Kwenye hotuba yake Bungeni Jumatatu yeye mwenyewe Lissu amesema Serikali ilitoa maagizo hayo, Lissu has some explaining to do:
"Mheshimiwa Spika... Bunge - kwa kupitia Spika - liliigiza Serikali kufanya yafuatayo....iandae Muswada huu kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi...
...kwa mujibu wa kanuni ya 84(2) Kamati ilikwishaanza kupokea maoni ya wadau ...Kazi iliyokuwa imebaki kwa Kamati ilikuwa ni kutumia mamlaka yake chini ya kanuni ya 84(3) ... kufanya marekebisho katika Muswada wa Sheria kwa kumshauri Waziri ... anayehusika na Muswada huo kufanya mabadiliko....
Kwa hiyo Lissu kasema Bungeni ( a ) Bunge lilitoa maagizo ...( b ) muswada ulishaanza kufanyiwa kazi na kamati... ( c ) Kanuni zinasema mwisho wa siku Waziri anayehusika na Muswada ndio anaefanya mabadiliko ya muswada . Sasa je:
( 1 ) Kama Bunge halikutoa maagizo muswada urudi kwa Kombani, nani kwa mfano angeutafsiri kwa Kiswahili, Tundu Lissu na Spika?
( 2) Kama hakuna Hansard za ruhusa ya Tume, kina Lissu walikuwa wanafanya nini wakati Kombani anaingia kuwaibia makabrasha ya muswada, walikuwa "wanatafakari" kama Wassira?
(3) Kama tume ya kina Lissu haikumpa Kombani muswada, na wala Kombani hakuingia kwenye makbrasha ya Tume kuiba muswada bali alifanya mabadiliko juu kwa juu akiwa wizarani (maana kila mtu ana nakala) ni kwa nini Tume iliacha kuendelea na kazi ikasubiri Kombani aka take over the marekebisho?
( 4 ) Kama Kombani anayo mamlaka ya kuzuia Tume isiendelee na kazi, Lissu atoe barua ya amri ya Kombani iliyowazuia kuendelea na kazi, na kama hana, Kombani kosa lake nini?