Ipi siri ya nchi ndogo ya Korea Kusini kuzalisha umeme mwingi wa Gigawatts 143?

ward41

JF-Expert Member
Apr 3, 2022
397
1,394
Screenshot_20240207-084715.jpg

Korea Kusini ni nchi ndogo sana, ina 100 Sqkm za mraba.

Ni nchi iliyoendelea sana kiuchumi, ki technologia.

Uzalishaji wa umeme wa hii nchi ni gigawatts 143. Gigawatts 143 ni sawa na megawatts 143000. Huu umeme ni mwingi sana. Nini siri ya wenzetu kua na uzalishaji mwingi kiasi hiki?
 
Korea kusini Ina ukubwa wa 100sq km?

Masihara haya!

Sent from my Infinix X660B using JamiiForums mobile app
Korea Kusini haina eneo lenye ukubwa wa 100 km². Eneo kamili la Korea Kusini ni takriban 100,363 km². Iko katika Rasi ya Korea Mashariki, ikishiriki mpaka na Korea Kaskazini. Ni nchi ya kisiwa iliyoko katika Asia Mashariki na ina idadi kubwa ya watu, ikiwa na karibu milioni 51. Seoul ndio mji mkuu na mji mkubwa zaidi wa Korea Kusini.
 
Hiyo nchi tamu sana!

Inaushirikiano sana na USA kama ilivyo Japan.

Jirani yake Korea Kaskazini kamshikilia Urusi na udikteta matokeo yake raia wanaishi kama wapo jehanamu.

Nina mpango niagize simu ya Samsung huko Korea Kusini.
 
Huwezi kuwa mshirika wa lile dubwana kubwa alafu ukawa mjingamjinga. South Korea, Japan, Taiwan ni washirika wake na wote wako vizuri kiuchumi. Meanwhile, North Korea majirani na ndugu kabisa wa South Korea hawafikishi 8,000 MW wakiokolewa na kuwa na deposit ya makaa ya mawe, na wenye umeme nchi nzima hawafiki 60%
 
Kuhusu size ya eneo LA nchi ya Korea Kusini amekosea, tusipoteze Mira kwenye hiyo typing error, turudi kwenye Nada nini siri kea nchi ndogo Kama Korea kusini kuweza zalisha umeme mwingi kiasi hicho na nchi kubwa Kama Tanzania hata mega wat 10,000 tuu hatujaweza fikia huko.
 
1. Vita baridi kati ya Marekani na Urusi. Korea ya Kusini ilikuwa upande wa Marekani ikapewa boost sana kuendelea.

2. Utamaduni wa Wakorea kutaka ufanisi zaidi, kujiongeza zaidi, kutopenda kufeli, kufanya kazi sana.

Tafuta kitabu kinaitwa "Why Nations Fail: The Origins of Power Prosperity and Poverty" kuna chapter nzima wamechambua maendeleo ya Korea na hata kulinganisha Korea ya Kusini na Kaskazini.
 
Mna hoja/maswali ya kitoto saana...unajua kabisa kiuchumi ata GDP(PPP) Korea kusini kazipita nchi nyingi saana zilizoendelea.. Canada wenyewe wamekimbizwa,Leo mnataka kuja kuilinganisha na Tanzania
 
View attachment 2896686
Korea Kusini ni nchi ndogo sana, ina 100 Sqkm za mraba.

Ni nchi iliyoendelea sana kiuchumi, ki technologia.

Uzalishaji wa umeme wa hii nchi ni gigawatts 143. Gigawatts 143 ni sawa na megawatts 143000. Huu umeme ni mwingi sana. Nini siri ya wenzetu kua na uzalishaji mwingi kiasi hiki?
Huku viongozi na TANESCO akili zimedumaa
 
1. Vita baridi kati ya Marekani na Urusi. Korea ya Kusini ilikuwa upande wa Marekani ikapewa boost sana kuendelea.

2. Utamaduni wa Wakorea kutaka ufanisi zaidi, kujiongeza zaidi, kutopenda kufeli, kufanya kazi sana.

Tafuta kitabu kinaitwa "Why Nations Fail: The Origins of Power Prosperity and Poverty" kuna chapter nzima wamechambua maendeleo ya Korea na hata kulinganisha Korea ya Kusini na Kaskazini.
Mbona nchi yao ndogo sana na wana viwanda vingi na exports nyingi. Wamewezaje eneo lao ni 100,410km². Mbona ni kama mikoa miwili tu ya Morogoro na Pwani. Halafu wana umeme mwingi mno.

Nashangaa mno, mpaka wanasaidia nchi za afrika. Hata Tanzania tusaidiwa na Korea na kukopeshwa matrillioni na korea kupitia shirika lao la Koica.

Hao wamewezaje?
 
Back
Top Bottom