Kizazi cha watumwa kutoka Afrika ya Mashariki kilifutika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizazi cha watumwa kutoka Afrika ya Mashariki kilifutika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mukuru, Sep 28, 2009.

 1. Mukuru

  Mukuru Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Biashara ya utumwa ilifanyika miongo kadhaa iliyopita (inasemekana bado inafanyika baadhi ya maeneo duniani) na kusababisha watu weusi kuenea maeneo mbalimbali duniani mfano visiwa vya Carrebean, Amerika ya kusini, Marekani na kwingineko.

  Nimesoma kuwa watumwa wengi kutoka Afrika Mashariki waliuzwa uarabuni lakini sijafanikiwa kupata maelezo ya uhakika iweje hakuna watu wenye asili ya afrika kama ilivyo maeneo mengine. Je, kizazi cha watumwa huko uarabuni kilifutika kabisa?

  Naomba wana-JF walio na ufahamu wa suala hili mnifumbue macho.
   
 2. M

  Mbega Mzuri Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nzuri, tunahitaji kujifunza kwa wanahistoria watueleze, maana waarabu waliokuja tangu enzi hizo za ukoloni tunaviona vizazi vyao wengine wakiwa hata ndani ya serikali yetu. ina maana waafrika wamebadilika ngozi na kuwa weupe?
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Kuna tetesi kuwa korodani zao zilikuwa zinapondwa na nyundo ili wasiwe na uwezo wa kuzaa, na ndio maana kizazi chao kikapotea!
   
 4. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  May be waarabu wao walikua ndo middle men wa hiyo biashara na watumwa walikua hawapelekwi uarabuni bali kwenye hizo nchi zilizokua zinanunua watumwa!!
   
 5. Kweli

  Kweli JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tofauti na Trans-Atlantic slave Trade ambapo watumwa wengi waliuzwa North America and The Carrebean kupitia Europe , watumwa wengi katika "East Africa slave trade" zaidi mnamo karne ya 18 - 19 waliuzwa kwa mabebari ya kiarabu ambao walikuwa wanamiliki mashamba katika visiwa vya ukanda huu wa Afrika Mashariki, (Unguja,Pemba,Reunion,Mauritius na Madagascar) na waliwatumia watumwa hao kwa kazi za kulima na majumbani. Kizazi cha watumwa hao bado kimetapkaa katika sehemu hizi mpaka leo.

  Lakini pia zipo kumbukumbu zinazosema kwamba baadhi ya watumwa hawa waliuzwa kwa wazungu na kuishia Amerika.

   
 6. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  DR David Livingstone,alivyofariki mmoja kati ya wapagazi wake,SUSI or CHUMA alisafiri na maiti mpaka uingereza,baada ya mazishi westminister abbey,huyu kipagazi alibaki england-huyu lazima alipata watoto but it seems historia imewapoteza,but hawa jamaa kwa kumbukumbu surely somewhere in england kuna lineage ya susi au chuma
   
 7. w

  wasp JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusidanganyane eti waliuzwa kwa wazungu.

  Majority ya watu weusi walioko Amerika ya kaskazini na kusini walitoka nchi zinazo pakana na pwani ya Afrika magharibi kutoka Namibia mpaka Senegal. Kimawasiliano ni nafuu kumtoa mtumwa kutoka sehemu hiyo mpaka bara la Amerika kwasababu wanavuka bahari ya Atlantic peke yake. Sasa hakuna mantiki kumchukua mtumwa kutoka East Africa umpeleke Amerika kwa sababu itabidi avuke Indian ocean na Atlantic Ocean.

  Kwa kifupi babu zetu toka East Africa waliochukuliwa utumwani, walifanyiwa kitu mbaya na waarabu. Yaani waliwavunja korodani (castrate) na kuwanyanyasa kijinsia kwa kufanyiza kazi za kuwaogesha wake zao pamoja na kuwaingilia hao watumwa kinyume cha maumbile yao.

  Kwa upande wa watumwa wa kike unaweza kuona baadhi ya machotara wa kiarabu tulionao kule Pemba, Unguja, Oman n.k.
   
 8. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  lakini sidhani kama ni kweli mpaka sasa kuna biashara ya watumwa kwenye dunia hii ya utandawazi
   
 9. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa, waarabu walikuwa ni mawakala wa Waingereza, katika kupeleka watumwa kwa makoloni ya Waingereza kabla ya mapinduzi ya viwanda ya Uingereza ya mwaka 1850.
   
 10. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135


  Kwa hiyo watumwa wa east Afrika walipelekwa pemba na Unguja???
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Kusema kuwa watumwa kutoka Afrika mashariki hawakwenda nchi za Marekani ni kutokuwa na data kamili.

  Wakati mataifa kama uingereza yalipositisha na kupiga marufuku biashara ya watumwa, walitumia majeshi ya maji kuzuia biashara hiyo. Lakini waReno waliendeleza. Hili waReno kukwepa vizuizi hivyo, walichukua watumwa kutoka Afrika Mashariki na kuzunguka nao Afrika Kusini na kupiga safari kwenda Brazil.

  Na kuhusu kuwa ni babu zetu waliochukuliwa utumwani hiyo ni siasa tu. Wengi wa watumwa hawa walikamatwa na sisi tuliobaki na kuwauza kwa waarabu au wareno. Hivyo uwezi kuwalalamikia waarabu wakati wewe ndiye uliye wauza.

  Empires nyingi tunazojivunia kama vile ya Mirambo iliendelea kwa sababu ya kujishughulisha na biashara ya watumwa. Hivyo kama ni babu yako ndiye aliyechukuliwa utumwa basi wewe ungekuwa Marekani, Shelisheli.

  Matumizi ya watumwa yalikuwa kwa kazi za nyumbani au mashambani. Kama wapo waliokatwa korodani basi ni wafanyakazi wa nyumbani ambao ni sehemu ndogo sana ya watumwa. Sehemu kubwa ya watumwa ilichukuliwa kwenda kwenye kufanya kazi mashambani.

  Katika sehemu zilizofanyika shughuli za mashamba kama vile Iraq, India wapo watu wenye asili ya Afrika Mashariki. Na hii ni source kuonyesha.

  http://www.npr.org/templates/story/story.php?storyId=96977550&ft=1&f=1001
   
 12. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  waarabu wahuni sana! Hii historia imefichwa na hakuna mtu anataka kuzungumzia! Pumbafu! Hawa jamaa ni wahuni mbaya! Walimfanyia Mwaafrika kitu mbaya sana, alafu sisi tunawabembeleza na Loliondo, nk. Inauma sana.
  Safi sana kwa kuleta hii topic...
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Bro, tuko kuelimishana, si kudanganyana!

  Duh!
  hii inahitaji ufafanuzi wa kina
   
 14. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  dah si mchezo jamani
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Watumwa walipelkwa Arabuni wengi wao ni ma rulers kwa sasa.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kama nani?
   
 17. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ni kweli walipelekwa uarabuni
  Ni kweli wengi wao walihasiwa
  On the positive side Imam mkuu wa Saudi Arabia ni kati yao see "The Saudi Obama"
  Kuna wachache sana wamebakia na wengi wao ni illiterate na wanafichwa ndani ndani kabisa.Nakumbuka miaka ya mwanzo ya 90s kuna rafiki yangu mmoja alienda kuchimba mafuta Oman, akanieleza alivyokutana naye mmoja, mzee, mweusi,alikuwa anaongea kiarabu tu, hajui kusoma wala kuandika wala hajui mambo ya dunia ya nje ya mazingira yake ya karibu.

  Biashara ya utumwa inaendelea mpaka leo hii Sudan ya kusini.
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Published: 10:58PM BST 14 May 2008

  [​IMG] Sheikh Saad: he mounted a PR drive to win over doubters Photo: REUTERS

  [​IMG]

  His Royal Highness
  Prince Bandar Ibn Sultan Ibn Abdulaziz

  Ambassador of the Kingdom of Saudi Arabia to the United States
  Doctor of Laws
  Biographical Note
  His Royal Highness Prince Bandar bin Sultan bin Abdulaziz is the Ambassador of the Kingdom of Saudi Arabia to the United States of America.
  Sheikh Saad al-Abddullah al-Sabah, who died on Tuesday aged 78, became the 14th Emir of Kuwait in 2006 on the death of Emir Jaber.


  Sheikh Saad al-Abdullah al-Salem al-Sabah, born in 1930, was the eldest son of the 11th Emir of Kuwait, Sheikh Abdullah III al-Salem al-Sabah, the man regarded as the founder of modern Kuwait, and of an African woman called Jamila. having headed the Kuwaiti government-in-exile after Saddam Hussein invaded his country in 1990; already in failing health when he took the throne, he reigned for only nine days before being removed by the country's National Assembly.
  Sheikh Saad's finest hour came after Emir Jaber and his court had fled to neighbouring Saudi Arabia as Iraqi troops overran Kuwait on August 2 1990. While the Emir remained shell-shocked by the diplomatic fiasco that had preceded the Iraqi onslaught, Sheikh Saad applied his energy to building a coalition of 30 nations to liberate Kuwait.
  [​IMG]

  Qaboos Oman

  Those are just some and many many more
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  You should remember that 2/3rd of all Arabs are African.

  For Lailah23, "Black" Arab pop singers

  By GustavoMustafa - Posted on February 2nd, 2009
  [​IMG]
  On a lighter note, but in all seriousness, the "personal is political."
  Most of the Arab world's female vocalists in the pop arena could pass to be "white" women.
  When improving my Arabic pronunciation, I listen to pop music from the Arab world.
  Two women stand out in terms of vocals and quality of their music, both are Black Arab women, a sad rarity in the Arab world despite 2/3 of all Arabs being African.
  Egypt's Shereen Ahmad and Saudi Arabia's Waed. YouTube them!
  [​IMG]
  Bookmark/Search this post with:


  Shukran GM, they are both so
  Submitted by lailah23 on Tue, 2009-02-03 12:43.
  Shukran GM, they are both so beautiful and talented, I hope that they get the international
  recognition they deserve and keep their clothes on while doing it.
  I know there are beautiful black women all over the world. Maybe its a good thing they've been kept hidden away, like your best diamonds and gold. Somehow I would not like to
  see them get too Hollowwood, but who knows.
  What a treat.
   
 20. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hao unaowasema wa Loliondo utakuta asili yao ni wa hapa hapa kwani 2/3rd of Arabs are African, besides, wa Loliondo ni UAE na wakati huo wa zama za waArabu kutawala, Oman ilitawala hapa kwetu na karibu pwani yote, na waarabu wajulikanavyo, wamejichanganya na wenyeji. Wengi wetu tuna mashemeji, wajomba, binamu, shangazi au japo jirani mwenye asili ya kiarabu. Hali kadhalika hata huko Arabuni, zaidi nch za Gulf, zina historia ndefu sana na hapa kwetu. Wahabashi walishatawala huko, yemen na sehemu kubwa ya uarabuni, kama waAfrika walitawala huko, huoni kuwa hawa Loliondo ni katika wenzetu?
   
Loading...