Wadau nimepokea taarifa Kuwa Umoja wa Chama cha Kampuni za simu (MOAT) sio kile cha baba Mengi. . . Leo wanaenda mahakama ya Kodi kuweka pingamizi kwa kila Mtanzania kukatwa shilingi 1000 kuanzia Mwezi Julai. Sasa niko njiani kwenda kuwaunga Mkono hawa jamaa...... Mimi nina Laini tatu inamaana nadaiwa elfu 9. Mungu anisaidie. Watanzania tunaumizwa si mchezo.
Siungi mkono kampuni za simu kuweka pingamizi,wao ni wakusanyaji tu wa hii kodi iweje leo wawahurumie wateja wa simu waliozoea kukuibia!!
Great Thinkers nataka mjue siri iliyojificha hapo,kampuni za simu zimekuwa wakwepaji wakubwa wa kodi na sasa imefika mwisho wao,serikali itakuweka system mpya ya kupata kodi na hivyo kampuni hizi hazitaweza kuweka kodi kama waliozoea.
Tusikubali kudanganyika,tulipe hiyo kodi na tuibane serikali katika matumizi yake.
Hii kodi ya shilingi elfu 12 kwa mwaka ni kubwa sana kwa mtanzania. Naunga mkono juhudi hizo kwa kuwa mchakato wa kuanzisha hiyo kodi haukushirikisha wadau, imeletwa kibabe, pia kodi hiyo itawahusu hata watoto wadogo wa umri chini ya miaka 18, wazee na wagonjwa. Kodi ya simu haikubaliki. Usaliti wa January Makamba huu.
tatizo si kodi tatizo ni matumizi mabovu ya serikali..... hizo zitatumika kugharamia safari za hawara zao tu ni vyema kupinga hiyo kodi.
Kodi siyo kubwa ila "DIRECT TAX" is always painful. Mbona kuna "INDIRECT TAX" - excise ya 14% hiyo hatulalamiki?
wanaenda kwa nia njema?? Ni kwasababu wanawapenda ama kuwahurumia watanzania?? Gharama za tozo za simu wameziangalia kwanza?? Na hii serikali ndio maana watu wanasema kiongozi wake ni dhaifu...Mengi/manji/lowasa akatwe 1000 sawa na juma wa kwamtogole ama mzee manywele wa sitimbi?
Kweli mkuu kwani kama zingekuwa na faida kwetu sidhani kama kungekuwa na matatizo kamwe
Hata maandamano mnafanya kwenye barabara za lami siku hizi, halafu mnasema hazina faida?
Ni kweli faida zipo..Maana hata mkuu safari zimeongezeka na magari ya kifahari..Tulipe KODI...
Wadau nimepokea taarifa Kuwa Umoja wa Chama cha Kampuni za simu (MOAT) sio kile cha baba Mengi. . . Leo wanaenda mahakama ya Kodi kuweka pingamizi kwa kila Mtanzania kukatwa shilingi 1000 kuanzia Mwezi Julai. Sasa niko njiani kwenda kuwaunga Mkono hawa jamaa...... Mimi nina Laini tatu inamaana nadaiwa elfu 9. Mungu anisaidie. Watanzania tunaumizwa si mchezo.
Naunga mkono baadhi ya sehemu za comments zako ... tangu lini haya makampuni yakatuonea huruma? kila siku wanaibua promotion ambazo zimejaa wizi ... wanatuhadaa eti kifurushi sms 300 ili hali hata kumi kwa siku hutumi na wanalijua hilo fika ... kati ya makampuni ambayo ni wezi na wanyonyaji wakuu wa mtz ni haya ya simu ... alipoteuliwa January nkajua tumepona kumbe laa ...Nawashangaa Watanzania mnabeba simu tatu halafu mnakataa kulipia kodi.
Hii kodi iwepo na nnaikubali kwa roho kunjufu kabisa.
Na hizo kampuni za simu zitashindwa hii kesi na kila zitakavyochelewesha kuanza kukata hii kodi ndivyo tutalimbikiza kodi na tutaumia sisi zaidi na wao watajichotea humohumo. Ni wajanja tu hao.
Serikali iwaambie kama wanahuruma sana na wananchi wapunguze bei zao kufidia hii kodi.
Na Mitanzania ijinsi tulivyo mingine itaingia kichwachwa na kuwaunga mkono hizi kampuni ambazo hazitazami maslahi ya Mtanzania zaidi ya bishara yao tu.
tulipokubari utandawazi hatukujua kama ipo siku moja tutaikumbuka posta na simunahisi mfumo wa kutuma barua alafu unatumbukiza kwenye basi unataka kurudi taratibu
MAHAKAMA YA KODI??!! iko wapi hiyo mkuu?
Kweli mkuu kwani kama zingekuwa na faida kwetu sidhani kama kungekuwa na matatizo kamwe
Mwambie huyo anayeishi zama za mawe kuwa pia una modem ya Vodacom,unatumia kwenye laptop yako huko uliko amabapo siku hizi ofisi sio lazima iwe kwenye jengo maalumu bali hata nyumbani na ukafanya kazi zote huku ukisubiri chakula cha nyumbani anachopika mamsap ukiwa home na kazi ikaendelea kufanyika .tena kazi zenyewe zikiwa mbali hata zikiwa kwa Obamausiwe KILAZA jaribu kujifikirisha,sio kila kitu utafuniwe.Haya meza basi ngoja nikutafunie.
Mimi kwa sasa nipo Dar kwa bussines zangu na bussines partiners wengi wanatumia sim card za tigo,hivyo kuepusha gharama za kupiga kati ya voda(line yangu )na tigo{partiners} itanibidi niachane na voda kwa muda ili hamie tigo,licha ya hayo Nimeiacha familia yangu mtwe mafi,kigoma mwisho tena kijijini kabisa,kule nertwork inayo patikana ni airtel pekee na wao(my family)kwa kigezo kilekile cha kuepusha gharama itabidi wanipigie kuptia line yangu niliyo tokanayo huko shamba(airtel).
Sasa hapo tayari ninakuwa na line ngapi?
Iwapo kampuni za mitandao yoote Tanzania zingekuwa na gharama moja ya kupiga kwenda mtandao wowte hapa Tz,naamini tusingekuwa tunabeba line 3'3
Umenisoma wee KILAZA.
Nawashangaa Watanzania mnabeba simu tatu halafu mnakataa kulipia kodi.