Kombani na Lissu Live on Star TV

Kwanini usifanyika mjadala huu wa Katiba ya Tz baina ya Chadema (Tundu lissu ) na CUF mwakilishi (Aboubakar Hamis) ili tujue mbivu na mbichi. Kwani siku zote Lissu anapewa watu dhaifu na hivyo kutumia nafasi hiyo kuinanga Znz na wa Znz .

Apambanishwe na Mh Abobakar Hamis ili asomeshwe ili kujua katiba ni nini?

Halafu wakishapambanishwa?
 
Ni ukweli uliowazi kuwa Celini Kombani hawezi kusimama kwa hoja na Mh. Tundu Lissu. Ila start waliamua tu kuwapa shavu chadema la kuwaeleza watz kinagaubaga kile kinachoendelea ktk sakata zima la muswada wa katiba huko mjengoni huku wakijua ccm hawana la kueleza kwani wao hawataki katiba ila nguvu ya umma ndo wenye kuitaka hyo katiba mpya.
 
Rafiki Spika alivua joho la uspika na kuamua kufanya kazi za serikali,
Kama Spika ndio alichukua muswada kutoka kwenye Kamati basi BUNGE ndio limegawa muswada wake kwa serikali, na BUNGE ndio limejichakachua lenyewe na Kombani hana kosa!

Na kama Spika aliwapokonya muswada kamati ya Sheria, Spika Makinda ameuliza "kwa nini Tundu Lissu hakusema kwenye hotuba yake rasmi mbele ya Bunge na mbele ya Umma kwamba Spika umechakachua utaratibu, badala ya kukimbilia kwenye midahalo ya station za runinga?
 
very interesting, kweli mtoa mada lazima awe amejiandaa na azingatie kuwajuza wadau japo kwa ufupi kinachoendelea, o/w ni kama anawanawisha watu uku akiwahakikishia no kula, duh tuzingatie
 
Maneno ya mfa maji haya. Wa Znz wameshafikisha jambo hilo UN wanahoji huo muungano. Je wewe umefika wapi? au ndio kulalama chooni?
wazenj hawa wananishangaza. Hivi wakati wanaungana UN walihusika? Au wanataka no fly zone na civilian protection kama ya Nato?
 
mama kombani hakutakiwa kuendelea na swala la katiba mara baada ya ile kauli yake ya kusema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya, sasa mtu ambaye ndiye aliyetoa kauli leo hii ndio anashugulikia swala la kupatikana kwa katiba mpya hii ni ajabu na kweli.


Ndg yangu wa kujilaumu ni sisi wenyewe kwa kutokushinikiza ajiuzulu au rais amuondoe, hapa ndipo tulipo kosea. Lakini bado katupa fursa nyingine ya kulifanya hilo labda sasa turudie makosa.
 
Back
Top Bottom