Kodi ya SimCard sasa kuanza mara moja!

Kodi ya SimCard sasa kuanza mara moja!

bora mie niko bongo lakini natumia laini ya safaricom na airtel ya kenya.
 
CCM CCM ahhhh chama cha mapinduzi CCM namba wani, wananchi wanajua CCM namba wani!
 
Tatizo hawana akili mtu asipolipa kodi anakamatwa ina maana wanaodaiwa watakamatwa inamaana wenye line nne za Voda, Tigo, Airtel na Zantel wanadaiwa elfu 12. Mtanzania wa kawaida anazipata wapi jamani, Afu wanafanya kimya kimya.
 
PAYE hulipwa kulingana na Basic salary, kodi ya mapato hulipwa kutokana na mapato, VAT hivyohivyo. Kama kila nikinunua airtime nalipia kodi kwanini basi kodi ya simcard (kama kuna ulazima wowote kuwepo) isitozwe maramoja tu kwa mwaka kama ambavyo road licence hulipwa maramoja kwa mwaka? Ama ni aina fulani ya adhabu???????
 
kaka hawa ccm tuwafanyaje jamani kwanini wanatuendesha kama golikipa anavyoendeshwa uwanjani kuangalia mpira utaingia golini au la? wameniuzi sana tena sana hawajui kuwa kuna watu ambao wanategemea simu kula ugali
CCM wamesha tuona sisi ni bendera fuata upepo.
Wanatuendesha kwa remote control a.k.a kitendambali
 
Naungana na Juliana Shonza bora serikali ikate toka mwezi wa kwanza mwaka huu 2013. Watumiaji simu tupo kama 7mil sasa ukichukua 7m * 1000* 3=21B . Hapo tayari ushatengeneza kilometa 26 za barabara Serikali oyee Ahsanteni
kijana kwenye hili atakayekuunga mkono ni chizi na limbukeni, jalibu kufikilia babu na bibi zako uliowanunulia simu ili huwe unawajulia hali acheni upumbavu, mnafaham hadi sasa kodi ya vocha za sim ni kiasi gani au unaongea tu ili uonekane? acha UNYANTIRA
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

Kwahiyo ukotayari kukatwa nyuma.
 
Hahaaaa eti vipesa vyakupaka rangi kucha ,we unajua hayo tu ndo upeo wako wakufikiri ulipofikia na ww.
Serikali isiyokusanya kodi ni legelege
ccm si serikali legelege ni lazima ikusanye kodi ili kupush maendeleo
Tatizo lenu mnaleta mahaba ya vyama kwenye mambo ya msingi,kila kitu mmezoea kupinga.
kwakifupi hamueleweki.
Tozo liko palepale

Ccm si serikali legelege.......! Hapa dada yangu umejikaza tu kuandika! Anyway! Ata hivo unajitahidi sana kujitetea maana ninavosoma majibu ya watu wanayokujibu yanakatisha tamaa.
 
Kuna mambo mawili yataigalimu sana Ccm kwenye.uchaguzi wa 2015. Swala la katiba iwapo watazidi kucheza rafu na kodi ya simcard!
 
Nimesoma habari kwenye mitandao ya kijamii kuwa serikali ya Jamuhur ya Muungano wa Tanzania imeridhia tozo ya kila mwezi ya kadi za cm ambayo ni Tsh 1000.Je haya ndo maisha bora yaliyoahidiwa na serikali?Inashangaza kuwa tozo hyo inaanza mwez october kwa sharti la kukata kodi hyo kuanzia mwez july mwaka huu.Hivyo wananch watatozwa sh 3000 kwa maana ya july,august na septemba.Namfikiria sana bibi aliye kijijin kwetu kule Sungwizi mkoani Tabora anayesubiri kupigiwa tu.Haya ndo maisha bora tuliyoahidiwa na serikal ya chama cha mapinduzi.Sitaki kuamin kama viongoz wang wa serikali ni wavivu wa kufikiri.Kwel wameshndwa kubuni vyanzo vingne vya mapato mpaka kwenye tozo ya kadi za cm?wazibe mianya ilyopo sekta mbalmbali kama vle bandari,wafanya biashara wakubwa walipe kodi,wawadhibiti wakusanya mapato ipasavyo kwan wanapiga dili nying.Zipo sehem nying ambazo zipo zipo tu bila usimamizi wa kutosha.Serikal kuruhusu tozo za kadi za cm ni kuwaonea wananchi.Serikal ifikirie vyanzo vngne vya mapato.Waache uzembe!!
 
tafasiri yake kwa kiswahili serikali -------
 
Wakati mwingine hizi sumu ya siasa ni sawa na ya Alshababu au Alkaida.Mtu unatetea uovu kama huna akili nzuri!? Hivi ni njaa au ni ugonjwa?!

Mkuu humu ndani kuna watu wa namna nyingi, hata mumiani wamo ila kwa mwendo huu tutaumia sana.

Mpaka kuja kulifikia sanduku la kura tutakua tumepigwa mijeredi ya kutosha.
 
Kuna mambo mawili yataigalimu sana Ccm kwenye.uchaguzi wa 2015. Swala la katiba iwapo watazidi kucheza rafu na kodi ya simcard!

Hii kodi ya sim card itafutwa katika budget ya 2015/2016 ili kuwahadaa watanzania kabla ya uchaguzi mkuu na watakuja na sababu kama serikali sikivu ya CCM imesikia kilio cha wananchi na hivyo tumeamua kufuta kodi hii kumbe wanachokitafuta na kura za watanzania hasa wale wasio na uelewa wa kuchambua mambo.
 
machungu ya kiwango hiko hayanabudi kutokea ili ule mwisho wao upate kufika kirahisi ! haya shime wananchi, haya shime wapinga ufisadi , akili ndogo haiwezi kutawala akili kubwa...wameshindwa kutoza vyakutosha kwenye Gas, Dhahabu na Maliasili wanatusukumia mizigo wananchi

Mi naona mzilipe, watakao kaidi amri "wapigwe tu" ili iwe fudisho 2015. Hayo ndo bora maisha mlo ahidiwa na mliowachagua.
 
Tatizo hata tukilipa hiyo kodi ni kuongeaza uraji kwa mafisadi hakuna uwajibikaji na uzalendo tz
 
Back
Top Bottom