Kodi ya Simu: Serikali lazima isikilize kilio cha wananchi

Nape nakusifu kwa kuja hapa kujidhalilisha!thenki yuu vere machi

Hajajidhalilisha yeye mwenyewe ila ni pamoja na chama chakw, kwani anapisema wabunge wakipitisha, hao wabunge wako pake kwa ajili ya ccm au kwa niaba ya wananchi? Means wananchi wakikataa lazima serikali ikubalu kwamba walifanya maamuzi ya chumbani, na hii tabia ndiyo inayoigharimu ccm na serikali yake, ubabe acheni, muda sio mrefu tunakwenda kuwasahau kama KANU na wenzake. Hii nchi ni zawadi yetu wote tuliyopewa na Mungu na siyo ya Ccm peke yao. Tuheshimiane
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
Akili zimeanza kuongezeka kidoogo kidoogo!

Nasisitiza bwana mdogo Nape, utubu kwa kitendo mlichokifanya Soweto! Kitawamaliza nyie wahusika woote mark my word dogo!
 
ivi mkuu ni chama gani kimeshika madaraka sasa kama nyie ni chama tawala then mnalalamika chadema wafanyaje.nionavyo mnatengeneza anguko lenu wenyewe ni jukumu lenu kukaa ndani na kutoa suluhusho na sio kuja kulalamika hapa kama anavyofanya mnyika.take action.
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
 
kodi mpitishe wenyewe leo mnaikana na kusema ni mzigo kwa wananchi.
wakati huo huo JK anawaita wamiliki wa makampuni ya simu ikulu eti waangalie wafanyeje
huyu mfanyabiasha wa simu anataka faida,hivo wataongeza ktk muda wa maongezi,internet na simcard
bado hakuna kitakachopunguzwa mwananchi ndio atakaeumia..

pandisheni kodi wanayolipa makampuni ya simu walau ifike 60% ya faida wanayochuma
pandisheni kodi kwenye utafiti na uchimbaji wa gesi
pandisheni kodi kwenye madini walipe walau 65% both income na special tax..

Zile fedha walijitengea ikulu a kufuatilia miradi zifutwe ziingizwe kwenye miradi mingine muhimu.
Tuna utajiri wa kutisha lakini bado nchi maskini kwa sababu tunaongozwa na chama na watu wasiotumia akili zao kuongoza bali wameshikilia matumbo yao zaidi..

Rudisheni fedha walizoficha viongozi wako Uswizi na unawajua..la sivo CCM kwa heri
Kila mtu hapa lazima akaeneze ubaya wa CCM katik familia yake ili tuwazike vema 2015.
naona mmnaitumia TBC kama chombo chenu kuuwa upinzani lakini watu wameshaamka.
sio kama zamani tena mtahonga kwa kanga na kofia...this time no.
 
...wabunge wako hawakuliona hili wakati wanapitisha...? mbona hatuwaelewi,au msimamo wa ccm bungeni ni tofauti na ule wa ccm nje ya bunge..?
 
Yaani hii inaonyesha kwa sehemu chama ambavyo hakina Nguvu kwa serikali yake bali kuna mafisadi wachache wanayoiongoza na kuiendesha serikali kwa nuvu yao ya pesa.
Kama kiongozi wa juu wa Chama nape ilibidi useme mmetoa maagizo gani kwa serikali yenu na mpaka lini wawe wametekeleza na sio na wewe ni kama unatoa wazo. Na hapa ndio naona udhaifu wa Mwenyekiti wa chama kuwa rais. Haya ndio madhara yake.
 
Unaujua utaratibu wa kulifanya hilo unalolisema? Ndo maana wananchi wanamashaka na uwezo wa chama chako kuongoza nchi kama hata mambo madogo ya utendaji kama hilo unadhani ni swala la kumuita waziri na kuelekeza...
Wewe Nape vipi? Wananchi gani wana mashaka na uwezo wa chama( najua ulimaanisha CDM ingawa hukutaja) chake kuongoza nchi? Twende kwenye chaguzi, uchaguzi wa mwisho kufanyika ni ule wa madiwani Arusha 16/7 jee matokeo yalikuwaje? Ninavyo fahamu mie matokeo yalikuwa 4-0. Sasa hao wenye mashaka wewe umewatoa wapi?
Wewe ni kiongozi jaribu kuwa mkweli ingawa kwa tabia ya chama chako ni ngumu.
 
Mkuu nakubaliana na wewe, Nape ana wakati mgumu sana, haridhishwi na yanayofanyika CCM, Nnape ni mtu mzuri sana, anapopiga vita ufisadi huwa ni kutoka moyoni, lakini wakuu wake huwa wasanii tu, Walidiriki hadi kumzuia asikanyage Igunga kwenye uchaguzi mdogo.
Nnape hapendi CCM na ndio maana sera zake ni za tofauti.

Namsihi Nnape asiogope, afanye maamuzi magumu, liwalo na liwe.
Nitasema tena. Nape wewe ni kijana mzuri tu, huwa unaonekana usoni hata unapotetea ufisadi kuwa unayoyasema hayatoki moyoni mwako. Kufanya kazi na mijitu katili kama Mwigulu, Kinana, Chenge na wengine wengi unaowajua vizuri ufisadi na umafya wao itakutesa moyo wako maisha yako yote ndugu yangu. Huko uliko siko na wewe wajua. Isikilize sauti ya Mungu wako, watanzania wanahitaji kukombolewa kutoka mikononi mwa watesi wao CCM. Chagua njia iliyobora kumtumikia Mungu wako, maana nina hakika Mungu hunena nawe sometimes. Unaweza kudhani utapambana na watesi hao humohumo ndani ya CCM lakini wewe mwenyewe ni shahidi - juhudi zako za kuvua magamba zimefikia wapi? "Toka ukatengwe nao asema Bwana wa Majeshi".
 
'Those who make peaceful revolution impossible will make violent revolution inevitable' By John F kennedy
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

What a nonesense! Yan msimamo wa chama unautoa wewe au ulishatolewa bungeni wakati nyinyiem mnagonga meza?
Tena na huyo mzee wa kaya anavyojua kusikilizia upepo sijui atafanya sarakasi gani saiv.
Go to hell!
 
Tutalumbana weee humu JF na kwenye majukwaa ya kisiasa,lakini ukweli ni kwamba sheria ilishapita bungeni,imesainiwa na Rais huyuhuyu ambaye naye amengia katika orodha ya walalamikaji kama mimi na wewe....(USANII MTUPU) na imeshaanza kutekelezwa!!

Na jamaa hawa CCM ndani ya miezi miwili tu (Julai & Agosti) watakuwa wameingiza Bil 56!!....Na kama ni kweli wanatafuta fedha za kugharamia kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015 ktk chama chao,basi watakuwa wamefanikiwa kwa kiwango flani na kama kweli wamedhamiria kuifuta,basi itakuwa kuanzia mwezi Septemba baada ya bunge kukaa kuanzia mwishoni mwa mwezi wa 8!!

ON CONTRARY TO THAT; na nionavyo mimi ni kuwa tatizo si watu kulipa kodi hii na zingine zozote zile zinazoaanzishwa na serikali, ila tatizo liko kwenye pesa tunazolipa katika kodi hizo zinafanya kazi gani( And please don't tell me kuwa tumejenga barabara za rami kilometa 8000 nchi nzima au tumejenga shule za sekondari za kata na nyimbo zingine zinazofanana na hizo mnazoziimba kila siku kuwadaa wachache wanaofikiri kwa makario kwani haya mliyofanya CCM hayalingani na umri wenu wa kushika dola wa miaka zaidi ya 50 sasa!!)....Mpaka sasa tulitakiwa tuwe na barabara za rami za zaidi ya kilometa 30,000 na kila shule kila mwanafunzi kitabu kimoja,dawati lake,laptop moja,walimu wa kutosha,maabara za sayansi katka sekondari zetu,madawa ya kutosha katk zahanati na vituo vyetu vya afya na pasipokuwapo na mtumishi wa umma eti anayeidai serikali ya CCM iliyo madarakani kwa miaka zaidi ya 50 hela ya uhamisho,malimbikizo ya mishahara nk nk. Ni upuuzi na ni kukosa kujenga mifumo imara na thabiti and THIS IS A TOTAL FAILURE!!

Kwani pamoja na makusanyo makubwa ya kodi toka TRA yanayokimbilia bil. 800 kwa mwezi, bado hali za wananchi ni mbaya na umaskini unaongezeka badala ya kupungua; angalia na tembelea barabara za vijijini hazipitiki,mashule hayana vifaa vya kujifunzia na kufundishia,mashule hayana maabara,watumishi wa serikali (rejea madai ya walimu,madaktari,manesi nk nk) wanadai madeni ya miaka na miaka, zahanati,hospitali na vituo vya afya havina madawa na vifaa tiba na vitendea kazi vingine, miradi mingi ya maendeleo ina miaka imesimama kwa sababu eti serikali haina pesa!!......Hiki Bwana Nape ndicho kinachogomba na ndicho kinachowafanya CCM ionekane ovyo. Tatizo lenu kuu liko kwenye SERA na MIPANGO yenu na namna yaani MIFUMO mnayotumia kutekeleza mipango yenu ni ya hovyo na iko SO CORRUPTED na huu UFISADI umeshafikia ktk kiwango kibaya kiasi cha sasa damu ya binadamu zinamwagika kama sacrifice ya kuendelea ku-survive kwa mafisadi (rejea tukio la bomu la Soweto - Arusha ktk mkutano wa CHADEMA).

Kwa sasa
dawa yake si ninyi kujirekebisha bali kulazimishwa kujirekekisha kwa KUONDOKA madarakani na kuwaachia wengine wenye mawazo mapya nao TUWAJARIBU!!...Kwani ilivyo sasa ni kuwa kuanzia IKULU ya JAKAYA KIKWETE(rejea kashfa ya kamuni hewa ya kufua umeme kama mfano ulio wazi ya Richmond) hadi ofisi ya kitongoji cha kijiji ni RUSHWA na UFISADI mtupu. Ni wazi katika hali kama hii, serikali lazima ipate taabu sana kuweka mipango yake na kuungwa mkono na wananchi bila kulalamika kwani HAIAMINIKI!!....Ona mnavopingana ninyi kwa ninyi katk suala hili la sim card tax na bado mengi mengine yatakuja na kila mtu ktk CCM na serikali yenu atakuwa anaruka ki-manga!!

To me, bwana Nape, hii ndiyo problem yangu
na pengine hii ndiyo problem ya kila mtu anayepinga kodi hizi za ajabu ajabu na ni mara mia mngetafutia fedha hizi kwenye maeneo mengine kama migodi ya madini,mafuta na gesi yaliyojificha ambako hayagusi maisha ya kila siku ya watu moja kwa moja
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
Kushukuru na kupongeza hakutoshi. mwambie achukue kodi kwa wachimbaji wa madini, afute misamaha yote. Hivi Symbion power wanalipa kodi kweli???
 
Huko kote baada ya 2015 ni CDM kaka bila kusahau Iringa yoote,, Nape asidanganye watu bali aseme ukweli kuwa serikali yao si sikivu na asubili wanainchi wataifanya iwe sikivu 2015
Mkuu Iringa bado wapo nyuma sana kwenye mabadiliko... Uchaguzi wa madiwani uliopita Iringa na Njombe ndiko CCM ilipata kura nyingi zaidi!!!
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

Poor Nape.
Bandiko lako linalenga kupotosha ukweli wa swala hili.Nadhani una amini kuwa utafanikiwa katika hilo,inawezekana,Natamani sana kuendeleza huu mjadala mpana (according to you!) kwa kurejea mazungumzo yako na kuangalia ukweli ulivyo:

  1. Rais JMK ni mhusika nambari moja hivyo kusema eti "wahusika walitafakari upya" ni uongo.
  2. Huwezi kuitenganisha serikali ya CCM na Chama cha Mapinduzi.Serikali iliyoko madarakani inatokana na Chama cha mapinduzi.Kwa maneno mengine they are one and the same!
  3. Hapakuwa na ulazima wowote kwa watu makini kuingia katika mtego huu kwa sababu njia mbadala za kuongeza mapato ya serikali zipo,zimeainishwa na watu chungu nzima tu wakiwepo Kambi rasmi ya upinzani bungeni,report mbalimbali,wasomi na wachambuzi wengi tu wa masuala ya uchumi na sera.
  4. Hata siku moja huwezi kujaza kapu linalo vuja!Kwa hali jinsi ilivyo ni lazima mjadala wa sasa uwe mpana kiasi cha kulazimisha mabadiliko katika matumizi yasiyo ya lazima au yasiyona tija ya serikali,mfumo wa ukusanyaji kozi kwa ujumla wake,Misamaha ya kodi,ukwepaji wa kodi,uwajibikaji na kukosekana kwa ufahamu wa uhalisia wa hali za kimaisha za watanzania walio wengi(Disconnection between the ruling and ruled classes)
  5. Hii inatokana na ukweli kwamba tunapaswa kutoka katika mazoea yale ya kutafuta ufumbuzi kwa matatizo tuliyo yasababisha wenyewe na kwenda katika utendaji unao kwepa kutengeneza matatizo hayo in the first place.Hivyo basi nawataka watanzania wote tusikubali kuridhika na kuondolewa kwa tozo hili peke yake,tujadili uhalali wa tozo zingine zilizowekwa katika sector hii muhimu ya mawasiliano.Pia tudai kuwawajibisha hawa watu walio tufikisha hapo.Tudai tulicho stahili kukipata na sio walichotupa!
  6. Tusikubali kuwaruhusi watu walewale watumie muda na rasilimali zetu kurekebisha makosa ambayo hawakupaswa kuyafanya bila kuwawajibisha!Maana ni kawaida ya serikali hii kufanya mambo bila weledi na baadae kutufanyia mazingaombwe haya ya kusema mkono wa kushoto ulikuwa haujui wa kulia unafanya nini!
  7. Uozo huu unadhihirisha maneno ya Baba wa taifa aliposema "Serikali corrupt haikusanyi kodi....itaishia kukimbizana na watu masikini mabarabarani tu"

Wakati wananchi wakilalamikia ongezeko la tozo za ushuru na kodi mbalimbali katika bajeti ya Serikali ya 2013/14, imebainika kuwapo misamaha ya ongezeko la thamani (VAT) kwa bidhaa mbichi za kilimo, mifugo na mazao ambapo serikali hupoteza mabilioni ya shilingi kila mwaka.Uchunguzi unaoonyesha kuwa misamaha hiyo imekuwa ikitolewa kwa miaka sita mfululizo na kuligharimu taifa wastani wa Sh 503bilioni, fedha ambazo zingetosha kwa bajeti ya wizara kumi za Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/2014Bidhaa na vitu ambavyo vimekuwa vikipewa misamaha hiyo ni pamoja mazao ya kilimo vikiwamo nafaka na mbogamboga pia wanyama na ndege wa kufugwa na vitu hivyo vinapatikana kwa wingi hapa nchini.Licha ya misamaha ya kodi kuwepo kisheria, lakini imekuwa ikitumika vibaya, hata mazao ya kilimo na mifugo inayopatikana kwa wingi pia nchini. Mazao haya yamekuwa yakisamehewa kodi hiyo, hivyo kuathiri uzalishaji wa ndani.

Je?Kodi hii ilikuwa na ulazima? HAPANA!

Matokeo ya utafiti uliofanywa na Jopo la Taasisi za dini hapa nchini waliyoiita ‘The One Billion Dollar Question’ unasema na hapa nanukuu " In total, we estimate that Tanzania has in recent years been losing revenues ranging from $847 million - $1.29 billion (TShs 1.35 – 2.05 trillion) a year – thus the median figure is $1.07 billion (TShs 1.7 trillion). This figure is, under-estimate since it does not, for example, include tax revenue losses from other forms of unreported trade such as smuggling, for which no data are available.

The bottom line?You have a lot....just plug the holes!

Naomba kila mwana JF atakaye pata wasaa aipitie report hii http://kadulyu.files.wordpress.com/2012/08/onebilliondollarquestion.pdf mtu kama Nape anapokuja na kutuaminisha kuwa kulikuwa na ulazima wa kuingiza kodi hii tumwambie bila ya haya.....mwongo wewe!
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
dah! nape fahamu zimeanza kurudi polepole any ways ni mwanzo mzuri lakini uguswe kuanzia ndani ya moyo wako ili uweze kutetea wanyonge vizuri.
 
CCM mlikuwa wapi? leo unatueleza mambo yasiyoeleweka,kodi hiyo imepitia vikao mbalimbali ikiwemo kikao cha baraza la mawaziri amba cho Rais ni Mwenyekiti sasa kipi ambacho rais hakujua hapo au ni usanii mnatuletea.
Mimi nadhani CCM inahitaji kupumzishwa kwa sasa tuangalie Chama kinachoweza kumtetea mnyonge huyu muuza vitumbua na nyanya! anayenyonywa leo na mafisadi waliojaa ndani ya CCM!!!!
 
Aibu ni kwa wabunge waliokwenda bungeni kufanya hivi
wasira chapa usingizi.jpg
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.

lkn nape,kuomba serikali iiondoe hii tozo maana yake ni kukiri kuwa serikali na bunge la ccm walifanya makosa kubuni na kupitisha hii tozo! kwa nini hukuanza kuwaomba radhi kwanza wananchi baada ya kuckia malalamiko yao!?km ulisahau ndo nimekukumbusha ss.
 
kodi mpitishe wenyewe leo mnaikana na kusema ni mzigo kwa wananchi.
wakati huo huo JK anawaita wamiliki wa makampuni ya simu ikulu eti waangalie wafanyeje
huyu mfanyabiasha wa simu anataka faida,hivo wataongeza ktk muda wa maongezi,internet na simcard
bado hakuna kitakachopunguzwa mwananchi ndio atakaeumia..

pandisheni kodi wanayolipa makampuni ya simu walau ifike 60% ya faida wanayochuma
pandisheni kodi kwenye utafiti na uchimbaji wa gesi
pandisheni kodi kwenye madini walipe walau 65% both income na special tax..

Zile fedha walijitengea ikulu a kufuatilia miradi zifutwe ziingizwe kwenye miradi mingine muhimu.
Tuna utajiri wa kutisha lakini bado nchi maskini kwa sababu tunaongozwa na chama na watu wasiotumia akili zao kuongoza bali wameshikilia matumbo yao zaidi..

Rudisheni fedha walizoficha viongozi wako Uswizi na unawajua..la sivo CCM kwa heri
Kila mtu hapa lazima akaeneze ubaya wa CCM katik familia yake ili tuwazike vema 2015.
naona mmnaitumia TBC kama chombo chenu kuuwa upinzani lakini watu wameshaamka.
sio kama zamani tena mtahonga kwa kanga na kofia...this time no.
Hawahitaji kupandisha kodi katika maeneo uliyotaja, bali wanahitaji tu kukusanya kikamilifu kwa kiwango kilichopo na wataongeza mapato ya Serkali.
 
Kumekuwa na mjadala mpana sana juu ya kodi iliyopitishwa na bunge ya kadi za simu za mkononi. Kimsingi kama Chama tumeshatoa msimamo juu ya kodi hii.(SERIKALI IANGALIE VYANZO VINGINE NA KODI HII IFUTWE).

Ninamshukuru na kumpongeza Rais kwa msimamo wake juu ya hili. Agizo la Rais kwa wahusika kulitafakari upya swala hili ni la muhimu litekelezwe kwa wakati. Hapa nataka kusisitiza tu kuwa ni lazima serikali isikilize kilio cha wananchi ambao ndio chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Kinachonitia moyo mijadala mingi kwasasa juu ya hili imehusisha mapendekezo ya maeneo mbadala ya wapi pengo litakalosababishwa na kuondolewa kwa kodi hiyo litakavyozibwa. Hapa serikali lazima ionyeshe usikivu.
Since you can not CONVINCE Tanzanians, you are trying to CONFUSE them! Unataka ionekane eti CCM inataka tozo lilondolewe wakati Serikali ndo inataka tozo hiyo iwepo, ukweli tunaujua, CCM na Serikali ni kitu kimpoja
 
Back
Top Bottom