Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Msahihisho mkubwa

1. Sitarajii kuwa toka kwako kuwa Lowasa hana haki kikatiba kujiunga na chama chote isipokuwa CCM.

2. CHEDAMA inaendeshwa kwa katiba yake na itikadi zenye sera madhubuti kwa kila jambo kwa hiyo kufikiri kuwa inaendeshwa kwa ajenda nikushauri tu labda huko kwenye chama dola. Labda ungenilinganishia agenda ya chama dola ni nini?

3. Mimi ni kama wewe sina chama ila naipenda CHADEMA kwa katiba yake itikadi yake na misimamo yake iliyotofauti na chama dola cha dikteta uchwara. Sababu moja kuu ni kuwa chama dola hakina sera wala mwelekeo (Kolimba). Kinaishi kwa matakwa ya vyombo vya dola. Hakina ushiriki wa wananchi tulio wengi zaidi ya ubabe na ukandamizaji.

4. Nakuheshimu kama msomi tena "Learned Brother " ila nakusitikia kuchambua kwako kunakoelemea personalities badala ya issues. Sioni tofauti yako na akina Lisaboni na wale wachangiaji wa Lumumba bk 7.

5. Jiulize tungekuwa na sera inayokubalika kitaifa (kupitia sanduku la kura huru)na uongozi shirikishi tungekuwa wapi baada ya zaidi ya miaka 50 ya kujitawala.

Zidumu fikra duni za chama dola
Nisamehe Mkuu kama nimekukwaza. Ni mawazo yangu binafsi Mkuu sana MAGALEMWA
 
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF nimewahi kuandika hivi: Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA. Andiko langu hilo, nikiwa kama mtanzania nisiye na chama chochote cha siasa, lililenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.

Maneno hayo sasa yanakuwa ya uhalisia. Tangu Lowassa ajiunge CHADEMA, pamoja na kinachosemwa kuwa CHADEMA/UKAWA imeongeza idadi ya Wabunge na kuminywa kwa demokrasia, wanaCHADEMA kindakindaki wamekuwa kama 'wamejitenga' na chama chao. Wanakosa hoja za kukosoa masuala ya ufisadi kwakuwa waliyekuwa wakimsema sasa wanaye.

Tangu Lowassa kujiunga na CHADEMA, CCM imeibeba ajenda ya kupambana na ufisadi. Haikuwahi kutokea CCM kutamka hadharani kupambana na ufisadi kwenye kampeni zake au hata kwenye utawala wake kwa kujiamini kuliko kuanzia siku Lowassa alipojiunga na CHADEMA. Ufisadi, kama hoja ya kujidai kwa wananchi, umepokwa na CCM toka CHADEMA!

Kimsingi, hata kama ni kimya kimya, Lowassa anaitesa CHADEMA. Anawabana wasipate cha kusema kuhusu ufisadi. Imekuwa rahisi kwasasa kwa wanachama wa CCM kupindisha kila hoja ya ufisadi toka kwa CHADEMA kwa kusema kuwa hata Lowassa aliyesemwa miaka nenda miaka rudi naye yuko CHADEMA.
No wonder Rais hataki kufukua Makaburi ........ akiyafukua anaweza akawa ndiyo anamsafisha Lowasa!!
 
Tatizo la hawa jamaa wanataka kuharibu au kupotezea huo mgao w 10m. hata bosi wao hana jibu wamebakia kujichanganya tu ufisadi wa Lowassa mbona hata hilo faili hatujalisikia kwenda kwa DPP amebakia kulia lia tu kuwa hawezi kufukua makaburi kea sababu na ya kwake yamo humohumo tusichanganyane bwana
 
Msahihisho mkubwa


5. Jiulize tungekuwa na sera inayokubalika kitaifa (kupitia sanduku la kura huru)na uongozi shirikishi tungekuwa wapi baada ya zaidi ya miaka 50 ya kujitawala.

Zidumu fikra duni za chama dola


Kwa hiyo nani ayafanye hayo yote uliyoyataja? Au ndiyo kama yule anayemlaumu baba yake kwa kushindwa kwake maisha ?
 
Inaonesha ccm imewauma sana baada ya Mh. Mbowe kuanika uozo mnaoufanya huko kwenu mafichoni.Mbadilishe kauli mbiu ya Hapa kazi tu na iwe " Hapa rushwa tu"
 
Ni shabiki wa kutupwa wa cdm na msimamo wangu uko wazi. Walichokifanya cdm ni kama kuwa vitani halafu unamchukua kamanda wa wapinzani wako na kumpa ujemadari kupambana na huko akikotoka. Kibaya zaidi huyo kamanda mamluki hana uwezo wa kujenga hoja zaidi ya siasa za chini ya meza. Hv viongozi wa cdm hamuoni haya malalamiko yetu kila siku kwamba hapo tumelamba galasa?
Weye wapewa bk 7, wenzio wala 10m.
 
Rasimu/Katiba ya Warioba ndio jibu


Hata Katiba ikibadilishwa na kuwekwa mnayoitaka nyie bado CCM itashinda uchaguzi tena kwa tofauti kubwa sana tu na mtarudi hapa na malalamiko yale yale tu, tunayaona Kenya!
 
Huitaji hata cheti cha darasa la 7, kumpa ushauri lugumi, juu ya njia rahisi na nyepesi ya kujisafisha ktk jamii ya watanzania kutokana na tuhuma zinazomuangukia, bila kujali kama ni kweli, au la....
...ni kujiunga na chadema tu, kama alivyofanya lowassa!
Kwani huko lumumba, lugumi keshakuwa fisadi?
 
Weye wapewa bk 7, wenzio wala 10m.

Sijawahi kuishabikia ccm na wala sidhani kama nitawahi, ikiwemo huyo Lowassa. Kwa hiyo hizo unazoziita bk 7 sijui 10m sizitambui, ila nakuambia ukweli ni kuwa hyo Lowassa kwa cdm ni kama wali umeingia mawe.
 
Hata Katiba ikibadilishwa na kuwekwa mnayoitaka nyie bado CCM itashinda uchaguzi tena kwa tofauti kubwa sana tu na mtarudi hapa na malalamiko yale yale tu, tunayaona Kenya!
Kama hamuiogopi, kulikuwa na haja ya kupigisha kura mpaka marehemu?
 
Sijawahi kuishabikia ccm na wala sidhani kama nitawahi, ikiwemo huyo Lowassa. Kwa hiyo hizo unazoziita bk 7 sijui 10m sizitambui, ila nakuambia ukweli ni kuwa hyo Lowassa kwa cdm ni kama wali umeingia mawe.
Pole
 
Kama hamuiogopi, kulikuwa na haja ya kupigisha kura mpaka marehemu?


Hilo silifahamu hivyo sina jibu lake ila ninachofahamu ni kwamba tatizo la Tanzania siyo CCM kuwepo madarakani wala Katiba!
Katiba siyo inayowazuia Upinzani kuingia madarakani, kwani kama Watanzania wakiamua kuiondoa CCM hata kesho inaondoka, kinachoiweka CCM madarakani ndicho hicho kinachozuia Upinzani kuingia madarakani nacho ni Imani, Watanzania bado hawajawa na Imani na Upinzani na kwa kiasi kikubwa bado wanaiamini CCM, utabisha na kukataa unavyotaka lkn huo ndio ukweli!
 
Back
Top Bottom