Kodi ya simu yapingwa rasmi mahakamani

MATATIZO SABA

Member
Joined
Sep 28, 2011
Posts
8
Reaction score
4
Wadau nimepokea taarifa Kuwa Umoja wa Chama cha Kampuni za simu (MOAT) sio kile cha baba Mengi. . .

Leo wanaenda mahakama ya Kodi kuweka pingamizi kwa kila Mtanzania kukatwa shilingi 1000 kuanzia Mwezi Julai. Sasa niko njiani kwenda kuwaunga Mkono hawa jamaa...... Mimi nina Laini tatu inamaana nadaiwa elfu 9.

Mungu anisaidie. Watanzania tunaumizwa si mchezo.
 
Hii kodi ya shilingi elfu 12 kwa mwaka ni kubwa sana kwa mtanzania. Naunga mkono juhudi hizo kwa kuwa mchakato wa kuanzisha hiyo kodi haukushirikisha wadau, imeletwa kibabe, pia kodi hiyo itawahusu hata watoto wadogo wa umri chini ya miaka 18, wazee na wagonjwa. Kodi ya simu haikubaliki. Usaliti wa January Makamba huu.
 
Una line tatu zote hizo za nni?

 

Kodi siyo kubwa ila "DIRECT TAX" is always painful. Mbona kuna "INDIRECT TAX" - excise ya 14% hiyo hatulalamiki?
 

Huyo Makaamba hamna kitu mbona!!
 
Una line tatu zote hizo za nni?
usiwe KILAZA jaribu kujifikirisha,sio kila kitu utafuniwe.Haya meza basi ngoja nikutafunie.
Mimi kwa sasa nipo Dar kwa bussines zangu na bussines partiners wengi wanatumia sim card za tigo,hivyo kuepusha gharama za kupiga kati ya voda(line yangu )na tigo{partiners} itanibidi niachane na voda kwa muda ili hamie tigo,licha ya hayo Nimeiacha familia yangu mtwe mafi,kigoma mwisho tena kijijini kabisa,kule nertwork inayo patikana ni airtel pekee na wao(my family)kwa kigezo kilekile cha kuepusha gharama itabidi wanipigie kuptia line yangu niliyo tokanayo huko shamba(airtel).
Sasa hapo tayari ninakuwa na line ngapi?
Iwapo kampuni za mitandao yoote Tanzania zingekuwa na gharama moja ya kupiga kwenda mtandao wowte hapa Tz,naamini tusingekuwa tunabeba line 3'3
Umenisoma wee KILAZA.
 
Nawashangaa Watanzania mnabeba simu tatu halafu mnakataa kulipia kodi.

Hii kodi iwepo na nnaikubali kwa roho kunjufu kabisa.

Na hizo kampuni za simu zitashindwa hii kesi na kila zitakavyochelewesha kuanza kukata hii kodi ndivyo tutalimbikiza kodi na tutaumia sisi zaidi na wao watajichotea humohumo. Ni wajanja tu hao.

Serikali iwaambie kama wanahuruma sana na wananchi wapunguze bei zao kufidia hii kodi.

Na Mitanzania ijinsi tulivyo mingine itaingia kichwachwa na kuwaunga mkono hizi kampuni ambazo hazitazami maslahi ya Mtanzania zaidi ya bishara yao tu.
 

hizo kodi wanazotoa watanzania. je zinaendana na kipato chao? hivi unajua watanzania wanaishi chini ya dolla 1 kwa siku? nenda uko vijijin uone hali ilivyo ngumu. kupata elfu tu ni kazi kubwa.

pia usiangalie wachache angalia watanzania walio wengi.
hivi unajua serikali ina misamaha mingi ya kodi kwa matajiri na sekta kama madini.

kwenye madini serikali ya botswana inapata zaidi ya asilimia 40 ya kodi pia kuna sheria za kuwalazimisha wajenge miundo mbinu sehemu wanakochimba.

uku Tanzania serikali inachukua asilimia 3.
ujinga sana huuu
 

Lakini FaizaFoxy mtu wa mwisho anayeumia ni mtanzania,siamini kama serikali haina uwezo wa kuwabana
hao wawekezaji wa simu wakapunguza gharama,lakini badala ya kusaidia na serikali nayo inamuongezea mzigo
mtanzania hapohapo kwenye gharama kubwa za wawekeji hao kwa kumdai mwananchi kodi,wakati kiukweli
ukifuatilia hata hao wenye makampuni ya simu hawalipi kodi kama inavyotakiwa kulipwa kwa kisingizio cha uwekezaji
,hapa wa kulaumiwa ni serikali yetu na viongozi wake wanafiki'
 
nahisi mfumo wa kutuma barua alafu unatumbukiza kwenye basi unataka kurudi taratibu
 
serikali ina huruma kw wananchi wake?... kila mtu hapa ni mwizi tu! tayari kodi ya simu inakuwa imeisha katwa sasa hii tene kulipia line inatoka wapi, mbaya zaidi unakuta hii pesa tunayo lipa ndiyo inatumika wakati wa uchaguzi ili kuchakachua matokeo. hivyo tunakuwa tume kaangwa kwa mafuta yetu, huu ni utmbo mtupu!
 
Sijui niuze simu!! Ili tukose wote!!
 

MAHAKAMA YA KODI??!! iko wapi hiyo mkuu?
 
Nakuunga mkono, mguu, kichwa na kila kitu Money Stunna, siku zote mi hujiuliza hivi kwanin watawala wa nchi hii hawatak kuiga yaliyo mazur kw wenzetu, mf kwenye sector ya madin kwani hao investors tukiwawekea kodi yenye manufaa kwetu itakuw dhambi?
 
Last edited by a moderator:
waongeze ifke buku hata 5 kwa mwezi.baadhi ya watanzania mambulula yanayoendelea kung'ang'ania ccm yapate kujifunza manafk wakubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…