Kodi ya Simu: Serikali lazima isikilize kilio cha wananchi

Kodi ya Simu: Serikali lazima isikilize kilio cha wananchi

Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Kama ungekuwa genuine haya maneno ungetakiwa kumuita waziri Mgimwa na kumueleza nini cha kufanya lakini kwakuwa unafahamu kabisa kuwa serikali yenu ya ccm imeziba masikio wala haisikii ndio maana umeamua kuja hapa kutafuta huruma ya wananchi kwa kujifanya mnajali maslahi ya wananchi.

Wakati ccm mnafikiria kuianzisha hiyo simcrad tax at the first place mlitakiwa kufahamu kuwa wananchi wengi hali zao za kiuchumi ziko dhoofu na hawatoweza kuzimudu, na hata kama wapo wanaomudu lakini kuna maeneo mengine ambayo bado serikali ingeweza kujielekeza na kukusanya kodi ya kutosha kujiendesha.
 
Uwezo wako ndipo ulipoishia....

Lazima tukubali kwamba kuna mambo mengine ambayo hata kama uko makini kiasi gani siyo rahisi kuona impact ya uamuzi unaoufanya mpaka implementation ifanyike. Wamarekani juzi juzi tu wameandamana kuhusiana na hukumu ya kumwachia huru mtu aliyemuua kijana mmarekani mweusi, huwezi ukasema judges wote walikuwa siyo makini kujua nini kitaktokea baada ya kutua hukumu hiyo. Cha msingi kama alivyosema @Nape na mimi nakubaliana naye (kwa mara ya kwanza katika posts zake nyingi) ni kuwa serikali na chama (CCM) wanakili hili ni tatizo kama ambavyo Rais Obama alikili kuwa hukumu ile haikufuata misingi ya haki, hivyo tuwapongeze serikali ya CCM kwa kusikiliza kilio cha wananchi. Tujue kuwa serikali ingeweza kusema kama alivyowahi kusema Mh. Magufuri "asiyeweza kulipa sh. 200/= apige mbizi", pia serikali gaidi ingeweza kusema asiyeweza kulipia kodi ya simu aache kutumia simu.
 
Huu usanii mbaya sana....hii kodi imepitishwa na wabunge wa ccm...unfortunately si kodi tu wabunge wenu wa ccm wanapitisha mabo mengi ya kijinga sana....so kwa mimi nadhani kuliko kuangaika na serekali ungeangaika na wabunge wenu mambumbumbu mwaambie wafanye kazi za wananchi na sio kuleta ushabiki wa kijinga na mwishoni wanapitisha mambo ya kijing jinga kama hivi...
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Ni lini wananchi wa Mtwara watasikilizwa au mpaka serikali ilazimishwe kuwa sikivu?
 
Unaujua utaratibu wa kulifanya hilo unalolisema? Ndo maana wananchi wanamashaka na uwezo wa chama chako kuongoza nchi kama hata mambo madogo ya utendaji kama hilo unadhani ni swala la kumuita waziri na kuelekeza...

Kwani mlipokuwa mkiwaita viongozi wa serikali, tena wasiotokana na chama chenu kilichoshindwa maradufu, hukuwa ukijua some principles ambazo unataka kuonesha hapa, hata kama ni katika masuala au muktadha tofauti...
 
kp24072013.jpg
 
Pole sana ndugu yangu Nape. Nilikushauri mwaka 2010 utoke kwenye Chama Cha. Majanga ukusikia. Ona sasa masikini unavyotumiwa kutoa matamko ya kukudhalilisha wewe mwenyewe, hata kale ka public personality ulikokuwa nako kameisha kabisa! Pole sana ndugu ila tambua kuwwa hicho chama chako cha zamani sasa hakina jipya kimebaki kudandia au kujibu hoja za CDM. Utadhani nyie ndo wapinzani. Pole sana ndugu!
 
Nape

Soma hii taarifa hapa. Najua unayo ofisini kwako, maana unahitaji vitu kama hivi to stretch you are brain a liitle bit more...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa iliyotolewa na CCM na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari tarehe 18 Julai 2013 ya kuitaka Serikali inayoongozwa na CCM kuangalia njia nyingine mbadala ya kukusanya kodi na kuachana na hatua yake ya kukusanya kodi ya umiliki wa kadi ya sh. 1000 kila mwezi imethibitisha maneno ya Mwalimu Nyerere kwamba ‘chama lege lege huzaa serikali legelege’.

Aidha, taarifa hiyo ni mkakati legelege wa kujinasua katika malalamiko, kukusanywa kwa saini, kuandaliwa kwa miswada ya sheria, migomo ya kuzima simu kwa muda maalum na maandamano dhidi ya Serikali ya CCM kutokana na chama hicho kushindwa kuwa na sera sahihi na mikakati makini.

Taarifa hiyo haiwezi kurudisha nyuma hatua ya wananchi kukikataa chama hicho na kuunga mkono mabadiliko ya kweli kupitia CHADEMA kwa kuzingatia kuwa CCM imeshindwa kuhakikisha kwamba Ilani zake za uchaguzi ya mwaka 2005 na 2010 zinatekelezwa. Ikumbukwe kwamba kupitia ilani hizo CCM iliahidi maisha bora kwa kila mtanzania na badala yake maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu kutokana na ongezeko la bei na gharama za maisha.

Ili taarifa hiyo isiwe maneno matupu, Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ajitokeze na

kuagiza utozaji wa kodi hiyo usitishwe kuanzia sasa. Izingatiwe kwamba Muswada huo ambao Rais aliusaini mwanzoni mwa mwezi Julai ulianzisha pia ushuru mwingine na tozo zingine mbalimbali zenye kuongezea mzigo wa gharama za maisha wananchi hususan wa kipato cha chini badala ya kuweka mkazo katika kupanua wigo wa vyanzo mbadala nchini.

Kadhalika, kwa kuwa chanzo cha hali hiyo ni maamuzi yaliyofanywa katika Mkutano wa kumi na moja wa Bunge uliopitisha Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013; ufumbuzi lazima uhusishe marekebisho ya sheria kufuta makosa yaliyofanywa na Serikali ya CCM na kupigiwa kura ya ndio na Bunge lililohodhiwa na CCM.

Hivyo, Rais Kikwete awasilishe katika mkutano wa Bunge kwa hati ya dharura muswada wa sheria wa kufuta vifungu vilivyoingizwa kwa marekebisho ya Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147 na kuondoa ushuru wa bidhaa kwa kadi za simu (sim card) kwa wamiliki wa simu za kiganjani/mkononi.

Taarifa hiyo isipoambatana na hatua za Rais Kikwete kuagiza Mamlaka ya Mapato (TRA) kuacha kutoza ushuru huo na Rais kuwasilisha muswada bungeni kupitia Waziri wa Fedha itakuwa ‘kiini macho’ kama ilivyokuwa taarifa nyingine kama hiyo iliyotolewa na msemaji huyu huyu wa CCM mwaka 2011.

Taarifa ya Nape Nnauye inapaswa kupuuzwa kwa kuwa alitoa taarifa nyingine kwamba CCM kupitia kikao cha kamati kuu yake Agosti 2011 ‘imeagiza’ Serikali ‘kutafuta njia ya kushusha bei ya mafuta ya taa’ iliyopanda baada ya kuongeza kodi ya mafuta ya taa.

Badala ya agizo hilo kutekelezwa mafuta ya taa yaliendelea kupanda bei na kinyume na agizo hilo katika mkutano wa 11 wa Bunge mwaka 2013 Serikali hiyo hiyo ya CCM ikawasilisha bungeni muswada wa sheria ya fedha na majedwali ya marekebisho ya kuongeza kodi ya mafuta ya taa kinyume cha agizo hilo.

Taarifa hiyo haiwezi kuinasua CCM dhidi ya kuendelea kukataliwa kwa kuwa imehusika katika maaandalizi ya bajeti ya Serikali na muswada wa sheria ya fedha kabla na wakati wa mkutano wa Bunge uliofanya maamuzi ya kuwaongezea gharama za maisha wananchi. Chama hicho kimeshiriki moja kwa moja kupitia vikao vyake vya kikatiba ikiwemo kamati kuu, sekretariati na kamati ya wabunge wa chama hicho.

Taarifa hiyo imethibitisha madhara ya Serikali ya CCM na wabunge wanaotokana na chama hicho wanavyoshindwa kusimamia maslahi ya umma kwa kuwa iwapo dhamira hiyo ingekuwepo katika hatua za awali wasingewasilisha bungeni mapendekezo hayo. Hata baada ya kuyawasilisha wangeyaondoa katika hatua zote kufuatia kodi hiyo kupingwa na kambi rasmi ya upinzani inayoongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

CCM itambue kwamba wananchi wanakumbuka kuwa kodi hiyo ya simu iliingizwa kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge na Rais kupitia kwa Waziri wa Fedha aliposoma bajeti ya Serikali ya CCM. Ilikuwepo kwenye Hotuba ya maandishi ya Waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa CCM lakini wakati wa kusoma akaruka sehemu hiyo na kutangaza kwamba imefutwa.

CCM ieleze katika hatua hiyo, wazo hilo lilitoka kwa nani mpaka likaingia katika kitabu cha hotuba ya Waziri na nini maamuzi ya Baraza la Mawaziri ambalo Mwenyekiti ni Rais (ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM) kwenye kikao kilichofanyika siku moja kabla ya yeye kusoma hotuba yake kilichojadili hatua za kikodi (tax measures).

Kifungu hiki kilirejeshwa kwa mara nyingine tena kwenye Muswada wa Sheria ya Fedha kupitia jedwali la Marekebisho lililowasilishwa na Waziri wa Fedha mwenyewe kwa niaba ya Serikali ya CCM na Bunge lenye kuhodhiwa na CCM likakipitisha. CCM iwapo ilikuwa na msimamo wa kuona kwamba kodi hiyo ni mzigo kwa wananchi kwanini haikuwasiliana na wabunge wake ambao ndio wengi katika Bunge kuhakisha kwamba wanaikataa.

Iwapo CCM haitajitokeza kutoa majibu na Rais hataagiza kwamba kodi hiyo isitishwe na muswada kuwasilishwa bungeni kuifuta, natoa mwito kwa wananchi kujitokeza katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni.

Mkutano huo uliandaliwa kwa lengo la kutoa mrejesho kuhusu yaliyojiri bungeni katika mkutano uliopita na kupokea masuala ya kuyawasilisha katika mkutano ujao. Aidha, uchambuzi utafanyika kuhusu rasimu ya katiba sanjari na juu ya mchakato wa katiba mpya.

Hivyo, kupitia mkutano huo saini zitaendelea kukusanywa kwa ajili ya kutaka kodi hiyo ya kumiliki kadi za simu isitishwe na muswada kupelekwa bungeni kuifuta kodi hiyo yenye kuongeza gharama za maisha kwa wananchi na kuathiri haki ya kupata na kutoa taarifa pamoja na uhuru wa mawasiliano.

Taarifa hiyo imedhihirisha namna ambavyo tumefika hapa tulipo kutokana na udhaifu wa Serikali ya CCM, uzembe wa Bunge (ambalo limehodhiwa na CCM) na ulegelege wa CCM.

Hivyo, umma uipuuze na kuendelea kuchukua hatua za kuiunga mkono CHADEMA katika dhamira na dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.

Imetolewa tarehe 18, Julai, 2013 na;

John Mnyika (MB)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
 
Hivi ninyi wanasiasa mbona mnafanya maamuzi bila kufanya/kutumia utafiti?

Matamko yenu siku zote yamekuwa yakiwagawa wananchi ina maana hamuwatumii

wataalamu kwa ushauri?

Sawa kwa sasa mnashinikiza kodi kuondolewa kwa hiyo hivyo vyanzo vingine mmekwisha vifanyia utafiti

kubaini kama navyo havitakuwa kikwazo kwa wananchi?

Vitu vingine sio kutanga tangaza tu kwenye media mnahitajika kuchukua hatua zenye manufaa na sio

kuuma-uma maneno kwakua kufanya hivyo mtaonekana kana kwamba mnafanya dili zenu na si kwa

manufaa ya watu.

Siku zote mjitahidi kuwa na lugha ya pamoja katika kuwakilisha kitu/vitu vyenye maslahi ya wengi

vinginevyo mtaonekana kana kwamba mmekurupa au mnatengenezo vitu vyenye majibu mepesi au
visivyowezekana ili mvitumie kujiimalisha kisiasa.

Binafsi napendekeza lipa kadri unavyotumia kama njia mojawapo ya kutunisha mfuko unaohitajika,

au ninyi wenyewe kwa kushirikiana na wenzenu mkatwe sehemu ya marupurupu yenu kutunisha mfuko huo.
 
Unaujua utaratibu wa kulifanya hilo unalolisema? Ndo maana wananchi wanamashaka na uwezo wa chama chako kuongoza nchi kama hata mambo madogo ya utendaji kama hilo unadhani ni swala la kumuita waziri na kuelekeza...

Kwanza ni ukweli kuwa wananchi hawana shaka hata kidogo na uwezo wa chama changu cha Chadema kuongoza nchi na ndio maana unafahamu kuwa katika chaguzi ndogo za udiwani zilizomalizika hivi karibuni wananchi wametupigia kura nyingi sana; Chadema 46% na ccm 49% lakini pia tumeweza kuaminiwa na kujinyakulia kata nne kutoka ccm, sasa unawezaje kujishebedua kuwa wananchi hawatuamini?

Cha pili, kila mara wabunge wenu wanakuwa na vikao vya party caucus ambavyo kazi yake ni kuweka msimamo wa kichama kabla ya kuingia kwenye maamuzi ya kupitisha bajeti, na pale ndipo ccm kupitia kwa wabunge wenu mlipoamua kuipitisha tozo yz simcard. Kama hiyo haitoshi muswaada wowote hauwezi kupelekwa bungeni kabla haujapita kwa baraza la mawaziri(baraza la ccm ambapo mwenyekiti wake ni mwenyekiti wa ccm taifa), kamati ya makatibu wakuu na kabla ya hapo tayari ccm inakuwa imeidhinisha mpango huo katika vikao vyenu vya nec na kamati kuu.

Tunajua hawa mawaziri wenu mnavyowapeleka peleka kama tiyara hawana maamuzi yoyote ya maana wanayofanya kwa akili yao au utashi wao kwahiyo kwa kumalizia nikufahamishe bwana mwenezi kuwa tunafahamu sana namna mnavyoiendesha serikali yenu kuliko wenyewe mnavyoifahamu.
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Nitasema tena. Nape wewe ni kijana mzuri tu, huwa unaonekana usoni hata unapotetea ufisadi kuwa unayoyasema hayatoki moyoni mwako. Kufanya kazi na mijitu katili kama Mwigulu, Kinana, Chenge na wengine wengi unaowajua vizuri ufisadi na umafya wao itakutesa moyo wako maisha yako yote ndugu yangu. Huko uliko siko na wewe wajua. Isikilize sauti ya Mungu wako, watanzania wanahitaji kukombolewa kutoka mikononi mwa watesi wao CCM. Chagua njia iliyobora kumtumikia Mungu wako, maana nina hakika Mungu hunena nawe sometimes. Unaweza kudhani utapambana na watesi hao humohumo ndani ya CCM lakini wewe mwenyewe ni shahidi - juhudi zako za kuvua magamba zimefikia wapi? "Toka ukatengwe nao asema Bwana wa Majeshi".
 
Mmeanza ule mchezo wenu wa kujitekenya wenyewe sio?We Nape hizi pumba kaongee na watu wa Lumumba ambao uwezo wenu wa kuwaza ulishakwisha.Raisi ndio mwenyekiti wa baraza la mawaziri wakati majadiliano ya hii bajeti yanafanyika hakuona kwamba si sahihi hadi aanze kuliongelea hili leo?We are tired of your silly public stunts
 
Sina hakika kama unajua unachokisema...laikini pia inawezekana hujui utaratibu unaotumika kufanya maamuzi ndio maana sijui nianzie wapi kukushauri. Swala likishapitishwa na bunge si swala la wabunge flani ni swala la bunge...

Mangapi yamepitishwa na bunge au serikali na Chama tukayapinga na yakabadilika? Kama unakumbukumbu nzuri fuatilia nani alianza kulipinga hili kati ya vyama vya siasa nchini.

Hoja nzuri Nape umetoa darasa zuri kwamba bunge likiamua huwa inachukuliwa kwamba bunge ndio limeamua, the same hata tukimchagua kiongozi yoyote akishinda anachukuliwa kama kiongozi wa wananchi hata kama hujamchagua, ila huyu mdau fangfangjt nae ana hoja katika paragraph ya kwanza kama changamoto kwa wabunge wote hasa wale ambao ni wengi kwa idadi wawe makini kwenye hizi issue ili kuwajengea image nzuri kwa wananchi waliowachagua maana pamoja na kwamba bunge limeamua lakini bado wao ndio wengi pia wananchi tunaangalia mantinki nzima ya msimamo wa chama na maamuzi yaliyofanyika bungeni kutokana na idadi ya wabunge ya ccm kuwa kubwa, all in all ni vizuri kama mmeamua kuonyesha msimamo kwani mwisho wa siku tutafurahi na maamuzi yatakayofanyika kwa imani kwamba hili suala likirudishwa bungeni wabunge wa ccm kwa wingi wao ni mtaji wa kuiondoa hii kodi

By the way tutafurahi kama kodi hii itaondolewa maana watu tuna line 3 za simu si kwamba tunapenda bali gharama za muingiliano ni kubwa baina ya mitandao pia ubora wa mitandao unategemeana na mazingira uliyopo ukiongeza na moderm bado wengine wanasaidia na line za wake zao ambao wapo majumbani hawafanyi kazi na mama na baba kijijini hivyo kuna uwezekano mtanzania mmoja akawa anamlki line 5 though ukiangalia kwa juu ana line 2 zake tu.
 
Kama ungekuwa genuine haya maneno ungetakiwa kumuita waziri Mgimwa na kumueleza nini cha kufanya lakini kwakuwa unafahamu kabisa kuwa serikali yenu ya ccm imeziba masikio wala haisikii ndio maana umeamua kuja hapa kutafuta huruma ya wananchi kwa kujifanya mnajali maslahi ya wananchi.

Wakati ccm mnafikiria kuianzisha hiyo simcrad tax at the first place mlitakiwa kufahamu kuwa wananchi wengi hali zao za kiuchumi ziko dhoofu na hawatoweza kuzimudu, na hata kama wapo wanaomudu lakini kuna maeneo mengine ambayo bado serikali ingeweza kujielekeza na kukusanya kodi ya kutosha kujiendesha.

Mkuu Mwita Maranya
Hapo kwenye red
Watawezaje kufikilia kua kunawatu hawawezi kulipa hio hela ikiwa wao hawajui kama kuna watu wanakosa hata mlo mmoja wa siku kwa kusa fetha za kujikimu. Hii ni sawa na ile kauli ya Malkia Marie Antoinette wa Ufansa alivyo waambia wananchi wake kua; "Kama hamna mikate si mle keki."
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Spika makinda nakamati yake yabajeti wameichimbia CCM kaburi..!maamuzi yao mengi niyakishabiki bila kujali mahitaji ya jamii!Endeleeni kukaa kimya kuhusu hela zetu zilizoko Uswiswi,waliopitisha manunuzi ya rada kwa bei ya juu,wanaoendelea kuwamaliza tembo wetu,unyama unaoendelea mtwara...namwisho kama chama mtuambie Rais Obama alikuja kufanya nini!hakika mwisho wa ccm kutawala umefika mwisho tena kwa kasi!
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Nape - Swali rahisi, tafadhali naomba jibu.

Tanzania tumefanya uchaguzi. Vyama vikaweka wagombea wao. Mgombea wa CCM akashinda kiti cha Uraisi na Wabunge wake wake ndio majority.Katiba yetu tuliyonayo inasema - Rais ndiye Kiongozi wa nchi na serikali. Tunaongozwa na Rais Mh. Dk. J.M.Kikwete. Kiongozi wa Serikali ya CCM (Sio ya Chama Kingine)iliyoshinda kihalali.Mh Rais amekaa na baraza lake la mawaziri wakaridhia kuanzisha hii kodi ya simu.Ikaletwa bungeni na viongozi wa serikali ya CCM. Ikapitishwa.Baada ya malalamiko ya wananchi Rais anatoa agizo kwa wahusika. Yeye si ndio Kiongozi mkuu wa serikali.Kwa nini asimwagize waziri alete bungeni mswada wa mabadiliko ya sheria iliyopitisha, kisha yeye ausaini mara moja? CCM si ndio inawabunge majority - mswada ukiletwa naamini hautakwama. Vitendo ndio vinaonyesha dhamira mliyonayo, tupunguze maneno. Matendo yetu ndio yatuongoze.
Angalizo: Mie si mwanachama wa chama cha siasa chochote.
 
We dogo Nape
Leo umejitahidi kujibu. Japo najua utakimbia muda si mrefu, kama walivyo ccm wenzako.

Kwa jinsi unavyojikanganya, hii ni kiashiria kwamba huko ccm kila mmoja na chake. Umoja sifuri.
 
Nape Nnauye; Mkuu, tatizo lako ni pale unapodhani uko vizuri kwenye propaganda hata kwa masuala yanayohitaji ukweli. unaposema msimamo wa chama una maana gani zaidi ya kuruka ruka kusudi CCM mkwepe lawama? Waziri Mkuu Mhe.Pinda ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na amenukuliwa akisema "wanaopinga kodi ya kadi ya simu hawana lengo jema na taifa" au yeye hahusiki na misimamo ya CCM? Kubali kwamba kuna udhaifu mkubwa haswa kwa wabunge wa CCM kwani hata kwa logic ya kawaida inajulikana kwamba wanajivunia majority votes bila kufikiri mara mbili jambo ambalo linakigharimu chama kwani wanapitisha masuala nyeti kishabiki. Ikumbukwe kwamba nje ya Mhe.John Cheyo na wabunge wa CCM hakuna wabunge wengine waliounga mkono kupitishwa kwa bajeti kwani walihitaji marekebisho zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE). Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati.

Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali. Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Kweli hivi ni vioja kama sio vituko, sio chama chako kinachoitishaga vikao vya siri kabla ya kuingia kufanya maamuzi bungeni kwa minajili ya kupitisha hoja za serikali hata kama hazina maslahi kwa uma!

Wabunge wa CCM huwa wanadanganywa kuwa kupitisha kila jambo linaloletwa na serikali bungeni ni kuwakomoa wapinzani,sasa naona hili limewaumbua sasa mnataka kudanganya umma wa Watanzania kuwa kuna msimamo wa chama na msimamo wa serikali ili hali serikali inaundwa na chama hicho hicho. Mbaya zaidi mwenyekiti wa chama hicho hicho ndiye Raisi wa nchi.

Ukweli ni kuwa kuna mtandao wa wasaka uraisi ulikuwa unataka kukusanya fedha kama zilivyokusanywa za EPA enzi zile mwishoni wa utawala wa Mkapa. Tofauti ni kwamba kipindi hichi makundi yamekuwa mengi sasa mnaharibiana wenyewe kwa wenyewe. Makundi yenu yanatufaidisha sisi wananchi kwani mali zetu zinakuwa salama kwa kutajana kama jinsi Mh. Sitta alivyotoa hadaharani kuwa ana wasiwasi na matumizi ya mabilioni ya fedha kwenye ziara ya Obama nchini.
 
Ukweli sasa ni upi?

Ukweli ni Upi.jpg

Back
Top Bottom