Waziri, kilomita 7 ziendelee kutesa watu jimbo la Ukonga?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Kwanza, niishukuru serikali ya mama Samia kwa kufanikisha mradi wa DMDP awamu pili ili kuboresha miundombinu ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Ambapo kutokana na ubovu wake imegharimu mali na maisha ya watu.

Kimsingi mimi ni mkazi anayehudumiwa zaidi na barabara ya Nyerere.

Ambapo barabara hii mbali ya kutumiwa na wakazi Ukonga, Chanika, Kivule, Kitunda, Magole, Majohe, Msongola, pamoja na viunga vyake.

Pia inatumiwa na wakazi wa wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kuunganisha na Dar es Salaam yote.

Hakuna asiyeelewa umuhimu wa wa barabara ya Nyerere kutokana na uwepo wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

Viongozi wote wa kitaifa na kimataifa wanapita katika barabara hii makini.

Ambapo wakati mwingine wageni hupungua, na mwingine huzidi.

Hivyo usishangae kukuta barabara hii imefungwa kwa madakika kibao ili kupisha misafara mbalimbali kwa ajili usalama wa viongozi wetu.

Jambo hilo ni zuri endapo kutakuwa barabara mbadala, ili kunusuru wangonjwa, na wenye shida mbalimbali, na wanaotaka kuwahi shughurini.

Lakini kama hakuna mbadala, ni mateso na maumivu makali mno, endapo Mungu atatunusuru vifo!

Majuzijuzi hapa kampuni ya ujenzi iliifunga barabara hii kwa siku nzima ili kuvusha bombo la maji.

Hakika yalikuwa mateso kwa wasafiri, wagonjwa, wafanyabiashara, pamoja na usumbufu kwa wakazi wa maeneo husika.

Magali yalisongamana kuanzia Majumba sita hadi mwisho wa lami Ukonga! Hakuna kutembea wala kusogea!
Mimi nilikutwa karibu na njia panda ya Kitunda hapo Banana.

Nikawa najihoji kwamba hii barabara ya Kitunda ingetengenezwa kwa kiwango cha lami haingesaidia magari kupita pale misafara na dharura zinapotokea?

Magari yote ya Chanika, kisarawe na viunga vya vyote vya Ukonga wakaingia mjini kupitia Kitunda--Mwanagati hadi kwa Mparange ambapo wanaweza kwenda Tandika au Mbagala. Si unaona kusingekuwa na tatizo kubwa?

Sasa nimemsikiliza mhe waziri Mchengerwa akitaja barabara zinazojengwa ktk jimbo la Ukonga na mradi huu wa DMDP awamu hii kuwa ni Banana mpaka kitunda kwenda Kivule na kwingineko panapofaa.

Lakini sikumsikia akitaja kipande hiki muhimu cha kilomita 7 cha Kitunda-- Mwanagati hadi kwa Mparange.

Kwa hiyo bado wakazi wote wa maeneo yote niliyoyataja hapo awali ikitokea watazuiwa kwa dharura pale uwanja wa ndege, iwe ni misafara au ajali, kama ni mgonjwa ndiyo basi tena! biashara ujue imedoda.

Hapana, naomba wahusika pia waone umuhimu wa kipande hiki muhimu cha km 7 kutoka kitunda mpaka kwa Mparange ili kuipunguzia mzigo barabara ya Nyerere. Na hasa wakati wa dharura.
 
Jimbo la Ukonga linaongoza Kwa barabara mbovu hapa DAR.
Wiki iliyopita nimepita hiyo barabara sina hamu nayo maana sio Kwa yake mabwawa ya maji barabarani, kama serikali watashindwa kujenga kutoka kitunda-fremu kumi-msongola watakuwa hawajafanya kitu pia hata hiyo barabara ya kupitia kitunda,mwanagati Hadi Kwa mpalange ilikuwa kwenye mpango wa kujengwa ndiyo maana upande wa huku Kwa mpalange Hadi mwanagati ujenzi unaendelea ingawa Kwa kusuasua.

Huu mradi wa DMDP huwa kuna na upendeleo Kwa baadhi ya sehemu hasa wanakoishi WASHUA na viongozi wa serikali
 
Vile vile wakazi wa kitonga kupitia mbagala kuna shida kipande cha msongola mpka mbande...yaan barabara mbovu ajabu...safari ya dk 10 mnachukua saa 1.mbunge wa ukonga tukalitazame na hili....
 
Back
Top Bottom