Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF nimewahi kuandika hivi: Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA. Andiko langu hilo, nikiwa kama mtanzania nisiye na chama chochote cha siasa, lililenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.

Maneno hayo sasa yanakuwa ya uhalisia. Tangu Lowassa ajiunge CHADEMA, pamoja na kinachosemwa kuwa CHADEMA/UKAWA imeongeza idadi ya Wabunge na kuminywa kwa demokrasia, wanaCHADEMA kindakindaki wamekuwa kama 'wamejitenga' na chama chao. Wanakosa hoja za kukosoa masuala ya ufisadi kwakuwa waliyekuwa wakimsema sasa wanaye.

Tangu Lowassa kujiunga na CHADEMA, CCM imeibeba ajenda ya kupambana na ufisadi. Haikuwahi kutokea CCM kutamka hadharani kupambana na ufisadi kwenye kampeni zake au hata kwenye utawala wake kwa kujiamini kuliko kuanzia siku Lowassa alipojiunga na CHADEMA. Ufisadi, kama hoja ya kujidai kwa wananchi, umepokwa na CCM toka CHADEMA!

Kimsingi, hata kama ni kimya kimya, Lowassa anaitesa CHADEMA. Anawabana wasipate cha kusema kuhusu ufisadi. Imekuwa rahisi kwasasa kwa wanachama wa CCM kupindisha kila hoja ya ufisadi toka kwa CHADEMA kwa kusema kuwa hata Lowassa aliyesemwa miaka nenda miaka rudi naye yuko CHADEMA.
Unaamini kuwa Lowasa ni Fisadi? una ushahidi? kama huna alishawaambia pelekeni mahakamani kama hamna "SHUT UP"
 
Unaamini kuwa Lowasa ni Fisadi? una ushahidi? kama huna alishawaambia pelekeni mahakamani kama hamna "SHUT UP"

Hawa ndio wanapaswa kutoa ushahidi
 
Attachments

  • 1478676055306.jpg
    1478676055306.jpg
    56.1 KB · Views: 39
  • Thanks
Reactions: jmi
Hongera kwa kusema ukweli kijana wangu. Najua utatukanwa lakini,umeongea ukweli mtupu. Kwa sasa wamebaki na hoja moja tu...eti mtu akifa wanasema 'kafa sababu alimsema Lowassa'...ndio hivyo tena toka siasa za hoja hadi siasa za ramli. Kuelekea uchaguzi mkuu 2010 walitangazia umma kuwa chadema haitasimamisha Wagombea kumpinga Sitta,Mwakyembe,Olesendeka kwa jinsi walivyosimamia ufisadi serikalini lakini eti sasa wamekuwa maadui wao...wanasema eti ripoti ya Richmond ilikuwa ni uongo.
Sidhani kama huyu MTU ni asset kwa chama
 
Tamaa ya fedha ndio imeifikisha CHADEMA hapo ilipo.

Ndoano imekaa shingoni sawasawa hawatoki CHADEMA kwa Lowassa.
 
kumbe we shabiki nildhani mjumbe wa kamati kuu, peleka ushabiki wako simba na yanga ndo panakufaa

Yapni shabiki tena wa muda mrefu. Niko toka enzi tunamuita fisadi. Enzi hizo chama hiki kilikuwa kikisema kitu, watawala wanasikia. Naomba nikuambie kitu, Lowassa sio cdm ma wala hatokaa awe cdm bali anaitumia cdm kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.
 
Sasa choo kilipokuwa nje ya nyumba chama kilikuwa kikilaani ile harufu chafu ya choo. Leo hii chama kile kile kimekihamishia kile choo chumbani. Je bado wana jeuri ya kulaani ile harufu chafu. Ina maana chama chote KINANUKA harufu ya choo.
 
Maneno hayo.aliyesema Dr Slaa wakamuona hafai acha lichama liwadodee
 
Pamoja na kwamba nimekuelewa ila nina mtazamo tofauti, labda kwa mawazo yangu ni kuwa hoja za kisiasa zinabadilika, siasa hubadilika kutokana na agenda iliyopo uwanjani, kwa nionavyo chadema wameporwa ajenda, magufuli anaonekana kuifanyia kazi vizuri sana ajenda ya ufisadi.

Kwa sasa chadema hawawezi kupigia kelele ufisadi sio kwa kuwa wana lowassa ila ni kwa kuwa ajenda yao hii inafanyiwa kazi na magufuli amefanya vizuri sana eneo hili kwa hiyo kelele za chadema hazitaeleweka.

Nionavyo ni kama chadema wanashindwa kutumia fursa zingine kuisimamia serkali mfano kuna swala la ujenzi wa democrasia, swala la utawala bora, katiba mpya, mahusiano ya kimataifa hizi ni ajenda zingepata wasemaji wazuri (bahati mbaya chadema wanakosa wanasiasa wazuri), wangekuwa nao hoja hizi zingewabeba.

Kutegemea ndoto za kina lema kujenga chama ni kupotea kabisa.
 
Hebu pia tazama impact iliyopatikana.
Lowasa kujiunga chademe, ccm wakazinduka kupambana na ufisadi.
Mimi naomba na jembe lingine lijiunge cdm ili ccm washike adabu
 
mimi nilisha jua, maozea yote, makandokando yote, nimabaya yakiwa nje ya chadema, yakifika chadema ni masafi
 
Maneno hayo.aliyesema Dr Slaa wakamuona hafai acha lichama liwadodee
Dr. Slaa alisema "wamehamishia kinyesi chumbani", lakini choo kimebaki kule kule yaani (...) kinaendelea kuzalisha kinyesi zaidi.
 
Tuwaulize ninyi mliohubiri kwa miaka 8 Ufisadi wa Bwana fulani lakini mkampokea na kumteua kuwa Mgombea wenu! Niwaulize ni lini mtamfikisha Mahakamani????
Andika kiswahili ueleweke. Sisi akina nani na tuna mamlaka gani ya kukamata na kushtaki. Nani ana dola?
 
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF nimewahi kuandika hivi: Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA. Andiko langu hilo, nikiwa kama mtanzania nisiye na chama chochote cha siasa, lililenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.

Maneno hayo sasa yanakuwa ya uhalisia. Tangu Lowassa ajiunge CHADEMA, pamoja na kinachosemwa kuwa CHADEMA/UKAWA imeongeza idadi ya Wabunge na kuminywa kwa demokrasia, wanaCHADEMA kindakindaki wamekuwa kama 'wamejitenga' na chama chao. Wanakosa hoja za kukosoa masuala ya ufisadi kwakuwa waliyekuwa wakimsema sasa wanaye.

Tangu Lowassa kujiunga na CHADEMA, CCM imeibeba ajenda ya kupambana na ufisadi. Haikuwahi kutokea CCM kutamka hadharani kupambana na ufisadi kwenye kampeni zake au hata kwenye utawala wake kwa kujiamini kuliko kuanzia siku Lowassa alipojiunga na CHADEMA. Ufisadi, kama hoja ya kujidai kwa wananchi, umepokwa na CCM toka CHADEMA!

Kimsingi, hata kama ni kimya kimya, Lowassa anaitesa CHADEMA. Anawabana wasipate cha kusema kuhusu ufisadi. Imekuwa rahisi kwasasa kwa wanachama wa CCM kupindisha kila hoja ya ufisadi toka kwa CHADEMA kwa kusema kuwa hata Lowassa aliyesemwa miaka nenda miaka rudi naye yuko CHADEMA.
Msahihisho mkubwa

1. Sitarajii toka kwako kuwa Lowasa hana haki kikatiba kujiunga na chama chote isipokuwa CCM.

2. CHEDAMA inaendeshwa kwa katiba yake na itikadi zenye sera madhubuti kwa kila jambo kwa hiyo kufikiri kuwa inaendeshwa kwa ajenda nikushauri tu labda huko kwenye chama dola. Labda ungenilinganishia agenda ya chama dola ni nini?

3. Mimi ni kama wewe sina chama ila naipenda CHADEMA kwa katiba yake itikadi yake na misimamo yake iliyotofauti na chama dola cha dikteta uchwara. Sababu moja kuu ni kuwa chama dola hakina sera wala mwelekeo (Kolimba). Kinaishi kwa matakwa ya vyombo vya dola. Hakina ushiriki wa wananchi tulio wengi zaidi ya ubabe na ukandamizaji.

4. Nakuheshimu kama msomi tena "Learned Brother " ila nausikitikia uchambua wako kunakoelemea personalities badala ya issues. Sioni tofauti yako na akina Lisaboni na wale wachangiaji wa Lumumba bk 7.

5. Jiulize tungekuwa na sera inayokubalika kitaifa (kupitia sanduku la kura huru)na uongozi shirikishi tungekuwa wapi baada ya zaidi ya miaka 50 ya kujitawala.

Zidumu fikra duni za chama dola
 
Back
Top Bottom