Tusome mwanzo 9 kuanzia mstrari wa 20 mpaka ule wa 29 tuone jinsi pombe ilivyomtia aibu Nuhu na baadaye akapata hasira na kumlaani mwanae Hamu.
Kizazi cha huyo hamu kipo mpaka sasa;
20.Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21.akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22.Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23.Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24.Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25.Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26.Akasema,Na atukuzwe Bwana,Mungu wa Shemu;Na kaanani awe mtumwa wake.
27.Mungu akamnafisishe Yafethi,Na akae katika hema za Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake.
28.Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.
29. Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.