Kiukweli, Diamond ni mweupe sana jukwaani

Ipi Mkuu?
Ulitaka afanyeje zaidi ya hapo? Alijitahidi sana hata ulinganisha na performance za wasanii wengine. Kama wadau wengine wanavyosema kuimba huku ukicheza ni ngumu.
Huezi sema hajafanya vyema kiasi hicho otherwise uwe una tatizo naye
 
Mwenzio amesafiri nchi kibao kufanya hizo show unazosema hawez na watu wanatoa pesa kuingia show zake. Hata Iringa tu haijatosha kukuongea taarifa? Ile ya jana haikuwa ya shangwe ilikuwa ya kistaarabu ni tofauti na fiesta zenu.
 
Jana, kwenye tuzo za soka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mwanamuziki Diamond alitumbuiza. Katika tuzo hizo zilizofanyika katika jiji la Abuja, nchini Nigeria Diamond alitumbuiza nyimbo nne. Diamond, aliyeambatana na Rayvanny na wachezaji wake wa jukwaani, hakufanya vyema.

Hayo ni maoni yangu binafsi kwa nilivyomuona. Kwanza, Diamond alionyesha jinsi asivyo na pumzi ya kutosha ya kuimba nyimbo zake jukwaani mfululizo. Pili, Diamond muda mwingi aliacha CD iimbe na yeye akiwa kimya au akiongea mambo tofauti na wimbo wake.

Kiukweli, Diamond ni mweupe na mwepesi sana jukwaani katika kutumbuiza. Diamond ana jambo la kulifanyia kazi katika kutumbuiza jukwaani. Au, aishie kurekodi nyimbo zake na aachane na show za stejini. Maana jana alijitahidi tu kujing'ata midomo yake.
OK,mkuu vipi kwa Tanzania kulikuwa na msanii nwingine aliyealikwa tofauti na mond?
 
Angalau aliitwa!wewe lini tuone ulivyo gado?
Haaaaah hili ndio tatizo kuu kwa Maendeleo ya Taifa hili.
Hivi unaufahamu mtandao wa Rotten Tomato na kazi zake?

Acheni ushabiki wa ajabu watu wanapotoa mawazo constructive, hizo team zenu zisizo taka kukosolewa ziishie INSTAGRAM.
 
Diamond alikuwaga mtamu jukwaani miaka kadhaa hapo nyuma naw ni jina tu ndio linambeba,hata uandishi hayuko poa kbs
NOTE,sijaegemea timu yoyote am team myself
 
Sija angalia show yake, ila nnacho jua diamond ni performer sasa ukiwa perfomer halafu ukaweza na kuimba ni wachche sana wame fanikiwa, na hasa aliye kuwa mtaalam ni Michael Jackson.
Ila hata kina chris brown siku wana perform huwa hawako vzuri sana kwenye kuimba kwa kuwa ni kaz kweli kweli.
Na ndio maana baadhi ya watu toka mwaka 2013 wana lalamika hilo hilo, ila jamaa haachi kupata show ndio kwanza zina ongezeka so nadhan aongeze tu mazoez ila ni ngumu kubalance performance ya juu na kuimba furesh kwa wasanii wengi, na imani ukimpa kiti akae tuu halafu aimbe ana weza imba poa tuu.
nothing sells more than Brand
 
Back
Top Bottom