Kodi ya Majengo kupitia luku rasmi Vijijini

Ipo wazi mpaka sasa nyumba zote zenye umeme wanakata kodi ya jengo bila kujali ni mjini au kijijini pia nyumba ya tofali au ya nyasi ....hawa jamaa wanataka hela sana bila kujali utu.
Zipo nyumba ukinunu umeme wa 5,000 unatumia hata miezi 4 sasa hapo ukija kununua tena unakutana na deni.
Bado tozo hii inaongeza mzigo kwa wananchi.
Mimi nawapongeza kwa kuwakata,kila MTU achangie Uchumi wa nchi hii.Mbona wa mjini wamewezesha REA kwa muda wote.
 
Jana nilikuwa kijijini kwetu ndani ndani huko, umeme umefika pongezi kwa REA.

Sasa hapa kwa bibi yangu huwa wananunua umeme wa 2000 kila unapokwisha. Walikuwa wanafanya hivyo kabla na baada ya tozo ila jana imeshindikana.

Ikabidi mimi niongezee niwape elfu 10, ile kulipia tu wakakatwa deni la elfu 4.
 
Mkuu
Kweli kabisa alafu kwa mwaka unalipia 12000

Bado watu wanalalamika!

Ova
huko vijijini zipo nyumba zingine thamani yake haifiki laki moja waliwekewa huu umeme wa REA.
Kwa watu kama hao kulipa hiyo 12000/=
ni sawa?
 
Chifu ashikilie hapohapo tena ikiwezekana aingize na land tax huko huko maana wakati ule watu wengine wakimbakiwa kodi na kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi kuna watu walikuwa wakishangilia na kumsifu jiwe.
 
Kweli kabisa alafu kwa mwaka unalipia 12000

Bado watu wanalalamika!

Ova
Unakosea sana, Kodi ya jengo ni kwa makazi yaliyopimwa ama kurasimishwa.
Vijijini wana aina yao ya ardhi inaitwa "village land" na wanasheria yao village land act.
Makazi ya vijijini hayajapimwa, hivyo nyumba hazitambuliki kwenye upangaji. Watu Kama hao kuwatoza Kodi ya jengo ni kuwaonea.
Walichapaswa kufanya ni kupima makazi yao na kuyaingiza kwenye mchoro
 
Fact mkuu Kwa mfano bibi yangu alienda lipia benk mwanzoni mwa Mwaka huu Kodi ya jengo ya Mwaka mzima ila maajabu juzi walipoanza huu mfumo anaanza katwa Tena!
Aisee hii si double taxation kabisa?
 
TANESCO ni kweli hii system imeanza kama ni kweli je, mlitoa taarifa kama hapana je, lini mumeanza utaratibu mpya pasipo taarifa?

Nipo nasubiri majibu nawasikilizia counter
Mie napendekeza kila mmiliki wa nyumba ajulikane ili anaponunua luku asiendelee kukatwa na hii ionyeshe kuwa kwa mwaka amemaliza deni.kuepuka ukatwaji wa luku kila unaponunua umeme,maana wapigaji wa hela nao walishajiandaa kuiba hiyo hela tafadhali mtuondolee usumbufu wa kukatwa kila unapofanya miamala ya luku.
 
Yote haya yamesababishwa na viongozi wasiokuwa nahuruma kwa watu waishio vijijini ambapo mtu anapata pesa kwa maramoja kwa msimu,na matharani wangekuwa wameandaa utaratibu wa ulipaji Kodi za majengo kusingekuwa na sintofahamu kwa mteja.nasema kwa sababu mie tayali wameshakata alfu mbili.
 
Yeah,

Niliona isiwe tabu nikakimbilia Burundi Mkuu, maisha iko huku
Hatuoni shida Kama wananchi wangekuwa wameshawaingiza kwenye utaratibu wa ujazaji wa fomu za nyumba na kuwa vigezo ama Haina vigezo.sasa hapa tunaibiwa kwakutokuwa na mpangilo wa makazi husika.
 
Unakosea sana, Kodi ya jengo ni kwa makazi yaliyopimwa ama kurasimishwa.
Vijijini wana aina yao ya ardhi inaitwa "village land" na wanasheria yao village land act.
Makazi ya vijijini hayajapimwa, hivyo nyumba hazitambuliki kwenye upangaji. Watu Kama hao kuwatoza Kodi ya jengo ni kuwaonea.
Walichapaswa kufanya ni kupima makazi yao na kuyaingiza kwenye mchoro
Ndio maana ninasema wameharakisha ukatwaji wa Kodi,kwani bado vijiji vingi havijapimwa na umeme ameshavuta,hivo Cha msingi tu nikuvipima vijiji vyote ili viingizwe kwenye ramani na hatimae watu walipe Kodi ya jengo kwa utaratibu usioleta Shaka kwa mpokeaji wa mwisho vinginevyo tutakuwa tunawachangia kumalizia nyumba zao na kununua magari ya kifahari na hii Ni hatari Kama wananchi tutanyamaza.
 
Mkuu ninavyojua makazi ya vijijini hayako kwenye utaratibu rasmi wa kulipa kodi ya jengo kwa sababu ni makazi duni ambayo yapo kwenye maeneo ambayo hayajarasimishwa, hii ndo failure kubwa kwa hii serikali ya chifu hangaya ku maximize makusanyo bila kujali taratibu na sheria wala kujali hali za maisha na vipato vya watu. Hayati mwalimu Nyerere aliwahi kusema na hapa namnukuu 'Serikali corrupt haikusanyi kodi, inawaogopa matajiri ambao kimsingi ndo wanatakiwa kulipa kodi na inabaki kufukuzana na maskini' haya maneno ya Nyerere yanaishi leo hii kwa sababu matajiri na wakoloni wanaoitwa wawekezaji wanapata faida kubwa na kujitwalia rasilimali bwerere huku wanyonge wakitaabishwa kwa kodi na tozo zinazobuniwa kwao kila kukicha...........rasilimali zetu, gesi, madini, mbuga, bandari zinamnufaisha nani hadi tuwe watumwa kwenye nchi yetu wenyewe!
Mimi na wenzangu tuna kikundi cha Tofali tumejenga Banda tu la miti tukaweka Mashine zetu za kufyatua tofali Tunashangaa tunakatwa haya makato tena pesa nyingi.
Tanesco wamekurupuka ktk hili
 
Yote haya yamesababishwa na viongozi wasiokuwa nahuruma kwa watu waishio vijijini ambapo mtu anapata pesa kwa maramoja kwa msimu,na matharani wangekuwa wameandaa utaratibu wa ulipaji Kodi za majengo kusingekuwa na sintofahamu kwa mteja.nasema kwa sababu mie tayali wameshakata alfu mbili.
Hatari sanaaaa, wanasema wanataka kuwasaidia masikini lakini cha ajabu masikini anachokipata wanakunyakua juu juu duu🤔
 
Jana nilikuwa kijijini kwetu ndani ndani huko, umeme umefika pongezi kwa REA.

Sasa hapa kwa bibi yangu huwa wananunua umeme wa 2000 kila unapokwisha. Walikuwa wanafanya hivyo kabla na baada ya tozo ila jana imeshindikana.

Ikabidi mimi niongezee niwape elfu 10, ile kulipia tu wakakatwa deni la elfu 4.
Ndo hivyo inatakiwa walipe
 
Back
Top Bottom