Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

mi nadhani kwa uelewa wangu,hata kama asingekuwepo Lowassa,maadamu ccm wameibeba ajenda hiyo(ingawa sijakubaliana na namna inavyoshughulikia huo ufisadi,labda kama pia hakubaliana na ufisadi wote uliowahi kutajwa na chadema sasa wao wanatafuta ufisadi mpya) ni lazima kama chama cha siasa kiangalie jambo jipya. Fikiria chadema iseme ufisadi,ACT ufisadi,Cuf ufisadi,ccm ufisadi mambo mengine je?
Ajande ifanyiwe kazi,chadema wao waliimba,sasa leo sitarajii chama tawala kiimbe wimbo wa ufisadi badala ya kufanyia kazi ufisadi.

Awepo EL,asiwepo haiwezi kubaki chadema ya 2010.
Tuache kuvilisha maneno ya ajenda vyama vya siasa,Tuangalie uwajibikaji zaidi,maana hata chadema wakibaki na ajenda ya ufisadi midomoni haina maana. Rais afanyie kazi ubadhirifu wote uwe wa nyuma,sasa hata baadae ilimradi tunaokoa wachache kujilimbikizia mali na kulitia hasara taifa.
Umelewa Hela Za Mamvi Wewe
 
Simkubali kabisa bwana Majivuno.Nilichokuwa nakiamini toka kipindi kile mpaka sasa nakiamini.Majivuno ni fisadi tu.
Bwana Majivuno amenifanya nipoteze imani na viongozi wangu wa CHADEMA.
 
Simkubali kabisa bwana Majivuno.Nilichokuwa nakiamini toka kipindi kile mpaka sasa nakiamini.Majivuno ni fisadi tu.
Bwana Majivuno amenifanya nipoteze imani na viongozi wangu wa CHADEMA.
Kaka THINKINGBEING Majivuno hafai. Unakumbuka enzi zile? CHADEMA wamekaribisha tatizo kubwa. Bado uko Monduli?
 
Kaz ya chadema na wafuas wake ni kunja sheria za nchi na kuchonganisha wananchi na serikali yao
 
Kwa kuanza naomba niweke interest zangu wazi kuwa mimi ni mmoja ya watu waliokuwa wakiisupport CDM kabla ya ujio wa Lowasa ila baada ya ujio wa Lowasa niliacha kabisa hata kufatilia siasa yenyewe, kwa ufupi nilikata tamaa. Ni kweli ujio wa Lowasa umewafanya CDM kuwa na kigugumizi kukemea ufisadi, hii kitu ina ukweli kwa kiasi fulani.

Kilichotokea mwaka jana mpaka sasa mimi bado siamini kabisa, na bado najiuliza siasa ni nini haswa. CDM walijaribu kutuaminisha watanzania kuwa CCM ni chama cha mafisadi na Lowassa ni fisadi mkuu na watanzania tukaamini hivyo. Binafsi niliamini kuna watu wana maovu makubwa sana ndani ya CCM zaidi ya Lowasa but walikuwa hawasemwi sana na upinzani kama Lowasa alivyokuwa akisemwa. CDM walisema mengi sana mabaya kuhusu Lowasa na gazeti la mwanahalisi liliandika mengi sana kuhusu Lowasa. Nakumbuka Tundu Lissu aliwahi kufanya mahojiano kwenye kipindi cha General On Monday kwenye miaka kati ya 2006-2008 hivi, alifika studio akiwa na nakala za mkataba wa Buzwagi, Lissu aliuchambua vizuri sana ule mkataba na kuainisha kipengele kwa kipengele ya jinsi ule mkataba unavyoenda kuliangamiza taifa na alisema umesainiwa Hotelini na aliyekuwa waziri wa nishati na madini kwa wakati ule, Nazir Karamagi, Lisu hakuishia hapo, alimsema sana Lowasa kuwa akiwa kama Waziri Mkuu ameshiriki kusimamia utiaji saini makubaliano ya mkataba huo wakiwa kwenye chumba cha Hotel. Nikijaribu kukumbuka kauli za Lisu kuhusu Lowasa kipindi kile na kauli zake kwa sasa hivi, inanipa wasiwasi kuhusu dhamira ya CDM kwa future ya Tanzania.

CDM wamekosa ujasiri wa kukemea ufisadi, hii iko wazi, hawazungumzi tena ufisadi, sasa wanazungumza kuvunjwa kwa demokrasia na kuporomoka kwa uchumi na mbaya zaidi kuliko yote wanafanya siasa za propaganda zaidi kuliko nyakati zote kuwahi kuifahamu CDM. CDM nayoifahamu mimi haikuwa CDM ya propaganda, ilikuwa CDM yenye kujenga hoja zaidi na kuibana serikali kwa fact. CCM ni mabingwa wa propaganda lakini naona CDM wameamua kufata nyayo hizo, na nadhani ni Lowasa na Sumaye ndiyo wanawafundisha staili hii ya kufanya siasa kwakuwa wao ndiyo walikuwa wanafanya staili hii ya siasa zidi ya wapinzani wao huko walikotoka.

CDM walikuwa ni watu wa kujenga hoja sana, watu wenye ujasiri wa kukemea ufisadi na kuwanyoshea vidole wale wanaoaminika kushiriki ufisadi. Nikikumbuka LIST OF SHAME na kufikishwa mahakamani kwa Mramba na Mgonja na kutiwa hatiani, ilinifanya niamini LIST OF SHAME ilikuwa ni ukweli lakini sasa mambo yamebadilika, CDM imewakumbatia watu ambao ilikuwa ikiwasema usiku na mchana. Asili ya UKAWA ni kuipigania katiba ya Wananchi, sasa tuwaulize Lowasa, Sumaye na Kingunge wanaamini rasimu ipi ya katiba kati ya Warioba au ya Chenge? Sumaye amewahi kukiri wazi kuwa anaamini katiba ya serikali mbili, lakini leo anakwambia katiba hii ya serikali mbili inawakandamiza wananchi, swali ni je alikuwa halioni hilo alipokuwa CCM?

Sumaye alisema Lowasa akichaguliwa kugombea Uraisi kupitia CCM yeye anahama chama, Lowasa amekatwa CCM na kuhama chama na yeye mmefata, je huyu mtu ni wa kumwamini kirahisi rahisi, why CDM wamewaamini hawa watu kirahisi rahisi hivi?

Kuna Yule bwamdogo aliyekuwa mbunge wa Sikonge, anaitwa Said Nkumba, Yule muheshimiwa alitumia nguvu nyingi sana kuipinga rasimu ya Warioba kwenye bunge la katiba, na akaunda hadi umoja ulioitwa TANZANIA KWANZA akishirikiana na wabunge wenzake wa CCM, baada ya kukatwa kwenye kura za maoni CCM amekimbilia CDM na CDM wakampokea kirahi rahisi tu.

Mimi naungana na wewe Petro Mselewa, msema kweli ni mpenzi wa mungu, Lowasa anaitesa CDM. Na mimi naamini unafiki na ubabaishaji uliyopo kwenye kila nyanja kuanzia kwenye siasa na kwingineko kwenye hii nchi ndiyo unaligharimu taifa.

Mimi binafsi naamini mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa na mtu aliyewahi kuenjoy matunda ya mfumo wa ukandamizaji uliojengwa na CCM , Lowasa hana jipya atakaloleta kwa Watanzania. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Vyama vya siasa badirikeni jengeni madaraja ya zege kati ya wenye vyama na viongozi nina hakika upepo mkali unaovuma ulaya na marekani Mwisho wake ni dunia nzima Msipo jipanga mwe
 
Ndio waache kelele hapo ujikute ww simba alafu upo chadema ndio unatamani aridhi ipasuke ikufunike bado sumaye naye atamfuata tu kaka yake
 
Back
Top Bottom