Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,857
Jana, kwenye tuzo za soka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), mwanamuziki Diamond alitumbuiza. Katika tuzo hizo zilizofanyika katika jiji la Abuja, nchini Nigeria Diamond alitumbuiza nyimbo nne. Diamond, aliyeambatana na Rayvanny na wachezaji wake wa jukwaani, hakufanya vyema.
Hayo ni maoni yangu binafsi kwa nilivyomuona. Kwanza, Diamond alionyesha jinsi asivyo na pumzi ya kutosha ya kuimba nyimbo zake jukwaani mfululizo. Pili, Diamond muda mwingi aliacha CD iimbe na yeye akiwa kimya au akiongea mambo tofauti na wimbo wake.
Kiukweli, Diamond ni mweupe na mwepesi sana jukwaani katika kutumbuiza. Diamond ana jambo la kulifanyia kazi katika kutumbuiza jukwaani. Au, aishie kurekodi nyimbo zake na aachane na show za stejini. Maana jana alijitahidi tu kujing'ata midomo yake.