Enthusiastic
JF-Expert Member
- Dec 21, 2023
- 347
- 691
Kuna ule msemo unaosema "ajira ni utumwa" kuna ukweli katika msemo huu sana sana kwa TAMISEMI na OR-Utumishi.
1. Hawajali kabisa ustawi wa mtumishi. Mtumishi hawezi kuwa na utulivu kazini kama yuko mbali na Mwenza tena kwa kazi yenye mshahara tu bila marupurupu.
2. Kuna kisingizio cha msawazo na upungufu wa watumishi. Hii hoja haina mashiko. Hakuna mahali ambapo watumishi wamewahi tosha hata huko anakotaka kuhamia kuwaweza kukawa na upungufu mkubwa kuliko anakotoka. Mbona wakistaafu hamuwazuii? Mbona wakifa hamuwafufui?
3. Vyama wa wafanyakazi TALGWU na TUGHE havitetei ustawi wa watumishi ambao ni wanachama. Wanachojua ni kula michango ya wanachama.
4. Ukiendelea kukomalia kuhamia unaambiwa chagua kazi au ndoa. Kuna watu maofisini wamekula maharage wameshiba wanajibu shombo.
5. "KAZI NA UTU" sio halisi.
Dr. Mwigulu Nchemba ofisi yako mnatusumbua. Wewe ni Mkristo, maandiko yanasema, "ndoa na iheshimiwe na watu wote......" Waebrania 13:4. Imagine mtumishi aliye Mbeya DC anataka kuhama kumfuata Mwenza wake Chato DC! Unamzungusha asihame!! Unataka ndoa yake ivunjike?
Nina mengi ya kuandika but kwa leo naomba niishie hapa.
Mods please msiunganishe uzi huu