameniingiza hasara sana tu. Lakini kumuua au kumburuza mtu kiasi hicho hadi mauti imkute sio jambo la kufurahia.
 
Endelea kuomba Mungu usiingie katika mikono ya wezi/majambazi ili uendelee kuhubiri ubinadamu pindi wanapokamatwa!!

Nakukumbusha tu: watakupiga bila huruma, ikiwa bahati kwako ufe au laah upone ujikute pengine mlemavu!! Na hali hiyo hiyo polisi nao wanataka kula hapo kwako, yaan umeporwa na umeumizwa pengine ulilazwa mawiki kadhaa hospitali bado unafuatilia upelelezi polisi wanataka chochote kitu.

Kuna mengine kama kudhalilishwa mbele ya mkeo na familia, Kupoteza ajira kutokana na ulemavu!! Daaaah! Bro, endelea kuhubiri ubinadamu kwa wezi, Mungu atakulipa
Nilishawahi kuibiwa,si mara moja!Nilishawahi kupoteza ndugu kwenye jaribio la wizi na mwaka jana kijana niliyempa pikipiki aliporwa kwa kupewa soda iliyokuwa na madawa!Alikuja kuzinduka baada ya siku 2 hospitali na pikipiki ilikuwa imeshaenda!
Pamoja na hayo,sijawahi kupata hata wazo la kufanya unyama wa kiasi hiko!Kuangalia tu hiyo video nimeshindwa!
I will never stand so low and do such a thing to a human kind!
 
Ila wezi wao wakiwa wanachinja hao bodaboda wanakua wako sawa kichwani?
Hapana,hawako sawa!Hawana ubinadamu!
Ona sasa watu wanaenda kufungwa maisha kwa ujinga wao!
Hapo ni kutokuwa na utu lakini ni ujinga!
 
Kwanini wanarekodi?? Sioni haja ya kurekodi na masauti yao kabisa na sura zao aisee hawa jamaa bna.

Yani mpaka leo kuna watu hawajui kua kuuua ni kosa la jinai, wao walitegemea polisi watawasifia au ni kipi hasa walichotegemea??

Na kuna mwamba alikua anamrudia na gari mwenzie tabata kule sijui aliishia wapi yule.
 
Hivi hawa wezi wa toyo si hua wanawapiga nondo au kuwachinja dereva wa bodaboda ili wachukue hizo pikipiki?
Hata kama wanafanya hivyo bado haihalalishi kufanya ujinga huo!!sasa wamefaidika nini nao wanaenda kufia jela kutokana na maamuzi ya kipuuzi hayo!!hata kama wangekuwa wamemkamata kweli ameiba kulikuwa na njia za kumfanya ambazo zisinge wapelekea kwenye matatizo hayo!!
 
Tofauti yako na wao inakua wapi hapo?
Nimeshaibiwa sana na wameniingiza hasara sana tu. Lakini kumuua au kumburuza mtu kiasi hicho hadi mauti imkute sio jambo la kufurahia.
Mwaka 2017 katika kijiwe chetu kwa kopa kuna mmoja aliibiwa pikipiki waliomuibia pikipiki walimtoboa macho jamaa na kuondoka na pikipiki.

Mwaka huo huo nyuma ya Victoria Service Station ya Ali Hassan Mwinyi Road kuna bodaboda wa kijiwe cha Victoria aliporwa pikipiki akaibiwa hesabu ya siku na kuumizwa.

Mwaka 2018 kuna dereva bajaji aliuawa na kuporwa bajaji eneo pa Uporoto ya Mwananyamala Bwawani.

Mwaka 2018 hiyo hiyo kuna dereva bodaboda alipigwa na kuibiwa pikipiki eneo hilo hilo la Uporoto.

Mwaka 2018 hiyo hiyo aliuawa jamaa aliyemleta dereva bajaji hilo eneo la Uporoto ili kumuibia bajaji. Aliokua nao walikimbia.

Mwaka 2018 mwanakijiwe aliibiwa pikipiki Sinza kwa kipigo.

Mwaka 2018 deiwaka alitapeliwa pikipiki kwa kudanganywa anagewa dili ya kusafirisha mirungi.

Mwaka 2019 mwanakijiwe aliibiwa pikipiki Keko at knife point huku wauza vitumbua na samaki wa hapo mtaani wakiangalia.

Hayo ni matukio ninayoweza kuyakumbuka kwa haraka ambayo yalihusisha kutishia uhai. Bodaboda wakiungana kumshughulikia mwizi kwa ambaye nishakua in action naelewa kwanini wanafanya hivyo.

Utakuta pikipiki wanaiba wako watatu au wanne. Wanaiuza kuanzia laki nne mpaka nane so kwa wastani wanapata laki mbili kwa tukio. Kama yeye yupo radhi kuua mtu ili apate laki mbili kwanini asiwe radhi kufa kwa laki mbili hiyo hiyo?

Bome-e
 
Mbombo ngafu, mbombo jilipo
 
Hao jamaa ni wajinga sana wameona haitoshi wameamua hadi kuchukua video ili kutaka sifa.
Wasubiri mvua ya kutosha
 
Back
Top Bottom