KKKT ni kanisa kubwa kuliko mtu, Kiburi kimemponza Mchungaji Kimaro

Hii ndio tofauti kubwa ya ma padri wa Katoliki, Katoliki ni utii na nidhamu kwanza ndipo ije ibada, sisi Katoliki tuna mpaka jela za kiaina!, kama alivyo fungwa Archbishop Milingo wa Zambia, aliitwa Vatican akatulizwa!. Ukikatazwa kitu na askofu wako usipotii unafukuzwa kama Padri Dr. Wilbroad Slaa, Felician Nkwera na Kalugendo. Wengi wa wachungaji wenye makanisa yao ni Walutheri, Wakatoliki ni wa kuhesabu!.
P
Huu ni ukweli mweupe kabisa ndugu umeusema hivi vijiwe vya mtaani wenyewe wanaita makanisa ni waLutheri tupu hata waumini wa hayo makanisa.... waKathoric ni wachqche sana

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Kanisa ka Kiinjili, la Kilutheri Tanzania, KKKT ina historia , na ni taasisi ya muda mrefu.

Ina taratibu na kanuni zake , mchungaji au mtumishi atafanya mbwembwe zake zoote lakini lazima awe ndani ya utaratibu wa Kanisa.

Mtumishi akiwa na Karama au upako lazima aongozwe na hekima, na siyo jeuri na kiburi cha kufanya na kusema atakavyo kwa kujiona yuko juu ya taratibu zilizowekwa.

Hakuna Mtumishi aliye juu ya KKKT kama taasisi.
KKKT ni kubwa kiasi kwamba hata askofu hayupo juu ya KKKT.
Sasa hivi tunaona watumishi wanao lipatia kanisa au usharika mafanikio.
Cha kushangaza mafanikio yao yanawapanda kichwani na kuanza jeuri, dharau na kiburi.

Sababu kubwa ni ukubwa wa wafuasi binafsi walionao.

Mwaka jana katika Dayosisi ya Konde , Askofu wake Dr Mwaikali alivuliwa uaskofu. Wengi wa tulioifuatilia ile ibada ya kumvua Uaskofu tulisononeshwa na ukaidi wa Askofu Mwaikali.

Leo, Dayosisi ya KKKT Konde na kanisa linaendelea.

Kama mtumishi anajiona ana karama na unapendwa na watu wengi, bado una wiwa kufuata taratibu za Kanisa.

Kinyume na hapo kwa karama zako anzisha taasisi yako,

Jeuri na kiburi alichoanza kuonyesha hadharani huyu Dr Rev Eliona Kimaro ni upungufu wa maono ya kutoona mbali.
Kuna fununu kuwa Kimaro alionywa mara kadhaa juu ya tabia yake binafsi kujiona yuko juu ya utaratibu, akakaidi, na wakati mwingine anajibu hadharani, na clips zipo.

Sasa inaelekea anavuna alichopanda.
Japo issue ya uhamisho, likizo ni kitu Cha kawaida kwenye taasisi nyingi ila bandiko lako Umeandika meengi nimesoma mpaka mwisho sijaona hicho kiburi chake.
 
Kanisa la wachagga hilo... migogoro huwa haiishi. Subiri ukifika wakati wa uchaguzi ndo utaona muziki wake.

Kiufupi KKKT ni kama CCM tu. Uongozi unapatikana kwa kupiga kampeni na kupigiwa kura. Unategemea migogoro itaisha? Ina maana masuala ya kupanga safu huko yapo kwa sana tu.

Wanaokwenda kiimla (Wakatoliki) ni nadra kusikia wanagombana. Mi nimeshuhudia ugomvi wao mmoja tu ule wa Father Nkwera na wanamaombi wake. Ila Katoliki kiongozi wao wa kitaifa hapa Tanzania anateuliwa na Papa. Hapigiwi kura na wakatoliki walioko hapa Tanzania. Wanaambiwa tu, fulani ndo Papa amemteua kuwa Kiongozi wenu Tanzania.

Hapo ugomvi utaanzia wapi? Nani atayeweka kutoka Tanzania akalipate sikio la Papa amuume na umbea na majungu dhidi ya fulani na fulani.
Mkuu usiingize ukabil katika jambo ambalo ni dhahiri.
Kila Dayosisi ina taratibu zake zilizowekwa kikatiba.
Ukikiuk unachukuliwa hatua.
 
1674132128996.jpeg

Na hao ndio waumini waliolelewa na Rev DR E Kimaro.
" WE LOVE YOU DADY KIMARO"
 
Kanisa ka Kiinjili, la Kilutheri Tanzania, KKKT ina historia , na ni taasisi ya muda mrefu.

Ina taratibu na kanuni zake , mchungaji au mtumishi atafanya mbwembwe zake zoote lakini lazima awe ndani ya utaratibu wa Kanisa.

Mtumishi akiwa na Karama au upako lazima aongozwe na hekima, na siyo jeuri na kiburi cha kufanya na kusema atakavyo kwa kujiona yuko juu ya taratibu zilizowekwa.

Hakuna Mtumishi aliye juu ya KKKT kama taasisi.
KKKT ni kubwa kiasi kwamba hata askofu hayupo juu ya KKKT.
Sasa hivi tunaona watumishi wanao lipatia kanisa au usharika mafanikio.
Cha kushangaza mafanikio yao yanawapanda kichwani na kuanza jeuri, dharau na kiburi.

Sababu kubwa ni ukubwa wa wafuasi binafsi walionao.

Mwaka jana katika Dayosisi ya Konde , Askofu wake Dr Mwaikali alivuliwa uaskofu. Wengi wa tulioifuatilia ile ibada ya kumvua Uaskofu tulisononeshwa na ukaidi wa Askofu Mwaikali.

Leo, Dayosisi ya KKKT Konde na kanisa linaendelea.

Kama mtumishi anajiona ana karama na unapendwa na watu wengi, bado una wiwa kufuata taratibu za Kanisa.

Kinyume na hapo kwa karama zako anzisha taasisi yako,

Jeuri na kiburi alichoanza kuonyesha hadharani huyu Dr Rev Eliona Kimaro ni upungufu wa maono ya kutoona mbali.
Kuna fununu kuwa Kimaro alionywa mara kadhaa juu ya tabia yake binafsi kujiona yuko juu ya utaratibu, akakaidi, na wakati mwingine anajibu hadharani, na clips zipo.

Sasa inaelekea anavuna alichopanda.
View attachment 2487643
Waumini(predominantly women) aliowalea Rev Dr Kimaro wakiandamana.
Mpaka unajiuliza alipanda roho gani ndani yao?
"WE LOVE YOU DADY"
Mch Kimaro aombe radhi tu ili huduma iendelee.
Kushupaza shingo kutamharibia.
 
Back
Top Bottom