kimaus
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 565
- 652
Mh. Samia, jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kwa maoni yangu ndio jimbo lenye barabara mbovu kuliko jimbo lolote. Barabara zetu zote ni mbovu yaani ni kama tumesahaulika au tumeikosea Serikali. Barabara ya kutoka Banana kwenda Kivule hadi Msongola ni mahandaki. Kitunda mwanagati ni mahandaki. Ukonga Mombasa to kivule ni Mahandaki.Kitunda, Nyantila mpaka Buza ni mahandaki.
Huku kivule Serikali imejenga hospitali ya Wilaya, lakini kiukweli ni kama haifikiki, maana barabara ni mbovu mno. Hapo awali wakati wa Mwendazake tuliadhibiwa kwa kuwa wawakilishi wetu walitoka upinzani, lkn sasa hv viongozi wetu ni wa chama tawala.
Ukonga tumekosea wapi???