digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 7,872
- 14,294
Wakuu hamjambo,ni matumaini Yangu kuwa hamjambo,mnaendelea na ujenzi Wa taifa kama kawaida.
Naomba twende kwenye hoja Yangu,nimekuwa nikifatilia swala la uhamisho kwa watumishi Wa umma na urasmu uliopo,ni ukweli usiopingika kuwa kuna haja ya Serikali kutoa tamko kuwa uhamisho umefungwa na nikosa kwa mtumishi kuhama au serikali itamke wazi kuwa kuanzia sasa watu wafuate taratibu za uhamisho na waruhusiwe kuhama na kwenda kufanya kazi maeneo wanayopenda wenyewe.
Hii ni kwasabu maofisaa Wa TAMISEMI wamekuwa miungu watu,na wamehodhi zoezi la uhamisho kwa watumishi Wa umma ili kujipatia kipato,ni ukweli usiopingika kuwa usipokuwa na laki nane hadi millioni moja kamwe huwezi kuhama,nina watu wangu wengi tu ambao wamekuwa wakihama bila kufuata taratibu,ila wapo waliokamilisha taratibu mfano uhamisho Wa kubadilishana,mtu kapata mtu Wa kubadilishana vituo vya kazi lakini hapewi ruhusa ya kuhama,lakini kuna wenye pesa ,hawa huhama hata bila kumjulisha mkurungezi ,yaani barua hutoka TAMISEMI moja kwa moja ,kwa vile mkurugenzi hana mamlaka ya kuhoji barua toka juu basi watu hawa huhama,kituoni kwangu kuna watumishi wawili walihama baada ya kutoa kitu kidogo kwa maafisaa Wa TAMISEMI na kuhama,huku wapo wengi tu ambao wamekamilisha vigenzo vya kuhama lakini hawapewi vibari vya kuhama.
Nashauri rais wetu mpendwa atoe tamko, watumishi waanze kuhama mara moja ili kuepusha huu utapeli unaofanywa na watumishi Wa TAMISEMI,Na hii itasaidia kuamuasha Ari na morali ya watumishi Wa umma, maafisaa wanawaibia wananchi ,ili khali pesa ni ngumu kuipata ,hebu fikiria kununua haki yako kwa milioni moja na kwenda kushibisha Tumbo la jamaa huku ukiacha familia yako ikilalama kwa shida
Naimani kubwa kabisa kuwa waziri husika na rais watatoa tamko ili kuacha nafasi kwa watumishi waliokidhi vigezo wawezi kuhama.
#kaziIendelee.