Kodi ya Simu: Serikali lazima isikilize kilio cha wananchi

Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.
Nakubaliana na wewe ila si hii tu. Inabidi hata Kodi ya MPESA na Ile ya Internet ifutwe pia.
Mimi kama mmoja wa wadau ambao tunapigania taifa hili kusonga mbele kiteknolojia mnatukatisha tamaa. Internet imepanda bei na muda sio mrefu (kama hili pia halitabadilishwa) itabidi turudi tu zama za SLP! Sasa kama Serikali iko serious na manendeleo na ninyi kama Chama kinachoongoza serikali naomba muangalie suala hili kwa jicho lingine. Kuna faida gani serikali ikipata kodi hii halafu kiteknolojia ikarudi nyuma? Internet ni sehemu ya kujifunzia kwa wanafunzi na wao hawana uwezo wa kumudu gharama zinazopanda.

Pia MPESA kodi hii ifutwe kwa kuwa muda mwingi watu wanatumia ndugu zao visenti vidog walivyovuna mjini ili na bibi nae ajisikie duniani. Kama ni muhimu sana basi at least kodi hii itozwe kwa fedha kuanzia 300 000 na kuendelea. Nape Nnauye gharama za kodi zibaki tu kwenye VAT basi. Hapo tutakuwa na uhalali wa kusema serikali ina mpango wa kuleta maendeleo kwa wananchi wake!

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
Nape Nnauye ni kweli serikali LAZIMA isikilize wananchi wake KAMA inataka kuwa na moral authority ya kuitwa serikali ya wananchi. Ila kwa nini kodi ya migodini isipandishwe. Siamini kama makampuni ya simu hayakuwa ktk top ten ya walipa kodi pamoja na mamigodi makubwa haya! Huko ndiko pa kubanana nako kwanza kabla ya kutubana wanakijiji wa Mkonze!

BTW Nape Nnauye unaweza mweleza Mwenyekiti wako Mh. JMK kuwa atumie kofia yake ya Urais kuyaingiza mapendekezo yako haya. Ila tu mwambie pia kuwa kodi ya Internet, na MPESA ni mzigo kwa wadau wanaomsaidia kupeleka maendeleo na Teknolojia kwa wananchi anaowaongoza!
 
Last edited by a moderator:
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Nape Bana!!!
 
Sina hakika kama unajua unachokisema...laikini pia inawezekana hujui utaratibu unaotumika kufanya maamuzi ndio maana sijui nianzie wapi kukushauri. Swala likishapitishwa na bunge si swala la wabunge flani ni swala la bunge...

Mangapi yamepitishwa na bunge au serikali na Chama tukayapinga na yakabadilika? Kama unakumbukumbu nzuri fuatilia nani alianza kulipinga hili kati ya vyama vya siasa nchini.
Nape Nnauye Wabunge wa CCM na mawaziri wa CCM ndo wamepitisha hii KODI YA LINE YA SIMU, KWA nia OVU ya serikali ya CCM kuendelea kubinya mawasiliano nchini, mlianza na ving'amuzi mkatuondoa wengi kwenye kuangalia TV sasa mmekuja na kwenye simu za mkononi tena mtufute wengi kwenye kuunganishwa na mawasiliano! Kwanini mnafanya hivi wakati technologia inaongezeka mawasiliano yanapaswa kupungua bei lakini Tanzania inakuwa kinyume chake. Mlisema mkongo wa taifa ukijengwa mawasiliono yatashuka bei lakini sasa mawasiliano ndo yamekuwa balaa kabisa! Kwanini mnatafuta vyazo rahisi vya mapato kwa gharama ya mwananchi mnyonge? Nape Nnauye kiri tu kuwa serikali yako ya CCM imeshindwa.
 
Last edited by a moderator:
Unaujua utaratibu wa kulifanya hilo unalolisema? Ndo maana wananchi wanamashaka na uwezo wa chama chako kuongoza nchi kama hata mambo madogo ya utendaji kama hilo unadhani ni swala la kumuita waziri na kuelekeza...

Nape ulicho andika hapa KIMENISHTUA SANA na kimeonyesha kuwa CHAMA na serikali yake HAWANA mawasiliano juu ya mustakabali wa kuwahudumia watanzania!

(1)Katibu Mwenezi CCM-Taifa Nape anapinga SIMCard Tax
(2)PM Pinda anasisitiza tozo la SIM Cardtax ni halali na lzm ianze kulipwa kama ilivyopitishwa na Bunge
(3)Waziri Mgimwa mara anasema lzm ilipwe mara anadai kwa kupitia Bunge suala hili linaweza jadiliwa tena
(4)Mawaziri wa wizara husika akiwemo Makamba Jr yy anasema kuwa WALIPINGA tozo kwenye ikao vya Baraza la Mawaziri lkn walizidiwa na wajumbe wengine
(5)Rais JK yy HANA NONGWA na kutolewa kwa kodi hii lkn LZM APEWE ALTERNATIVE ya wapi zitapatikana tsh Bilion 179 kuziba pengo kwenye bajeti kuu!

Hizi ni kauli tata zisizofaa kutolewa na watu wanaounda serikali moja ya chama hicho hicho;Kwa mtiririko huo juu na kauli yako kama Katibu Mwenezi wa CCM-Taifa ni dhahiri CCM na serikali yake kila mtu na lake!Wananchi sasa hawajui wamuamini nani!

Kwa nn CCM hawakukataa kodi hii mapema?Ham-wasiliani na serikali yenu?
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Nape
Naona sasa umeamua kukili kuwa Serikali yako ya CCM sio Sikivu (Hapa lazima Serikali ionyeshe usikivu),,,Nakushauri wataarifu pia wabunge wako wa CCM waache kuwa wanasifia mambo ya kijinga yasiyokuwa na tija kwa Taifa, maana wao kila wakisimama kuchangia wa Hoja yoyote utasikia Serikali hii Sikivu wakiongozwa na Mama Anne Kilango,,,

Ni kwa sababu ya CCM kutokuwa wasikivu watu wasio hata na akili siku hizi wakiongozwa na Ndg Mnyika, Dr. Slaa, Mbowe, Wenje, Msigwa, Mdee, Lema hawaachi kukilaani CCM huku wakipongeza sana juhudi zinazofanywa na CHADEMA kutetea maslahi ya wanyonge wa Taifa hili. Nina wasiwasi hali ikiendea hivi hawa watu wasio na akili watakabidhiwa nchi 2015 na nyie Magenius mtakuwa hamna cha kusema. Jipangeni Kiongozi, wakati sio wenu, washkaji washajiandaa vya kutosha na wananchi hakuna namna wanawataka wao tu.

Nakulaumu unasema katika kumjibu mtu fulani hivi unaposema ili ni Suala dogo huwezi kumuita waziri kumshauri wakati Rais mwenyewe kakutana na wadau akiwemo waziri kujadili suala hili, Nasema hivi zile kodi zilizosamehewa kule kwenye migodi zirudishwe kufidia hiyo pesa ambayo ingepatikana kwa kuwadhulumu wananchi..HONGERA NAPE kwa kuongoka
 
Uwezo wako ndipo ulipoishia....
Nape, siku za nyuma ccm iliwahi pia kuja na mapendekezo serikali isikize maoni ya watu wa Loliondo, na wa Mtwara katika migogoro ya ardhi na gesi. Unaongeleaje reaponse ya serikali katika mambo hayo?...
 
Nimnukuu Mh. Peter Msigwa (Mb.) "Problems cannot be solved by the same level of thinking that created them". Hiyo kodi imewekwa na nani na sasa Nape Nnauye unataka iondolewe na nani? Au ndio mlikuwa mwatikisa kiberiti??
 
Last edited by a moderator:
PHP:
Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Vichekesho!
Kumbe unajua serikali yako hainaga usikivu!
Sasa nyie serikali ya ccm kwanini mlibuni hii kodi in the first place, na kwanini mkagonga mabenchi kuipitisha?
Mnawapelekesha wananchi kwa viini macho vya kitoto ili muonekane mnatetea wananchi!
This time you are totally stuck na hatutawaonea huruma...!
Tumecheka na nyani siku nyingi sana!

mbona unakimbia kivuri chako mwenyewe mambo yote unayofanya ni kwa hisani ya serikali ya ccm,hata aliyekutuma uje jf kuichafua ccm kafikishwa hapo alipo kwa sababu ya ccm na serikali yake.
 
Sina hakika kama unajua unachokisema...laikini pia inawezekana hujui utaratibu unaotumika kufanya maamuzi ndio maana sijui nianzie wapi kukushauri. Swala likishapitishwa na bunge si swala la wabunge flani ni swala la bunge...

Mangapi yamepitishwa na bunge au serikali na Chama tukayapinga na yakabadilika? Kama unakumbukumbu nzuri fuatilia nani alianza kulipinga hili kati ya vyama vya siasa nchini.

Party cocus ya ccm ndiyo matatizo ya wstanzania, bunge lililopitisha hii sheria ni bunge la ndiooooo! na makofi mbele ya tumbo.
Wabunge makini hawakuwepo bungeni ikafika hata waziri mmoja akasema Cdm haiko bunheni bajeti zinaputa kirahisi, tunakujua wewe ni mtu wa maneno ambayo huyatafakati kabla ya kuyatoa kinywani kwako, kwani ni wewe uliyesema Cdm walijilipua wenyewe kule Arusha ili waonewe huruma ili hali ukijua kwa dhati kwamba mlikuwa na shindwa vibaya.
Si shangai kiona unapingana na serikali yako ya ccm inayolitisha bajeti kwa kuwapima wapiga kura wake, leo wewe unaipinga ili hali mwenyekiti wako alikubaliana nayo tuendelee kuumia! Wewe na mwenyekiti wako ni nani mwenye mamlaka? Tuambie aliipitisha akiwa amelazwa hosipiti au akiwa bar?

Hii inaonyesha ambavyo serikali ya Ccm isivyokuwa na upeo wa kuwajali watu wake, inawakumbatia wawekezaji na kuwainia Watanzania fikeni mahi mjue nyie ni viongozi na sio watawala
 
Sina hakika kama unajua unachokisema...laikini pia inawezekana hujui utaratibu unaotumika kufanya maamuzi ndio maana sijui nianzie wapi kukushauri. Swala likishapitishwa na bunge si swala la wabunge flani ni swala la bunge...

Mangapi yamepitishwa na bunge au serikali na Chama tukayapinga na yakabadilika? Kama unakumbukumbu nzuri fuatilia nani alianza kulipinga hili kati ya vyama vya siasa nchini.

Kupinga mnakokufanya ndio tunauita usanii tu na kujikosha kwa wananchi. Nataka nikuambie kuwa safari hii hatudanganyika na maamuzi tayari tunayo. YOU HAVE TO GO! PERIOD.
 
watu wamepiga kelele wee, mkuu kashtukia dili wewe ndo unakuja kusema msimamo. Ama kweli, uso usio na haya ........
 
Nape ulicho andika hapa KIMENISHTUA SANA na kimeonyesha kuwa CHAMA na serikali yake HAWANA mawasiliano juu ya mustakabali wa kuwahudumia watanzania!

(1)Katibu Mwenezi CCM-Taifa Nape anapinga SIMCard Tax
(2)PM Pinda anasisitiza tozo la SIM Cardtax ni halali na lzm ianze kulipwa kama ilivyopitishwa na Bunge
(3)Waziri Mgimwa mara anasema lzm ilipwe mara anadai kwa kupitia Bunge suala hili linaweza jadiliwa tena
(4)Mawaziri wa wizara husika akiwemo Makamba Jr yy anasema kuwa WALIPINGA tozo kwenye ikao vya Baraza la Mawaziri lkn walizidiwa na wajumbe wengine
(5)Rais JK yy HANA NONGWA na kutolewa kwa kodi hii lkn LZM APEWE ALTERNATIVE ya wapi zitapatikana tsh Bilion 179 kuziba pengo kwenye bajeti kuu!

Hizi ni kauli tata zisizofaa kutolewa na watu wanaounda serikali moja ya chama hicho hicho;Kwa mtiririko huo juu na kauli yako kama Katibu Mwenezi wa CCM-Taifa ni dhahiri CCM na serikali yake kila mtu na lake!Wananchi sasa hawajui wamuamini nani!

Kwa nn CCM hawakukataa kodi hii mapema?Ham-wasiliani na serikali yenu?

I like this. Nape hupo hapo? Iweje mpingane ktk mambo ya msingi kama hayo au mtatwambia ndo demokrasia ndani ya magamba. Mnaliyumbisha taifa kwa mawazo yenu yasiyo na msingi. Hakuna mwenye mahamuzi ktk chama na serikali. wabunge wenu kwao kila kitu ni ndioooooo!!! makofi mengi na zomeazomea za kitoto. CDM kaza buti watanzania wajue wanavyouziwa mbuzi kwnye gunia.
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Japo Mwenyekiti wetu Rais Jk huwa hasikilizi na wala haambiliki, angalau kwa hili la kodi ya simu amekurupuka............. let's wait and see.........

But the bottom line ni kwamba serikali ya ccm siyo sikivu, yaana mpaka wakurupushwe kutoka usingizini na CHADEMA ndiyo waanze kuchungulia nje ya pazia kuona wananchi wapo upande gani wa shilingi...........................
BTW, hongera kwa ujasiri........
 
Nape, siku za nyuma ccm iliwahi pia kuja na mapendekezo serikali isikize maoni ya watu wa Loliondo, na wa Mtwara katika migogoro ya ardhi na gesi. Unaongeleaje reaponse ya serikali katika mambo hayo?...

Huko kote baada ya 2015 ni CDM kaka bila kusahau Iringa yoote,, Nape asidanganye watu bali aseme ukweli kuwa serikali yao si sikivu na asubili wanainchi wataifanya iwe sikivu 2015
 
Back
Top Bottom