Kivule Ukonga tumeikosea nini Serikali?

Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,872
1,200
Ni barabara kubwa sana iliyonyooka inayoanzia Banana pale mbele kidogo ya Airport Dsm kuelekea maeneo ya Kitunda~Kivule mpaka Msongola!

Barabara hii imetelekezwa kwa muda mrefu sana naweza kusema toka uhuru, hasa kuanzia maeneo ya kitunda shule.

Kwa hisani yenu, uongozi wa jiji la Dsm, Tanroad, halmashauri ya jiji na wilaya ya Ilala, mbunge bwana Waitara na yeyote anayehusika, Tuwaombe mtutengenezee barabara hii!

Barabara hii wala haihitaji mtu kuvunjiwa nyumba na kulipwa kwa vile tayari wananchi walijenga nyumba zao vizuri tu mbali na hifadhi ya barabara. Mtusikie wakuu!!

Tunataabika sana wakazi wa Kivule na Msongola na kucheleweshewa maendeleo kwa sababu ya hii barabara!

IMG_20190422_091106.jpg
IMG_20190422_090322.jpg
IMG_20190422_090319.jpg
IMG_20190422_090536.jpg
IMG_20190422_085931.jpg
IMG_20190422_085755.jpg
 
Tunapata shida sana wakazi wa kivule, hasa kipindi hiki cha mvua. Magari machache mengi yameharibika kabisa.
 
bongo sijui tumerogwa nani.. yombo, kiwalani, dovya zinajengwa lami mitaani.
yaani kila mtaa una lami.. hata kama hakuna gari linalopita.. watu wanatembelea kwa miguu tu... ukichukua lami zilizowekwa mtaani yombo na kiwalani ukiziunganisha urefu hizo km za lami... unaweza jenga njia ya kivule hata mara 10...

njia zinazohitajika sana wanachelewa kuweka lami.. wale wasiohitaji wanawekewa hadi mitaani
 
Mwita alikuwa anatafuta uwaziri kishaupata. Ila 2020 asiposhughulikia barabara basi ndo byebye
Hata awamu hii hakuchaguliwa na wananchi, wana ukonga hawakutoka kabisa kupiga kura lakini tukatangaziwa kapata kura 85,000!!!

Naamini hata 2020 ataendelea kuwa Mbunge tu kwa kuwa awamu hii kura si kigezo cha mtu kushinda uchaguzi!!
 
bongo sijui tumerogwa nani.. yombo, kiwalani, dovya zinajengwa lami mitaani.
yaani kila mtaa una lami.. hata kama hakuna gari linalopita.. watu wanatembelea kwa miguu tu... ukichukua lami zilizowekwa mtaani yombo na kiwalani ukiziunganisha urefu hizo km za lami... unaweza jenga njia ya kivule hata mara 10...

njia zinazohitajika sana wanachelewa kuweka lami.. wale wasiohitaji wanawekewa hadi mitaani
Ule ni mkopo wa wazungu wa world bank kupitia mradi wa DMDP.....sharti kuu ni kuendeleza bara bara za maeneo ya watu wa hali za chini(underprivileged)....huko kwenu kumejaa middle class; not qualified kwa DMDP.
 
Wadau kwa nini tusipige kambi kwa diwani ama mkuu wa wilaya ama kwa manager wa tarura ama kwa RC ili tupate majibu?
Kadri tunavyokaa kimnya ndio tunavyoteseka
 
Ule ni mkopo wa wazungu wa world bank kupitia mradi wa DMDP.....sharti kuu ni kuendeleza bara bara za maeneo ya watu wa hali za chini(underprivileged)....huko kwenu kumejaa middle class; not qualified kwa DMDP.
kaka katika huo mradi ukiacha hizo kata , kuna barabara kibao za hao middle class kama chang'ombe,kijitonyama,kilongawima,sokota mpaka kwa azizi ali,kijichi tuangoma na zingine kibao, hivyo tunaloona hapa ni uzembe tu wa waliokuwepo wakati wa mchakato ndio maana kata za kitunda na kivule hakuna barabara ni mahandaki.
 
Kwan huko mwendokasi si unakuka so kausheni tu kwanza maana nasikia kuna eneo hapo karibu na iyo mitaa mtaporomoshewa stendi ya mwendokasi na shida iyo mtaisikia ktk bomba
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom