Kodi ya SimCard sasa kuanza mara moja!

Kodi ya SimCard sasa kuanza mara moja!

Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

Nenda TRA wakukate, wakishindwa nenda kitaa watakukata tu
 
Ivi hakuna njia ingine ya kuweza kukusanya hizo bilioni178 zinazotakiwa kwenye bajeti iliyopangwa? Maana kwa rasilimali zilizopo nashindwa kabisa kuelewa kwanini tunashindwa kukusanya kwenye vyanzo vingine!
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

Ndo njia pekee ya kuendelea kuishi kwako, pole, hata ukiambiwa utembee uchi utatembea kisa tu ni ccm imesema.. you poor thing..! I never imagined that you could end up like this.
 
Kweli magamba akili zao fupi hii itakuwa mbinu ya mr bumbuli awalaghai wananchi wake kwa kuwalipia kodi ili wasimtose ubunge
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yanguNaomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.Nawasilisha.

mwandalie Papuchi Nchemba yu karibu kurejea
 
si hivyo tu ndugu. watu wa dar walivyozoea kutumia tigo akienda kishapu maana yake hatopatikana. nchi hii kuna baadhi ya maeneo hakuna network ya sim je tutawasilianaje?
 
Wana jukwaa! Hivi ina maana serikali yetu ya JMT haiwajali wananchi wake? Nakumbuka tuliahidiwa kwamba kodi ya Tshs 1,000/- ya line ya simu haitochajiwa. Nimeshtuka nilivyosoma kwenye gazeti la Tanzania Daima 24/09/2013 kwamba TRA imeagiza makampuni ya simu kutoza kodi hiyo kuanzia mwezi wa saba mpaka sasa tena kwa mkupuo. Hii ina maanisha kila mwenye line ya simu atatozwa Tshs 3,000/-, acha wale wenye line zaidi ya moja ambao watatozwa zaidi. Watanzania wenzangu mnalionaje hili? Hebu fikiria yule mtu ambaye kupata kipande cha muhogo kwaajili ya chai yake na familia ni tabu sasa atozwe hiyo kodi itakuweje? Kwa ukweli binafsi imeniumiza sana, hasa nikikumbuka maneno ya spika kwamba nanukuu "SIDHANI KAMA KUNA MTANZANIA ATASHINDWA KULIPA SHS 1,000/- WAKATI ANAPATA HELA YA KUNYWA BIA". Hii ni dharau sana kwa wale wanaohangaika kupata hata hiyo shs mia ili wanunue kipande cha muhogo wa chai na wakishakula hiyo ni mpaka jioni au wengine mpaka kesho tena.

Kukumbushia kwa tunaopata bahati ya kuchungulia magazeti, Mh. Halima Mdee alipeleka hoja binafsi ya kupinga kodi hiyo kwenye bunge lililomalizika baada ya kugundua udanganyifu wa Serikali lakini hakupewa nafasi ya kujadiliwa kwa hoja hiyo.

Angalizo: Naomba tuchangie kama watanzania na kama watu tunaowajali wenzetu na sio kushabikia mambo ya siasa, hii tunaongelea yule mtu ambaye anajitahidi kusave Shs 250 kwenye line yake kwa mwezi au zaidi ili akipata shida ambip mtu ambaye anajua atampa msaada.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI VIONGOZI WETU.

WATUMIAJI wa simu wapatao milioni nane wapo hatarini kufungiwa simu zao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, Tanzania Daima limebaini.
Tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeziandikia kampuni za simu waraka wa kuzitaka zianze kukata kodi mpya ya laini (simu card) mara moja kuanzia Julai 30, 2013.
Hatua hiyo inatokana na serikali kushindwa kufuta kodi hiyo ya sh 1,000 iliyopitishwa na Bunge kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete baada ya kukutana na wadau wa sekta ya mawasiliano.
Kwa maana hiyo kila anayemiliki laini moja ya simu atakatwa sh 3,000; anayemiliki laini mbili sh 6,000 na anayemiliki laini tatu sh 12,000, lengo ni kuhakikisha serikali inakusanya sh bilioni 178 zitakazopelekwa kwenye bajeti kuu ya serikali.
Watumiaji wa simu sasa watalazimika kulipia kodi hiyo ya miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba kwa wakati mmoja.
Bunge kupitia Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) lilitaka kuwapo kwa kodi hiyo ili kusaidia shughuli za bajeti ya Serikali Kuu.
Kupitishwa kwa kodi hiyo kuliibua malalamiko ya wanasiasa dhidi ya Chenge anayelazimisha kuwapo kwa kodi hiyo, huku akishindwa kuamini kwamba kuna Mtanzania anayekosa sh 1,000 kwa mwezi kwa ajili ya laini ya simu.
Malalamiko hayo yaliendelea hadi kwa wananchi na baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliotaka posho za wabunge zipunguzwe ili kuziba pengo hilo badala ya kuwabebesha wananchi mzigo.
Inadaiwa kwamba msimamo wa Chenge unaungwa mkono na Spika wa Bunge, Anne Makinda, jambo lililosababisha kutojadiliwa kwa hoja binafsi ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA) iliyohusu kodi hiyo katika mkutano wa Bunge lililopita kwa kisingizio cha kukosekana kwa muda wa kufanya hivyo.
Hata hivyo, takwimu zilizotolewa na kampuni za simu zinaonyesha kuwa miongoni mwa wamiliki wa laini za simu milioni 22; milioni nane wanatumia chini ya sh 1,000 kwa mwezi.
Baada ya malalamiko hayo, Rais Kikwete alikutana na wadau wa mawasiliano ambao ni wamiliki wa kampuni za simu Tanzania (MOAT), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kisha kuwaagiza waiondoe kodi hiyo.
“Rais alisema lengo kuu la mkutano huo liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la sh bilioni 178 zitakazopotea katika bajeti iwapo kodi hiyo itafutwa.
“Alisema hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha kujazia pengo litakalotokeza huku tayari Bunge limezipangia matumizi,” alinukuliwa Makamba baada ya kikao hicho na rais.
Kwa upande wake, rais alikaririwa akiwaambia wadau hao wa mawasiliano kwamba: “Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito, na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu.”
Licha ya agizo hilo la rais kutekelezwa kwa MOAT kutakiwa kuongeza kodi nyingine iitwayo ‘Excise duty’ kutoka asilimia 14 hadi 17 bila kujali kwamba katika Bunge la bajeti kodi hiyo iliongezwa kutoka asilimia 12 hadi asilimia 14, tozo hiyo ya laini za simu haijaondolewa.
Wachambuzi wa masuala ya siasa na mawasiliano walisema kutojadiliwa kwa mabadiliko ya kodi hiyo ya simu ni dalili kwamba Waziri wa Fedha amezidiwa nguvu na kiti cha spika kinachounga mkono hoja hiyo ya Chenge na kushindwa kutekeleza agizo la rais.
Wataalamu wa mawasiliano walilieleza gazeti hili kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kutaifanya Tanzania kuwa na kiwango cha juu cha kodi kuliko nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ushauri wa wataalamu hao ulibainisha kwamba kuongezeka kwa kodi hiyo kunaleta nafuu kidogo kuliko ile ya laini za simu inayomuumiza zaidi mwananchi wa kawaida.
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

usihofu utakatwa tigo kwanza uchangie pato
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.
acha ushabiki wa kisiasa wewe unaongea kama mjinga wa mitaani hapa ni kwa maslahi ya wananchi sasa wewe kama mtu uliepewa dhamana kuitetea tanzania kwa upande wa vijana ndo unatetea nini hapo? inasikitisha sasa kama mpaka sasa hujielewi. sisi kila tutumiapo simu tunatozo la kodi kwa makampuni ya simu, inatosha kwa serikari kukusanya kodi kwa hayo makampuni na sio kuongeza mzigo kwa wananchi. shame on u!
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

Wakati wasichana wenzako wanavaa Weaving kuonesha uzuri wao wewe unavaa Weaving
kuonesha ni wa jinsia gani haha!ha! Bila weaving wewe ni dume hivi Nchemba alipendea nini.
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

wewe bado hujapona sawasawa!
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

Hamna kitu kibaya kama kuwa kibaraka!

Unaweza hata kuuza utu wako kuwaridjidha mabwana zako!

Wewe ni mmojawapo.

Fanya hata kazi ya mama ntilie uachane na kutumika na wanasiasa!
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

kodi ya simu itakua ndo sera yetu 2015, cdm ikichukua nchi hakuna kodi ya simu
 
Nimehangaika kusoma thread kumbe source ni jarida la udaku wa kisiasa?
Anyway najisikia fahari kuchangia pato la nchi kwa maendeleo ya nchi yangu
Naomba kukatwa kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu.
Nawasilisha.

Mi sidhani kama kuchangia ni tatizo, tatizo kile tunachochangia kinatumikaje? Au ndo kinachotwa na mafisadi wa ccm kama alivyofanya Nimrodi BOT na Tanesco, Rostam kwenye Richmond?

KWA KIFUPI KUNA TATIZO KUBWA SANA KWENYE UWAJIBIKAJI JUU YA MATUMIZI YA RASILIMALI ZA UMA. TATIZO HILI LINAITAFUNA NCHI KILA KUKICHA.
 
Ninahofu na uwezo wa kufikiri wa Waziri wetu wa Fedha kwani ni juzi tu alikubaliana na Waziri wa Rwanda kurekebisha ushuru wa magari yanayovuka mpaka kwa kelele za wafanyabiashara wa malori ambayo wanashare lkn Leo anashindwa kukubaliana na matakwa ya watz wanaolalamikia kodi hii ambayo ni mzigo kwawananchi wengi
 
Mbona wameshaanza kukata tangu zamani,sababu ya kupandisha vifurushi bei wanasema kwa sababu ya kodi
 
Kwa iyo mi nalipa sawa na Bakhresa sio?

Ila sipingi, kwani huenda ni mpango wa Mungu, tuingie madarakani kwa ushindi wa kimbunga.
 
Back
Top Bottom