Mie sipingi kabisa kulipa kodi yoyote kwa maendeleo ya nchi yangu.Nipo tayari kukatwa kodi ya SIM,nipo tayari kuchangia ujenzi wa reli ya Kati,nipo tayari kuchangia ujenzi wa barabara na nipo tayari kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ya ujenzi ya umeme kama nitahitajika kufanya hivyo.
Lakini kabla ya kuanza kuchangia,ninaomba mniambie wale wote waliohusika na kesi za kifisadi za Richmond,EPA,na nyingine mbalimbali mmewachukulia hatua zipi mpaka sasa!La sivyo mtakuwa mnanifanya niamini huu pia utakuwa ni mradi wa kufanikisha ufisadi kama miradi mingine iliyofanyika ambayo wahusika mmeshindwa kuwachukulia hatua.
Hamuwezi kutuambia tuwe WAZALENDO kwa nchi yetu, kwa kuchangia kodi mbalimbali wakati nyie viongozi mmeshindwa kuwa WAZALENDO wa nchi yenu kwa kuwakamata na kuwashitaki wale wote waliohusika kwenye matumizi mabaya ya kodi za nchi ambazo tumekwishachangia mpaka sasa!
HAIWEZEKANI!
Unless mtuambie kuwa hv sasa nchi hii imekuwa ya ki-dicteta,na mnaweza kutufanyia vyovyote mnavyotaka bila kutushirikisha sisi wananchi katika maamuzi makubwa kama haya!
Bila kuwachukulia hatua hawa MAFISADI waliotuhumiwa kwenye matukio hayo ya kifisadi yaliyokwishafanyika naomba mjue tu kuwa sitashiriki katika zoezi hilo na kama mtachukua kodi hiyo kwa nguvu basi tambueni kuwa SITAITAMBUA RASMI SERIKALI HII kwani sidhani kama kuna serikali ya aina hiyo DUNIANI na AKHERA!
ACHENI UNAFIKI!