Kivule Ukonga tumeikosea nini Serikali?

Waitara hata watoto wake wamehamishwa Zawadi Primary unategemea ye ataendelea kuwepo huko? Bar ya Vegetable haonekani.Kifupi Waitara sio mnyonge tena yaani siyo mwenzetu
Waitara si mwanaUkonga tena, atajifanya mwana Ukonga kwa sababu ana makazi huku lakini najua kwa sasa atakuwa anaishi Masaki huko.

Lakini vilevile tunajua kwamba Mbunge hana hela za kutujengea barabara yeye kama yeye!! Ila juhudi zake za kulipigia kelele hili zinamaana sana!!

Wanaukonga, Kivule na Msongola woote kwa pamoja tupige kelele bila kuchoka kuikataa hali hii!!
Haiwezekani Dar hii zinajengwa barabara mpaka vichochoroni maeneo mengine lakini barabara kubwa na muhimu hii ya Kivule haijengwi kwa miaka sasa!!

Tupige kelele wanaweza kuzisikia siku moja.
 
bongo sijui tumerogwa nani.. yombo, kiwalani, dovya zinajengwa lami mitaani.
yaani kila mtaa una lami.. hata kama hakuna gari linalopita.. watu wanatembelea kwa miguu tu... ukichukua lami zilizowekwa mtaani yombo na kiwalani ukiziunganisha urefu hizo km za lami... unaweza jenga njia ya kivule hata mara 10...

njia zinazohitajika sana wanachelewa kuweka lami.. wale wasiohitaji wanawekewa hadi mitaani
Wale hata siyo CCM bali ni project ya World Bank!

Hivi unafikiri serikali wangeweza kufanya wao hivyo???
 
Wanamwangusha rais Magufuli tuu, bajeti ilipita,mkandarasi akapatikana, akafika site,akaanza kazi, kwa makusudi tu wakaacha kumlipa mkandalasi akaondoka site , sasa haya yanafanyika ili sijui ionekane rais ndo mbaya, watendaji wake shida wanamwangusha mwangusha tu
 
Back
Top Bottom