Naamini wale waliokuja kuleta neno ndio walikuwa wanaweka kanuni zao kulingana na eneo. Huku walijua kabisa ulabu ndio chanzo kikuu cha matendo maovu wakaona watafute njia ya kupunguza kwa kuutamka kabisa kuwa ni dhambi kwetu waafrika.
Nasikia hata wahubiri walipoenda kwa Waeskimo Kule kwenye baridi Kali ikaonekana ukiwaambia kuwa dhambi itakupeleka kwenye moto wa milele kwao ni kama unawaambia humo kuna maisha mema kwani wamechoka na baridi hivyo wakaambiwa unatupwa kwenye shimo la barafu na hadi Leo wanaiogopa dhambi kwa sababu za shimo la barafu