Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,167
- 5,604
Nakubaliana na wewe ila si hii tu. Inabidi hata Kodi ya MPESA na Ile ya Internet ifutwe pia.Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.
Mimi kama mmoja wa wadau ambao tunapigania taifa hili kusonga mbele kiteknolojia mnatukatisha tamaa. Internet imepanda bei na muda sio mrefu (kama hili pia halitabadilishwa) itabidi turudi tu zama za SLP! Sasa kama Serikali iko serious na manendeleo na ninyi kama Chama kinachoongoza serikali naomba muangalie suala hili kwa jicho lingine. Kuna faida gani serikali ikipata kodi hii halafu kiteknolojia ikarudi nyuma? Internet ni sehemu ya kujifunzia kwa wanafunzi na wao hawana uwezo wa kumudu gharama zinazopanda.
Pia MPESA kodi hii ifutwe kwa kuwa muda mwingi watu wanatumia ndugu zao visenti vidog walivyovuna mjini ili na bibi nae ajisikie duniani. Kama ni muhimu sana basi at least kodi hii itozwe kwa fedha kuanzia 300 000 na kuendelea. Nape Nnauye gharama za kodi zibaki tu kwenye VAT basi. Hapo tutakuwa na uhalali wa kusema serikali ina mpango wa kuleta maendeleo kwa wananchi wake!
Nape Nnauye ni kweli serikali LAZIMA isikilize wananchi wake KAMA inataka kuwa na moral authority ya kuitwa serikali ya wananchi. Ila kwa nini kodi ya migodini isipandishwe. Siamini kama makampuni ya simu hayakuwa ktk top ten ya walipa kodi pamoja na mamigodi makubwa haya! Huko ndiko pa kubanana nako kwanza kabla ya kutubana wanakijiji wa Mkonze!Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
BTW Nape Nnauye unaweza mweleza Mwenyekiti wako Mh. JMK kuwa atumie kofia yake ya Urais kuyaingiza mapendekezo yako haya. Ila tu mwambie pia kuwa kodi ya Internet, na MPESA ni mzigo kwa wadau wanaomsaidia kupeleka maendeleo na Teknolojia kwa wananchi anaowaongoza!
Last edited by a moderator: