Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF nimewahi kuandika hivi:
Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA. Andiko langu hilo, nikiwa kama mtanzania nisiye na chama chochote cha siasa, lililenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.
Maneno hayo sasa yanakuwa ya uhalisia. Tangu Lowassa ajiunge CHADEMA, pamoja na kinachosemwa kuwa CHADEMA/UKAWA imeongeza idadi ya Wabunge na kuminywa kwa demokrasia, wanaCHADEMA kindakindaki wamekuwa kama 'wamejitenga' na chama chao. Wanakosa hoja za kukosoa masuala ya ufisadi kwakuwa waliyekuwa wakimsema sasa wanaye.
Tangu Lowassa kujiunga na CHADEMA, CCM imeibeba ajenda ya kupambana na ufisadi. Haikuwahi kutokea CCM kutamka hadharani kupambana na ufisadi kwenye kampeni zake au hata kwenye utawala wake kwa kujiamini kuliko kuanzia siku Lowassa alipojiunga na CHADEMA. Ufisadi, kama hoja ya kujidai kwa wananchi, umepokwa na CCM toka CHADEMA!
Kimsingi, hata kama ni kimya kimya, Lowassa anaitesa CHADEMA. Anawabana wasipate cha kusema kuhusu ufisadi. Imekuwa rahisi kwasasa kwa wanachama wa CCM kupindisha kila hoja ya ufisadi toka kwa CHADEMA kwa kusema kuwa hata Lowassa aliyesemwa miaka nenda miaka rudi naye yuko CHADEMA.