Wengi wetu habari za KK tunazipata hasa kwenye vyombo vya habari vya Magharibi ambavyo vimejikita zaidi katika propaganda na si ukweli.
KK ni moja ya nchi ambayo ina usiri mkubwa sana na sio rahisi kujua wanaishije kama hujawai kufika huko.
Vyombo vya Magharibi haviwezi kumsifia Kim na nchu yake kwa sababu wa yupo nje ya Mfumo Dunia.
Tuwe wa kweli kabisa kabisa . Wazungu huwa hawadanganyi kwenye taarifa zao.
Waandishi wa habari wa nchi za magharibi wanajitolea kuandika taarifa za kiuchunguzi hata kama mwenzake ameuaja jana leo atakwenda tu.
Na pia vyombo vingi vya habari vya magharibi viko huru na havimililkiwi na serikali zao vyote .
Na wenzetu wanajua adhari ya kuandika taarifa za uongo. Kuwadanganya watu kuwa wazungu ni waongo ni kuwafanya watu wawe wajinga. Leo hii taarifa zote zimewekwa kwenye mitandao mtu anagoogle tu anapata jibu hapo hapo.Sasa kama utamfundisha mtoto wako kuwa wazungu ni waongo utamfanya ashindwe kutafuta taarifa na kujifunza mambo mengi.
Elimu yote tunayoisoma na kujifunza asilimia kubwa ni ya magharibi sasa ukisema kila kitu ni propaganda unapotosha umma.
Kwa mfano Mzungu akikuambia tarehe 25/7/2015 saa mbili asubuhi patakua na kupatwa kwa jua na mwezi basi ujue utafiti ulishafanyika.
Mzungu ameshatafiti mpaka namna mchwa ,siafu ,simba,nyoka n.k wanavyoishi na kuzaliana na hatimaye akaweka kwenye dvd na wote tunafaidi. Ukitaka uwe wa ajabu waambie watu kwamba ni tafiti za uongo.
Kama ni move au tamthilia basi wazungu wako wazi wanakuambia hii sio kweli ni igizo.
Korea sio tishio kwa nchi za magharibi kama tunavyofikiri bali ni tishio kwa baadhi ya wakorea wenye maoni tofauti na aliyonayo mfalme na serikali yake.
Ni tishio kwa watu wenye imani tofauti na imani ya dini zao za asili.
Nakumbuka wakati mh Rais wetu alipoingia madarakani alienda uingereza akakutana na kashfa ya watu wa Mwanza kula mapanki ya samaki kutokana na umaskini wa kushindwa kununua minofu ya samaki kama wanayosafirisha kwenda ulaya.
Watu walikuja juu sana akiwemo mh .Rais na kusema kuwa ni propaganda za kuchafua nchi yetu.
Lakini wale tuliokua tumeyaona hayo mapanki yakitumika kama chakula tulikua hatukushangaa.
Hata mauaji ya albino yalianza kuandikwa na vyombo vya magharibi watu wakasema ni propaganda chafu kwa watanzania.
Na pia tukumbuke kuwa vyombo vya magharibi huwa vinaandika hata taarifa za kukosoa nchi zao.
Kwa mfano kama wanajeshi wa nchi kama marekani watafanya vitendo vya kudhalilisha binadamu wengine wakati wa kufanya kazi zao ni wazi kuwa vyombo hivyo hivyo vimekua vikitoa taarifa na hatua zinachukuliwa.