Kopesha ushangazwe

Kopesha ushangazwe

Mm baada ya kuzungushwa na ninao wadai nimeamua.

Anayetaka kukopa kwangu kama mwanaume lazima aache mkewe kwangu nikae naye kwa muda anaokaa na pesa yangu.
Kama mi mwanamke naye awe radhi kukaa kwangu kwa muda anaokaa na pesa yangu hadi atakaporudisha pesa yangu.
Wahenga walishapata kusema kukopa harusi kulipa matanga.

Wabongo almost wote wakisha kopa pesa huwa hawaangalii tena nyuma ni sawa na amejisaidia "kimba" gumu/kavu.
Ni hatari sana Mkuu tutashidwa kusaidiana kisa kukosa uaminifu Mdogo Mdogo.
 
Mh dada unaweza kudhani uwa hawajali ila ukweli ni kuwa wanajali sana ndiyo maana utakuta kama ni mwanaume anaotwa na tambi tepetepe maana akiwa na stress za deni njaa haikawii ,hivyo kila muda nikula tu .

Note :uchunguzi huu nimeufanya mimi mwenyewe kupitia madeni niliyonayo
😁😁 Kitambi na unadaiwa Mkuu.
 
Biashara ya kukopesha isiyofuata sheria ni utapeli na pia hauwezi kutoboa kwa biashara hiyo.

Kuna kaka'ngu alistaafu, akaanzisha mradi huo.

Masharti eti mtu akaweke dhamana asset zake, mf: makochi, fridge, Tv's, magodoro, radios, baiskeli nknk.

Bila kujijua akawa anafanya biashara ya kununua vitu chakavu.

Kumbe waliokuja kuweka dhamana na kukopeshwa fedha, walikuja kuuza.

Hakuna aliyejishughulisha kwenda kukomboa!

Kimbembe kikaja yeye kuvitafutia soko la kuviuza kwa faida!

Tunavyoongea, tayari yupo kwenye magogo.
Aisee noma Sana Mkuu hasara tupu.
 
Mimi Kuna demu aliniface for the 1st time alitaka laki4 nikasema nayo nusu laki2 akasema ndani YA week atanipa

Kilichofuata akawa hapokei simu (Dah Shida aisee) demu mwenye tulisoma naye chuo...Na alikuja personally kuwa ana Shida..tulikuwa Na miaka Zaidi YA Kumi bila kuwa Naawasilano YA moja Kwa moja...as of now hata sh Kumi hajarudisha..niliamua samehe
Aisee noma Sana Mkuu sijui huwa wanawaza nini au tuseme umasikini.
 
Huyu mmoja alianza dharau aliponikopesha elfu mbili ili niongeze bia pale kitelewasi taarifa nikazikuta kwa work mate wangu tena wakiwa wananicheka eti naenda bar na hela pungufu ni hapo najaribu kumfundisha kuwa dunia ina pande mbili ndugu .

Huyu mwingine ningemlipa ila shida akipiga simu kunidai hela yake hakuwahi kunisalimia ilihali namzidi umri na cheo hivyo namfundisha kuwa na heshima
Hahaa wewe ni mdhulumaj tu huna lolote
 
Kumkopesha mtu shida sana,
Mimi wiki kama 2 kuna jamaa alinifata home usiku akaniomba nimsaidoe kiasi kidogo cha fedha alikuwa mpole sana na mnyenyekevu nikamwambia sina.
Akanifata tena siku iliyofata akiwa na mtoto wake anatia huruma kwamba mtoto anaumwa akanisisitiza nimkopeshe atanirudishia baada ya wiki moja.
Imefika wiki simuoni nikaanza kumtafuta nikikutana naye ananiambia hana hela hajapata. Ananiahidi kesho ,ikifika hiyo kesho aliyosema haji naanza kumtafuta nikimpata ananijibu hajapata ananipa ahadi ambazo hatekelezi.
Yaani ikawa mimi ndio namtafuta namdai .
Jinsi ambavyo sipendi kufatilia watu nimeamua kumchunia kila akiniona anajistukia saa nyingine anajificha wakati mimi nishamuona na mimi nampotezea.
Kukopesha watu imekuwa jau sana .
Unapata kazi ya kuanza kumfatilia akulipe wakati alipokuwa anashida yeye ndiye alikutafuta
Inakera mno kuanza kufatilia den wakati mtu anatakiwa alete mwenyewe tu
 
Mimi Kuna jamaa mtu mzima Aliniambia nikopeeshe jero ntantalilalila nyingi halafu ni mtu mzima nikmuona mjinga tu afadhlali angeniambia niungie jero hadi Ile sehemu akawa anaogopa kuja mwingine nitakuletea ela yako kwenye biashara ni watu wajinga na kuwapuuzia ila kama deni kubwa mfuate mtu muulize shida nini?
 
Mimi Kuna jamaa mtu mzima Aliniambia nikopeeshe jero ntantalilalila nyingi halafu ni mtu mzima nikmuona mjinga tu afadhlali angeniambia niungie jero hadi Ile sehemu akawa anaogopa kuja mwingine nitakuletea ela yako kwenye biashara ni watu wajinga na kuwapuuzia ila kama deni kubwa mfuate mtu muulize shida nini?
Hakika Mkuu mambo yasiwe mengi.
 
1.Nimebwagiwa simu ya tachi kwa elfu 20 kwa ahadi ya kulipa ndani ya wiki moja lakini mwezi unakata sasa na yupo kimya tu.
2.Mwengine mpangaji mwezangu naye mwaka unakakaribia kukata kwa ahadi ya wiki moja atarejesha,nimebaki namwangalia tu na alivyo kauzu akipataga changamoto ananikimbilia vidogo nam save vikubwa namwambia sina ata kama ninacho.
 
Mimi Kuna demu aliniface for the 1st time alitaka laki4 nikasema nayo nusu laki2 akasema ndani YA week atanipa

Kilichofuata akawa hapokei simu (Dah Shida aisee) demu mwenye tulisoma naye chuo...Na alikuja personally kuwa ana Shida..tulikuwa Na miaka Zaidi YA Kumi bila kuwa Naawasilano YA moja Kwa moja...as of now hata sh Kumi hajarudisha..niliamua samehe
Maelezo yako nimeyapima na kuona kuwa huyo classmet wako ashakuwa tapeli.

Lakini mbinu hiyo pia hutumiwa na wanawake kumpata mwanaume wanayemtamani, wanasema 'kukuelewa', sazingine mitego inakuwa haikunasi na huna hili wala lile.

Mbinu anayotumia kujenga mazoea ya kukufikia, anakuja na gia ya kukukopa.

Sasa katika kupigiana simu za kudaiana, ndounakuta humo humo kaweka nyavu zake.

Kunakuwa na options mbili tu hapo, 'ule uliwe au uliwe bila kula'.
 
Back
Top Bottom