Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Kiukweli, Lowassa anaitesa CHADEMA

Hii kitu imenikumbusha siku nilipoamua kuwa upande wa CDM asili na kupambana na wale wanaokataa ukweli kuwa CDM imekosa dira.

Nikweli tumepotea hata mitaaani hoja zinazosemwa ni zile za kuwatoa viongozi katika matope na si kuisaidia nchi na wananchi wake.

Hili liwe fundisho kwa wanaoona kutukana ni siasa.
 
Mkuu, pamoja na kwamba hata mimi sina chama kama wewe, lakini kitendo cha watu kuendelea kumsema Lowasa sio tu kwamba kinaendelea kumpa hadhi ambayo huenda hana, lakini kinasababisha watu wasiokuwa na mlengo wa kisiasa kama mimi na wewe tubaki kujiuliza kuwa huyu mtu ana nini hadi asakamwe hivyo, mpona kuna watu wegi sana wameondoka kwenye vyama vyao lakini kwa kuwa hawatajwi, wameiha sahaaulika ? Huyu mtu kaondoka na nini hadi afuatwe fuatwe hivyo ?
Wanaotajwa si ndiyo maarufu? Basi sawa
 
Ni shabiki wa kutupwa wa cdm na msimamo wangu uko wazi. Walichokifanya cdm ni kama kuwa vitani halafu unamchukua kamanda wa wapinzani wako na kumpa ujemadari kupambana na huko akikotoka. Kibaya zaidi huyo kamanda mamluki hana uwezo wa kujenga hoja zaidi ya siasa za chini ya meza. Hv viongozi wa cdm hamuoni haya malalamiko yetu kila siku kwamba hapo tumelamba galasa?
Mawazo yako, na wewe peke yako ndio unalalamika, umeandika vitu vya kusadikika na sio halisia. Tuambie jokeri ni yupi?
 
A

Asante Mkuu. Hongera kwa kuwa timamu!
Ni hali maisha kuwa magumu kwa sasa mpaka kifikia watu kutembea barabarani na kuongea wenyewe ?!!!

Au ni kupungua kwa clients imesababisha kukupelekea kutafuta adui yako ukajikuta umechagua the opposite side.?!!

Au ni umetishiwa/umepewa mlungula kama propesa bwana yule?!!

Hapa nahisi hali ngumu ya maisha inaweza ikawa imechangia kukufanya kuwa katika hali hii ya kuvurugwa.

Ila samahani mkuu ata nafsi nayo ikusute au uwe na aibu basi na usitie ukakasi dhamira yako uliyokuwa nayo hapo awali.
 
A

Asante Mkuu. Hongera kwa kuwa timamu!
Mkuu samahani sana kwa bandiko langu lile la kwanza ni typig error naomba usinielewe vibaya kwa sababu ninakuheshimu sana na nitaendelea kukuheshimu.

Ila nina wasi wasi kama ni wewe unaweza kutoa mawazo mgando kama haya labda vijana wa lumumba kama kina jinga lao na lizaboni sio vijana wazuri wanaweza wakawa wamehack acc yako au kuna sumu wamekutegea ukavurugwa kiasi hiki.

Nakuheshimu sana mkuu.
 
Hongera kwa kusema ukweli kijana wangu. Najua utatukanwa lakini,umeongea ukweli mtupu. Kwa sasa wamebaki na hoja moja tu...eti mtu akifa wanasema 'kafa sababu alimsema Lowassa'...ndio hivyo tena toka siasa za hoja hadi siasa za ramli. Kuelekea uchaguzi mkuu 2010 walitangazia umma kuwa chadema haitasimamisha Wagombea kumpinga Sitta,Mwakyembe,Olesendeka kwa jinsi walivyosimamia ufisadi serikalini lakini eti sasa wamekuwa maadui wao...wanasema eti ripoti ya Richmond ilikuwa ni uongo.

Leo mtemi chenge yupo ccm hamsemi chochote, kesho akihamia chadema mtakuja tena hapa na kupiga makelele fisadi fisadi,
mahakama ya mafisadi iko tayari.. Lowasa yupo na juzi alikuwa bungeni jiulize why hakamatwi?
 
Wakili msomi na unayejitambua Peter Mselemwa kama kweli unakerwa na ufisadi njoo nikupe kadi ya ccm. Ndani ya ccm kuna demokrasia ya kweli na ndiko kuna mawazo huru, hakuna miungu watu waliojipa madaraka ya kudumu.

naomba unitajie mafisadi ambao hawajawahi kuwa ccm
Rais anasema pale bandarini zilifika meli 63 na kila moja ikiwa na makontena zaidi ya 3000 na hakuna Record yyte ambayo iliwekwa je wakati ufisadi huo unafanyika waziri alikuwa ni mwanachama wa chadema? ATCL imeuliwa na chadema?
 
Ni shabiki wa kutupwa wa cdm na msimamo wangu uko wazi. Walichokifanya cdm ni kama kuwa vitani halafu unamchukua kamanda wa wapinzani wako na kumpa ujemadari kupambana na huko akikotoka. Kibaya zaidi huyo kamanda mamluki hana uwezo wa kujenga hoja zaidi ya siasa za chini ya meza. Hv viongozi wa cdm hamuoni haya malalamiko yetu kila siku kwamba hapo tumelamba galasa?

kwaiyo katika watu wote wa chadema ww umemuona lowasa tu? Kwani lowasa anacheo gani ndani ya chadema na hao wenye vyeo vya juu chadema why wasitajwe kwenye kuporomoka kwa chama?
 
Wakili msomi na unayejitambua Peter Mselemwa kama kweli unakerwa na ufisadi njoo nikupe kadi ya ccm. Ndani ya ccm kuna demokrasia ya kweli na ndiko kuna mawazo huru, hakuna miungu watu waliojipa madaraka ya kudumu.
CCM bado ni mtambo wa kufyatua na kutetea mafisadi. CDM baada ya kumkaribisha yule jamaa yake fulani ni wazi wana kazi ya ziada ya kufanya kwenye hoja ya ufisadi kwa upande mwingine chama dola kinashangaza kutokuchukua hatua zidi ya yule jamaa yake fulani-je hii ina maanisha jamaa ni safi au kama dereva alivyosema yeye hatafukua makaburi? Sote twajua kwenye makaburi kuna mifupa mingi pamoja na ile ya wale mzee mmoja alisema waacheni waenjoi wine na wiski zao na mwingine kasema atawalinda. Kwenye swala ya demokrasia ni wazi vyama vya upinzani vimebanwa na wengine wanafikiri wamekosa agenda. Hii issue ya demokrasia na katiba (especially mabadiliko kuhusu mazingira ya chaguzi zetu) ni agenda tosha na zinahitaji kupewa kipaumbele na upinzani la sivyo CCM wataendelea "kuwaliza" na magoli ya nape, february na jecha. EL anawatesa wote CCM (mikakati yake hawaishi kumhofia hata vikao vyao vya ndani) na CDM (hisia kuwa ni fisadi + propaganda ya CCM kumhusu). Kama Dr yule alivyosema mwishowe swali ni je EL ni asset au liability kwa CDM? Kujipanga kwa CDM kuelekea 2020 kutatoa jibu.
 
Sidhani kama CHADEMA inateseka kama ccm inavyoteseka. Ccm ndo wapo katika mateso makali kwasababu ya Lowassa Factor. Ndo maana wamewabana sana CHADEMA na Lowassa wasifanye chochote kisiasa. Kwani nini hasa kinawazuia CHADEMA kuzungumzia au kukemea ufisadi? Vinginevyo ni wazi kwamba hata wakati CHADEMA inamzungumzia Lowassa kama fisadi hawakuwa na uhakika wala ushahidi na ufisadi wake isipokuwa kutafuta kiki tu. Na kama Lowassa ni fisadi kweli kwanini hashughulikiwi na mamlaka zinazohusika ipasavyo?
Chadema juzi tu wamesema kuhusu rushwa ya ccm hatuoni hatua yoyote inayochukuliwa. Au sijaelewa ulichotaka kusema Mkuu Mselewa?
Nani kawabana. Wafanye hiyo mikutano ndio wajue kwamba awamu hii haijaribiwi. Mlisema JK dhaifu sasa mtaisoma!
 
Kwani Lugumi ana shida gani? Kama fisadi kwanini hachukuliwi hatua?
Tuwaulize ninyi mliohubiri kwa miaka 8 Ufisadi wa Bwana fulani lakini mkampokea na kumteua kuwa Mgombea wenu! Niwaulize ni lini mtamfikisha Mahakamani????
 
Ni shabiki wa kutupwa wa cdm na msimamo wangu uko wazi. Walichokifanya cdm ni kama kuwa vitani halafu unamchukua kamanda wa wapinzani wako na kumpa ujemadari kupambana na huko akikotoka. Kibaya zaidi huyo kamanda mamluki hana uwezo wa kujenga hoja zaidi ya siasa za chini ya meza. Hv viongozi wa cdm hamuoni haya malalamiko yetu kila siku kwamba hapo tumelamba galasa?
kumbe we shabiki nildhani mjumbe wa kamati kuu, peleka ushabiki wako simba na yanga ndo panakufaa
 
Mkuu samahani sana kwa bandiko langu lile la kwanza ni typig error naomba usinielewe vibaya kwa sababu ninakuheshimu sana na nitaendelea kukuheshimu.

Ila nina wasi wasi kama ni wewe unaweza kutoa mawazo mgando kama haya labda vijana wa lumumba kama kina jinga lao na lizaboni sio vijana wazuri wanaweza wakawa wamehack acc yako au kuna sumu wamekutegea ukavurugwa kiasi hiki.

Nakuheshimu sana mkuu.
Mkuu, hata kama nimeongea pumba kwenye bandiko hili usiache kuniheshimu. Nakuomba sana!
 
Sema wewe maana tukisema sisi inaonekana tuna bifu naye. Kwa hakika CHADEMA wamenasa pabaya!
Hilo Gamba Nape Kapambana Nalo Tangu 2008, Nadhani Lilipojivua Alichinja Kuku.Huyo Jamaa Zaidi Ya Kuwa Na Pesa Za Ujanja Ujanja Na Genge Hatari La Wafanyabiashara.Ni Mwiziii
 
Hiyo statement naifananisha na Taarifa aliyo itoa Gavana kuhusu mwenendo wa uchumi, imekaa kimapenzi zaidi na siyo kiuharisia
Wewe Ni Mchumi Mkuu Au Umejuaje Si Uhalisia ? Amma Unpenda Tu Kusikia Uchumi Siyo Mzuri Ili Iweje, Maana Hata Wachumi Tu Ni Mpaka Wafanye Tathmini Ya Hali Ya Uchumi.
 
Back
Top Bottom