UZUSHI Kiwanda cha Goba cha mayai kimefungwa, mayai ya viini viwili yakamatwa

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Habari,

Nimekutana na picha zinazodaiwa kuwa ni kiwanda cha mayai Goba ambacho kinadaiwa kimekaa karibuni. Pia kuna video inasambaa ikionesha mtu akiuza mayai yenye viini viwili.

Picha.jpg



Video inayosambaa ikihusishwa na kuwapo kwa kiwanda Cha kutengeneza mayai

Kuna ukweli wowote kuhusu picha, video na habari hii?
 
Tunachokijua
Tangu Oktoba 13, 2023 kumeibuka uvumi wa kuwapo kiwanda cha kutengeneza mayai bandia mkoani Dar es Salaam maeneo ya Goba. Uvumi huo ulichochewa na Video pamoja na picha iliyowekwa na lifeofmshaba katika ukurasawake wa Twitter (X). Katika andiko hilo lifeofmshaba alihoji:

Hii ya kiwanda Wachina cha mayai Goba ni kweli? Kuna hofu kwamba haijulikani mayai yanatoka wapi na namna yameifadhiwa kuwa changamoto?

Hata hivyo, baada ya kuweka hoja hiyo baadhi ya wachangiaji katika andiko lake walijitokeza na kupinga kwa kuonesha kuwa picha iliyotumika kunasibisha kuwa ni kiwanda cha Goba ilikuwapo tangu mwaka 2018. Mathalani mtumiaji wa mtandao wa Twitter (X) @mmkuti aliandika "Hakuna Kitu kama hicho" na kuambatisha picha ya andiko ikionesha picha hii kutumika mwaka 2018. Tazama hapa chini

mayai-2-jpg.2783695
Maoni haya yaliyotolewa na @mmkuti yanaweka msingi mzuri kuonesha kuwa picha hiyo iliyohojiwa na lifeofmshaba haikuwa ya hivi karibuni na hivyo kuna uwezekano kuwa haihusiani na Kiwanda cha Goba kinachodaiwa kufungwa hivi karibuni.

Zaidi ya hayo JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali ili kupata uhalisia wa picha hiyo na kufungwa kwa kiwanda cha mayai Goba, Dar es Salaam.

Kuhusu picha inayosambaa
Katika mapitio hayo, JamiiForums imebaini kubwa kuhusu picha anayohoji lifeofmshaba imewahi kutumika sehemu mara nyingi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Twitter (X) na Facebook.

Mathalani, kwa mara ya kwanza picha hii ilitumiwa na mtu anayejiita Mayai katika mtandao wa Facebook akiitumia kama picha yake ya utambulisho (Profile picture) Juni 27, 2016.

Pia picha hii imetumiwa na mtumiaji wa Facebook anayeitwa John Haule mnamo Oktoba 23, 2018 akielezea biashara yake ya kutotolesha mayai ya kuku. biashara yake ya kuu.

Kutokana na vyanzo hivyo, ni wazi kwamba picha hii haihusiani na jambo au taarifa zozote zilizotokea hivi karibuni kama anavyohoji lifeofmshaba. Zaidi ya hayo hakuna uthibitisho kama picha hiyo ilipigwa Tanzania.

Kuhusu Kiwanda
Baada ya kusambaa kwa taarifa ya kuwapo wa kiwanda cha mayai kilichofungwa Goba kama ilivyohojiwa na lifeofmshaba Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Hezron Nonga amejitokeza na kukanusha taarifa hiyo. Akielezea zaidi sakata hilo anasema:

Nimeona picha hiyo imezunguka sana kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa hizo sio za kweli na watu wabaya wametengeneza kwa nia ovu ya kupotosha jamii. Goba iko katika Manispaa ya Ubungo, hakuna kitu kama hicho. Tumefuatilia DSM yote hakuna taarifa kama hizi. Tumekuja kugundua kwamba picha hiyo ilipigwa nchini Indonesia mwaka 2017 na mtu mbaya ameipakua kwenye internet na kuiwekea hayo maneno na kuanza kuisambaza kwenye groups za mitandao ya kijamii. Nawaomba tuzipuuze taarifa hizo na Serikali inalifanyia kazi jambo hili. Niwaombe ndugu zangu tusiendelee kusambaza taarifa hizi.
Kuhusu Video ya muuza mayai
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali ili kujua Video hiyo inayosambaa na kuhusishwa habari ya kuwapo kwa kiwanda kinachotengeneza mayai yenye viini viwili Goba.

Katika mapitio hayo tumebaini kuwa Video hiyo inayohusishwa na kuwapo kwa mayai ya kutengeneza si ya hivi karibuni.

Video hiyo iliwahi kuwekwa na mtumiaji wa Facebook aitwaye Cornwell Tanzania June 26, 2023.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo, hoja zinazodai kwamba Goba kuna kiwanda cha mayai kilichofungwa hazina ukweli. Pia, video inayosambaa na kuhusishwa na kuwapo kwa kiwanda kinachotengeneza mayai sio ya hivi karibuni na haihusiani na kufungwa kwa kiwanda chochote.

Je, mayai yenye viini viwili yana usalama?
Pamoja hakuna kiwanda cha mayai kilichofungiwa Goba na Video ya mayai yenye viini viwili haihusiani na kiwanda chochote, leo Oktoba 16, 2023 kupitia Kurasa za Nipashe Serikali imewatoa wasiwasi Watanzania kwa kusema mayai hayo hayana madhara.

Zaidi ya hayo, mnamo Juni 30, 2019 Serikali pia kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) iliwahi watoa hofu wananchi juu uwepo wa mayai yenye viini viwili na kusema kwamba hayana madhara yoyote.
Aidha tovuti ya ‘Egg Safety Center’ imeeleza kwamba nikawaida yai kuwa na kiini kimoja lakini kuna nyakati za nadra hutokea kuwa naviini viwili. Katika kufafanua hoja hii wanaandika:

“Yai kuwa ni viini viwili ni jambo la nadra sana, kwa kawaida mayai yenye viini viwili hutagwa na kuku wadogo ambao mifumo yao yauzazi haijawa kamilifu pia yanaweza kutagwa na kuku wakubwa wanaokaribia kufikaukomo wa kutaga mayai” unaeleza mtandao huo.
Mtandao huo unaelezakwamba viini viwili katika yai moja si jambo la kawaida sana ‘unsual’ kutokakatika yai, na kutokea kwa viini viwili kunaweza kuhusishwa na usalama wachakula.
Habari za mda wadau wa jamik forum.
Nawasalim kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Bila ya kuwachosha niende moja kwa moja kwenye mada kama inavyosomeka katika kichwa hapo juu.

Leo nikiwa katika kuperuzi katika mitandao ikiwa ni baada ya shughuli nzima za kutwa nzima nimekutanq na video ikionyesha muuzaji wa mayqi akiwa na wateja wake wakibishana nuhusu mayqi hayo.

Muuzaji alikuwa akisistiza kuwa kila ya analoliuza lina viini viwili, jambo ambalo lilipelekea baadhi ya watu kutaka kujua na kuamua kununua mayai hayo yaliochemshwa na kuyavunja ili kuthibitisha kile walichoambiwa. Baada ya kuvunja mayai kadhaa ilionekana kuwa kila yai lina viini viwili.

Jambo hili kwa upande wangu ni geni na limenishtua kwa kiasi chake. Kwa anaejua naomba anijuze haya mayai yanatokana na kuku wa aina gani na je hayana madhara katika miili yetu?


Video ipo kwenye link hapa

 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom