Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Chama cha Watu wenye ualbino Tanzania (TAS) na Kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC), wamelaani vikali kitendo kinachodaiwa kufanyiwa siku ya Augosti 6, 2023 siku ya 'Simba Day' kumtumia mtu mwenye ualbino mithili ya mtu aliyekuwa katika hali ya nusu utupu na aliyevaa nepi ya mkojo jukwaani mbele ya kadamnasi ya maelfu kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Wadau hao ambao wamekuwa wakitetea haki za watu wenye ulemavu wamedai kuwa tukio la aina hiyo ambalo wamedai ni udhalilishaji lilijitokeza kwenye tamasha la Simba Day mwaka jana 2022, ambapo Klabu ya Simba walidaiwa kutumia jeneza, msalaba na kumnasibu mtu mwenye Ualbino kama msukule.
Kufuatia mfululizo wa vitendo hivyo wamedai kuwa vinatweza utu wa watu wenye ualbino nchini na kuwa vinapelekea kuwepo kwa mjadala mingi katika jamii ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha dhihaka kwa watu wenye ualbino kinyume na haki za binadamu.
Katika tamko lao ambalo wamelitoa leo Augosti 9, 2023 wamesisisitiza kuwa katika jamii nyingi watu wenye ualbino wamekuwa wahusishwa na mila na tamaduni mbaya zinazotweza utu wao, hivyo wamedai kuwa kuendelea kwa vitendo hivyo ni kudidimiza juhudi za Serikali, Mashirika ya Watetezi wa Haki za Binadamu na wadau binafsi wanaoelimisha jamii kuhusu ualbino.
Wadau hao wametoa wito kwa kuitaka klabu ya Simba kuomba radhi kwa watu wenye ualbino na umma wa watanzania kwa vitendo vinavyodaiwa kutweza utu wa watu wenye ualbino na wameiomba Serikali pamoja na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kusimamia jambo hilo.
Wamesisitiza kuwa klabu ya Simba wasipoitikia wito huo unaowataka kuomba radhi watachukua kwenye vyombo vya kisheria.