Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Kiboko yao binadam tu, kuna kipind huyo koboko alimuua mwenzetu, basi wanakijiji wakatuambia kua kuna mzee flan hv ana dawa ya kuwakamata, tukaenda kumwambia yule mzee akaja na dawa zake akasababisha, yaan daaah koboko wenyewe wakawa wanamfuata yule mzee na aliwapata zaidi ya koboko ishirini wakubwa kwa wadogo akawabeba kwwnye gari akaondoka nao.
 
Green mamba huyo. Pia Ana sumu kali ila Green mamba sio balaa Kama black mamba. Black mamba huogopewa sana kwa sababu ana spidi balaa, anang'ata zaidi ya Mara Moja na pia ni mpenda vurugu sana. Nyoka wengi mkikutana first instinct huwa ni kutoroka n'a watakuvamia tu iwapo watahisi wamo hatarini. Black mamba ni tofauti hapo.
Kwa hiyo, yeye akikuona tu anaanza mashambulizi??
 
Kwa hiyo, yeye akikuona tu anaanza mashambulizi??
Ana uwezo wa kusikia na kuona mbali na anapenda changamoto so akikuona anakufuata kuku-challenge sasa hana kiasi akifika anakugonga anaondoka,wahanga wakubwa wa Koboko ni wafugaji na mifugo yenyewe.ila Mungu anatukinga hawakai sehemu isiyo na misitu mikubwa ndiyo maana sio rahisi kuwaona ila kuna wakati wanafika kwenye makazi ya watu hasa zile sehemu zenye mf:miwa&mikahawa na humu hufuata panya.
 
Yupo nyoka mweusi Buti ama. Mwembamba, siyo mnene kama huyo kwenye picha.
Nyoka mweusi ti
Labda ndiyo black mamba.
Nyoka weusi wembamba wapo wengi sana kule.
Jioni Giza linapoingia ukiwasha taa, ukiacha mlango wazi, nyoka atafika upesi sana.
Kulikuwa na upenyo kwenye mlango nyoka wanaingia..
Sasa sijui kama wanapozunguka ndani ya nyumba dakika sitini wanakumbuka walikoingilia.
Nyoka wadogo wengi sana.
Halafu siku moja mchana saa name nimefungua mlango alikuwepo chatu pale anataka kunimeza.
Nimetazama makala ya wikipedia kuhusu python, sikuona kama kuna uelewa mzuri kama ch
atu anaweza kummeza mtu.
Katika wikipedia wanadhani chatu wanameza rodents tu.
Mimi sijamuona chatu hata siku moja, nashangaa kwa nini nyoka ameniona anakuja kama vile mimi sipo, kama vile mimi sio tishio.
Of course nyoka alikuwa na hofu moja tu, kwamba mimi nitaondoka.
Na ile spidi niliyokuwa nafikiria spidi ndogo ya nyoka probably ilikuwa kwa vile ile sakafu ilikuwa very rough.
Indeed ni bora kusema nyoka alinihurumia kuliko kusema kwamba nilitoroka.
 
Huyu ni hatari sana ila huku kwetu kulikuwa na mzee alikuwa anaitwa Magwisha alikuwa mtaalam wa kupambana na hawa nyoka alikuwa anakata mabapa ya katani kama 20 anajizatiti kwa kujifunga magunia mwili wote anabakiza macho kwa mbali anaingia chimbo kumtimua koboko anakuwa anamrushia yale makatani anayagonga yanakuwa kama yameungua moto zoezi linaendelea mpaka katani ya mwisho koboko anakuwa kachoka sana mzee Magwisha anaingia mzima kupambana naye mpaka anamuua
!

Huyo Mzee jasiri sana
 
Huyu ni hatari sana ila huku kwetu kulikuwa na mzee alikuwa anaitwa Magwisha alikuwa mtaalam wa kupambana na hawa nyoka alikuwa anakata mabapa ya katani kama 20 anajizatiti kwa kujifunga magunia mwili wote anabakiza macho kwa mbali anaingia chimbo kumtimua koboko anakuwa anamrushia yale makatani anayagonga yanakuwa kama yameungua moto zoezi linaendelea mpaka katani ya mwisho koboko anakuwa kachoka sana mzee Magwisha anaingia mzima kupambana naye mpaka anamuua
Huyo mzee lazima atakuwa Mnyamwezi maana huko hao nyoka wanawaona kama mjusi tu
 
Wataalam wa Nyoka, naomba mnisaidie.

Eti kuna jamii ya Nyoka wao wanagonga Utosi wa Binaadam!

Eti nasikia wanajiviringisha Mkia kwenye Mti na kisha wanasubiri Mtu apite, Mtu akipita anga zao wanagonga Utosi
 
Wanakuambia kutana na simba utakimbia na juu ya mti utapanda but hiki kiumbe kukikimbia ni ndoto,hatari zake kuu zinazotambulika ni nyegere(honey badger)na mioto ya msituni si zaidi ya hapo labda ajifie mwenyewe au auawe na mwenzake.
Kuna vikitu vinaitwa Meerkats wanamla koboko kama supu ya kongoro na chapati na ka pilipili kwa mbaali
 
Green mamba na Bkack Mamba wanatofautiana kitu kimoja.Black Mamba mara nyingi huwa shy na huepuka migongano /confrontation na binadamu na viumbe vyengine na hivyo hutokea mara chache kugonga mtu wakati Green Mamba wao ni wepesi katika kupambana/kuwa na confrontation na binadamu

Umeonge kinyume mkuu
 
Back
Top Bottom