Korea Kusini nchi yenye hifadhi kubwa ya silaha duniani wakataa kutoa silaha zaidi kwa Ukraine

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Raisi wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ameondoka nchini Ukraine kurudi Seul baada ya kufanya ziara ya kustukiza akitokea Vilnius nchini Lithuania.

Raisi huyo wa Korea Kaskazini alikuwa alihudhuria kikao cha NATO kilichokutana kujadili masuala mbaimbali likiwemo suala lla misaada zaidi kwa Ukraine ambayo iko vitani na Russia.

Akiwa mjini Kyiv raisi Yoon alikutana na raisi wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na kumuahidi kumpatia msaada zaidi ingawa usio silaha kali (non-lethal weapons).

Korea Kusini imeahidi kuipatia Ukraine msaada kama mavazi ya kujilinda (Body Armour), vifaa vya kuondoa mabomu (Demining Devices) na kofia ngumu (Helmets) lakini si silaha na vifaa vingine vizito kama munitions na silaha zingine ndogondogo.

Korea Kusini ni nchi yenye hifadhi kubwa ya silaha duniani zingine tayari ikiwa ilikwishatoa huko nyuma kwa ombi la Marekani. Korea Kusini pia ni nchi ya tisa duniani kwa biashara ya silaha na mshirika wa karibu wa Marekani.

Itakumbukwa kuelekea mwishoni mwa mwaka jana raisi Joe Biden alifanya ziara nchini Korea Kusini na baada ya hapo nchi hiyo ikatuma shehena kadhaa ambazo kwa njia ya nyuma (Indirectly) zikaenda kwa Marekani ambapo nchi hiyo nayo ikapeleka mzigo huo nchini Poland ili Ukraine iweze kupewa mzigo huo.

Lakini taarifa za kijasusi zimedai kuwa Russia ambayo ni nchi rafiki wa Korea Kaskazini kupitia ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi pamoja na Korea Kaskazini walifanya mazungumzo jna tangia hapo Korea Kusini hawajatuma tena silaha kwa Ukraine na hawatofanya hivyo. Hiyo ni kutokana na sheria na katiba ya nchi hiyo ambayo yakataza kutoa silaha katika sehemu zenye migogoro kama vita ya Ukraine.

Hata hivyo Korea Kusini imekuwa ikishiriki katika kampeni ya kuisaidia Ukraine ukiwemo msaada wa fedha zaidi ya Euro milioni 100 ambazo nchi hiyo iliipatia Ukraine na mapema mwaka huu ikatoa tena msaada wa Euro Milioni 150.

Pamoja na msaada huo wa fedha Korea Kusini imeshiriki kutengeneza vikwazo vya kiuchumi kwa Russia, kutoa kauli za kuilaumu Russia (rhetoric statements) na pia kusaidia teknolojia vita vya taarifa (technological information wars).

Taarifa hizo za kijasusi zimedai kuwa Korea Kusini safari hii wamekataa kutoa msaada wa kijeshi (vifaa vya kijeshi) kwa Ukraine kwa kuogopa kuharibu ushirikiano na Kremlin ambayo ni wa kihistoria na pia kuogopa kusababisha Kremlin kuipa nguvu zaidi Korea Kaskazini ambayo ni nchi yenye uhasama wa kihistoria na Korea Kusini.

Nchi nyingi zilounda umoja wa nchi za kujihami wa NATO zimegundua kuwa zimeingizwa mkenge na Marekani kwa kuwepo katika misheni ambayo haijulikani mwisho wake. Kitendo cha nchi hizo ambazo nyingi ni zile zilojiunga juzijuzi na zilokuwa sehemu ya USSR zimejikuta katika wakari mgumu kwani zimeingia woga kuwa iko siku nazo zaweza kushambuliwa na Russia na hata Belarus.

NATO haiwezi kuona ukweli kwamba katika karne hii ya 21 kuwa kwa kuifuata Marekani na sera zake za mambo ya nje ni kujitengenezea mazingira ya kuja kupqta shida siku za usoni.

Nchi kadhaa sasa hivi zaunda umoja wa BRICS, ambao ni muunganiko wa nchi za Brazil Russia India na China na ambao sasa hivi umoja huu wazidi kupata maombi ya uanachama kutoka katika nchi kadhaa kama Argentina, Iran, Saudi Arabia, South Africa, Egypt, United Arab Emitrates, Nigeria, Mexico na Algeria. Nchi zaidi zimeonyesha dhamira ya kujiunga na BRICS.

Mapema mwaka huu BRICS imetangaza kuwa nchi zipatazo 19 zimeomba kujiunga na BRICS zikiwemo Venezuela, Senegal, Uganda, ZImbabwe, Cuba, Angola, Gabon, Guinea Bissau, Honduras, Pakistan, Afghanistan, Belarus, Comoros, Syria, Sudan na Kazakhstan.

Pamoja na maazimio mengi yaliyomo katika uundwaji wa BRICS matumizi ya njia mpya za ubadilishanaji fedha ambazo zitatumika badala ya mfumo wa SWIFT. Mifumo hiyo ni ule wa CIPS (Cross-Border Inter-Bank Payment System wa China, SPFS(system for Transfers for Finanscial Systems) wa Russia, SFMS(Structured, FInancial Management System) wa India na mfumo wa Pix unotumiwa na benki kuu ya Brazil.

Kuundwa na BRICS na ukuaji wa wanachama wake ni tishio kubwa kwa ustawi wa bara la Ulaya na Marekani katika uimarishaji uchumi wake na mahusiano yake ya kimataifa kati yake na mabara mengine.

Vyanzo:

Reuters, NBC, Financial Times na kijarida cha Spytalk.
 
Screenshot_20230602-192931.jpg
 
Urusi ni miamba aisee.
Urusi anapambana na karibia silaha za Dunia nzima.
Huu mgogoro ndo umenifanya nijue kwa Nini NATO iliundwa
Huna akili., Urusi anakuwaje mwamba?
Mwamba aliyeekwa kati ni kikundi kidogo cha Wagner ambacho alikitengeneza mwenyewe, wakachukua kituo cha jeshi Rostov bila kuua hata kuku? Putin akajificha chumba chini ya ardhi mpaka rais wa Belarus alipomuangukia Prigozhin putini akakubali masharti mbio mbio kwa usalama wake na udikteta wake., Madevdev alikimbia usiku ule ule na ndege akatokomea kusikojulikana

Unafkiri siku NATO wakiamua kutumia Jesho la nchi 32 duniani kuingia vitani na Putin inaweza chukua hata dakika 10 nchi iitwayo Russia haijapotea kwenye ramani ya dunia na kubaki vumbi tupu
 
Wewe huna akili Wagner hana shida na urusi na kiongozi wao anaongea mpaka na putin.wagner ni sehemu ya jeshi la urusi.
 
Huna akili., Urusi anakuwaje mwamba?
Mwamba aliyeekwa kati ni kikundi kidogo cha Wagner ambacho alikitengeneza mwenyewe, wakachukua kituo cha jeshi Rostov bila kuua hata kuku? Putin akajificha chumba chini ya ardhi mpaka rais wa Belarus alipomuangukia Prigozhin putini akakubali masharti mbio mbio kwa usalama wake na udikteta wake., Madevdev alikimbia usiku ule ule na ndege akatokomea kusikojulikana

Unafkiri siku NATO wakiamua kutumia Jesho la nchi 32 duniani kuingia vitani na Putin inaweza chukua hata dakika 10 nchi iitwayo Russia haijapotea kwenye ramani ya dunia na kubaki vumbi tupu
Unafikiri NATO hawatamani kuona vumbi la Urusi? Unahisi ni nini wanaogopa? Kama unavyoona wamedhibitiwa nchi 30+ na hawana namna basi elewa huo ndio uwezo wao wa mwisho, wamebakiza mbinu chafu za kuviziana maana wakienda Vita ni Vita......unachokiona kinatokea Ukrain ndio "live simulation" ya vita kati ya Urusi na NATO, unahisi West wana huruma na Urusi hadi kuwatoa sadaka raia wa Ukrain kwa kuwapa pesa wapambane na Urusi...au unahisi pale West wanafanya mchezo wa kuigiza.
Wanakijua watakachokipata..
Hakuna wazungu wanakubali kufa waache mapesa yao waliyowekeza kwenye miradi yoote dunia hii kisa wanataka waifanye urusi vumbi...shtuka wewe..
 
Russia hana lolote huyo ni joka la kibisa tu, leo hii akipewa hata Poland tu anammaliza kama Ukraine tu mwaka wa pili amemshinda na hajui vita vitaisha lini yaani yuko gizani kabisa.
 
Huna akili., Urusi anakuwaje mwamba?
Mwamba aliyeekwa kati ni kikundi kidogo cha Wagner ambacho alikitengeneza mwenyewe, wakachukua kituo cha jeshi Rostov bila kuua hata kuku? Putin akajificha chumba chini ya ardhi mpaka rais wa Belarus alipomuangukia Prigozhin putini akakubali masharti mbio mbio kwa usalama wake na udikteta wake., Madevdev alikimbia usiku ule ule na ndege akatokomea kusikojulikana

Unafkiri siku NATO wakiamua kutumia Jesho la nchi 32 duniani kuingia vitani na Putin inaweza chukua hata dakika 10 nchi iitwayo Russia haijapotea kwenye ramani ya dunia na kubaki vumbi tupu
Ujinga wa kiwango hiki ni adhabu nzito sana kwa taifa unalotoka. Pole sana, najua ulipofikia hutabadilika
 
Huna akili., Urusi anakuwaje mwamba?
Mwamba aliyeekwa kati ni kikundi kidogo cha Wagner ambacho alikitengeneza mwenyewe, wakachukua kituo cha jeshi Rostov bila kuua hata kuku? Putin akajificha chumba chini ya ardhi mpaka rais wa Belarus alipomuangukia Prigozhin putini akakubali masharti mbio mbio kwa usalama wake na udikteta wake., Madevdev alikimbia usiku ule ule na ndege akatokomea kusikojulikana

Unafkiri siku NATO wakiamua kutumia Jesho la nchi 32 duniani kuingia vitani na Putin inaweza chukua hata dakika 10 nchi iitwayo Russia haijapotea kwenye ramani ya dunia na kubaki vumbi tupu
Hizi ndio akili za Pro nato!Aibu nimeona mimi!
 
kwa mchango wako huu...ww ndio huna hzo akili..!!!

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Huna akili., Urusi anakuwaje mwamba?
Mwamba aliyeekwa kati ni kikundi kidogo cha Wagner ambacho alikitengeneza mwenyewe, wakachukua kituo cha jeshi Rostov bila kuua hata kuku? Putin akajificha chumba chini ya ardhi mpaka rais wa Belarus alipomuangukia Prigozhin putini akakubali masharti mbio mbio kwa usalama wake na udikteta wake., Madevdev alikimbia usiku ule ule na ndege akatokomea kusikojulikana

Unafkiri siku NATO wakiamua kutumia Jesho la nchi 32 duniani kuingia vitani na Putin inaweza chukua hata dakika 10 nchi iitwayo Russia haijapotea kwenye ramani ya dunia na kubaki vumbi tupu
Takataka kama wewe ndo mnafanya bandari ziuzwee kizembe...mbona hao NATO wasimpe uanachama ili waingize hao mashoga zako wakapigane na Russia..maza fanta kabisaa ww
 
Back
Top Bottom