Kodi ya simu yapingwa rasmi mahakamani

Wanaacha kuyatoza makampuni ya mdini walio na fedha mpaka wanawaondolea kodi kwenye mafuta na vifaa vya kazi kwa sababu wana hisa huko nakuweka kodi kandamizi kwa wafanyakazi na masikini. Lo aibu gani hii Serikali yetu !!!!!!?!
 
dah majanga hayo!yani serikali badala ya kufikiria kuwapunguzia mzigo wa maisha magumu watanzania,yani wao ndo wanazidi kutuongezea!
 
Wazo lilitokana na vijisenti haliwezi kuwa tetezi kwa wananchi. Chenge ni bepari aliyejawa kiburi cha pesa, amtetee nani? Jina sahhihi ni maccm na miccm...tutawaheshimu ktk lipi kama mahamuzi wanayoyatoa bungeni ni kandamizi!
 
Hayo ndiyo maisha bora kwa kila Mtanzania. Serikali oyee,kidumu chama cha mapinduzi.
Wanzania tuko tayari kula majani lakini lazima rada inunuliwe!
 
pamoja na tuhuma kibao zinazoikabili mahakama za Tanzania , lakini huo angalau ndiyo angalau uchochoro pekee uliobaki kwa walalahoi kupata haki zao , inshallah tutashinda kesi hii .
 
Kwa kweli hata mimi naunga mkono kwamba hili suala la kukatwa elfu moja kila mwezi haliikumbi serikali bali linakumba watanzania wote hasa katika suala la uchumi! Ninachowaomba viongozi wa serikali ifikie kipindi wawe na msimamo juu ya maamuzi ya raia wake kwa kila hali mbaya iwakabiliyo.
 
Ana simu moja, anachobadili ni sim card, kwa maana kwamba ni mteja wa makampuni matatu ya simu, Hivyo basi hana simu tatu, ila ana line tatu za simu kila line ikiwa ni ya shirika pekee la mobile phone.

Mimi moja wapo na line zaidi ya moja, moja Voda, moja Tigo na moja niendapo nchi za nje, hili ni jambo la kawaida nashangaa unashangaa kwa kushangazwa na mshangao wa line tatu.

Jambo la msingi hapa wewe unatazama nafasi uliyo nayo, huangalii wengine walio katika mazingira magumu ndio tunaowaonea huruma. Mimi binafsi kulipia line hiyo si tatizo, lakini je, shangazi yangu, binafu yangu, wakulima huko vijijini ambao wana simu hutumia kupita tu wanapokuwa na shida pengine mara mbili au tatu kwa mwaka tu.
 
Lipia zote tatu ni shillingi 3,000 tu, halafu una uwezo wa kwenda nchi za nje kama unavyojigamba na kulipia 3,000 inakushinda?

Toa porojo zako. Unanshangaza!
 
Ni ule umoja unaokwenda shindwa kesi nini?CCM wanapenda tapatapa sana;mambao ya nini na Tanesco halafu tanesco wakashindwa kesi..serikali ikakazana lipa..
 
Lipia zote tatu ni shillingi 3,000 tu, halafu una uwezo wa kwenda nchi za nje kama unavyojigamba na kulipia 3,000 inakushinda?

Toa porojo zako. Unanshangaza!

Jibu swali langu, tunaowaonea huruma na ndugu zetu na wananchi wetu walio na uwezo mdogo wa kulipia, wengi huko vijijini wanazo simu kwa matumizi ya dharura tu na pengine huzitumia mara moja au mbili kwa mwaka wawapo na tatizo, hao wewe huna uchungu nao unataka warudi mazingira ya zamani?

Nimeshakuambia mimi sina shida kulipia lakini kinachoniumiza moyo ni hawa wananchi wasio na kipata ambao uwezo wao wa kulipia simu line hawana, hutumia simu kwa kiwango ambacho ni chini ya hiyo 1000 kwa mwaka, wewe unaona ni sawa?
 
huyo mama alishajitoaga akili....
 
Wazo lilitokana na vijisenti haliwezi kuwa tetezi kwa wananchi. Chenge ni bepari aliyejawa kiburi cha pesa, amtetee nani? Jina sahhihi ni maccm na miccm...tutawaheshimu ktk lipi kama mahamuzi wanayoyatoa bungeni ni kandamizi!

mzee wa vijisenti!
 
Sijawahi kupigiwa na ndugu zangu simu hata siku moja,wanachofanya ni kunibuzz mimi napiga, na hii ni kutokana na hali ya vipato vyao. Kwa maana hiyo hii kodi itatunyima fursa ya kupashana habari. Wakumbuke simu nyingi za ndugu zetu vijijini ni receiver, je hii kodi si itafanya tushindwe kuwasiliana na ndugu zetu?
 
Hela kwa ajili ya uchaguzi hizo! Wa Tanzania msikubali huu upuzi..
 
Hongera mkuu kwa kumuelimisha huyu kilanza...
 
Reactions: 1gb
Lipia zote tatu ni shillingi 3,000 tu, halafu una uwezo wa kwenda nchi za nje kama unavyojigamba na kulipia 3,000 inakushinda?

Toa porojo zako. Unanshangaza!

uwe unasoma na kuelewa we nae kakwambia yeye ndio anaweza ila vipi kwa wale wasio na uwezo? umejawa na wivu sasa waona kwenda nje ni kujigamba? kila mtu anakazi yake na mtu kwenda nje ni kawaida kutokana na ishu anazofanya. duh kweli tumetofautiana.
 
Tena hao wenye kazi za kuwapeleka nje ndio wangelipia zaidi na kuubeba mzigo wa wale wasio na kazi.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…