Kiujumla, nachukia Bongo Flava! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiujumla, nachukia Bongo Flava!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzee Mwanakijiji, May 8, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ukiondoa nyimbo chache na wanamuziki wachache wa Bongo Flava kiujumla naomba nikiri kuwa nachukia bongo flava; siwezi kusikiliza zaidi sekunda chache za mwanzo, nachukia wanavyoimba utadhani walizaliwa Marekani, nachukia wanavyobana pua na kuvuta maneno ya kiswahili, na ninachukia kwa sababu midundo yao yote karibu inafanana (sijui producer ni mmoja na arranger ndiyo producer huyo huyo!?) na ninachukia maudhui yao.. wako vulgar and nasty wakijaribu kujilinganisha na na magangsta wa US!

  Yaani, ukija kwenye nyimbo za mapenzi kwa kweli wamekuwa kama waharibifu wa Classic taarab ambao nao siku hizi wamegeuze Taarab kuwa ndombolo ya aina fulani!

  Ninaamini the kipindi cha dhahabu cha kutukuka kwa muziki wa Tanzania kilikuwa ni 70s na 60s wakati Taarab hadi hivi sasa nadhani bado ya Kina Siti Bint Saad bado wako juu.. ni sawa na kule misri na kina Kurthum..

  I'm sorry! but I had to say it!
   
 2. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  you are not alone...ni nyimbo chache sana za bongo fleva ndio nzuri...kuna huyu anajiita dudu baya, sijui hua anatoa ujumbe gani kwenye nyimbo zake...huwa simwelewi
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kweli
   
 4. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  "napenda manundu.....nachukia majipu"...... nyimbo ina malengo gani hiii!!!.....shenz type
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  yaani huwa najaribu kusikiliza lakini I really gave up! yaani ni bora nicheze mchiriku kwa sababu najua nacheza nini! kuliko haya madudu! Na ukiangalia utaona hata watu wanafurahia zaidi mchiriki, chakacha na ngoma za kikwetu kuliko wanavyofurahia bongo flava transplant
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hata mimi nauchukia na huwa siusikilizi muziki huo. Mi huwa sioni ladha yake kabisa.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, hii ndio faida ya freedom of choice, preference na freedom of expression, chuki zako kwa bongo flavour ni relative.

  Napenda Baadhi ya Bongo.

  Nimesema kupenda na kuchukia zote ni relative, ndio maana kwa asiyeelewa classic music, akisema anachukia clasic music, hiyo ndio freedom yake of choice na freedom of expression, ila akiponda classic kwa hoja kuwa hasikii kitu, hizi sio hoja. The same applies to Jazz kwa wana jazz etc. etc.

  love ya music ni taste na preference kama ilivyo love preference, kwa anaependa mwanamke mwembamba akisema wanawake wanene ni wabovu, anakuwa hajawatendea haki, maadam chaguo lake ni mamiss, wanene anakuwa hana mpango nao, sambamba na wagonjwa wa wanawake weupe, uzuri kwao ni rangi tuu, wakisema wanawake weusi ni wabaya, wanakuwa hawajawatendea haki.

  Nikirudi kwenye msingi wako kuchukia Bongo Fleva siwezi jua taste yako, lakini kuna nyimbo nyingi tuu za Fleva, zimetungwa, zikatungika, zikaimbwa zikaimbika huku zikibeba ujumbe unaozama na uliojitosheza kwa vina na maudhu.

  Ningeweza kukupa mifano michache laiti kwanza ningeliijua taste yako.

  Ila pia nakubaliana na wewe, nyingi ya nyimbo hizi ni trash, na beat wana download tuu, ndio maana stage performance ni chache sana.Kwenye maktaba yangu, nina bongo fleva zaidi ya 100 ambazo ni nzuri, master pieces!.

  Kulinganisha Bongo Fleva na nyimbo za 60's na 70's ni sawa na kulinganisha sera za Ujamaa na Kujitegemea na hizi za sasa za Free Market Economy.

  Kitu ambacho kwa upande wangu, naona Bongo Fleva za Zamani zilikuwa nzuri na zimetulia kuliko hizi za sasa. Ukimsikiliza Zahiri Alli enzi za Kimulimuli, 'Tumerudi Kishujaa', ukaja kumsikiliza enzi za Sambulumaa 'Cleopatra' na ukimsikiliza sasa kwenye wimbo wa ' Inasikitisha', utakubaliana na mimi, Zahir Ali is the same but his music is not the same, he is loosing.

  The same aplies to Balisidya enzi za Afrosa na alipoibuka na 'Shida'. Ndio maana mpaka leo, ukimsikiliza Marijani Rajabu, utakubali kuwa bado pengo lake halijazibika. Ya kale ni dhahabu! Hivyo kufananisha pure gold na English gold, unakuwa hujaitendea haki English gold.

  Hoja zako kwenye uharibifu wa taarabu, nazikubali.
   
 8. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bongo flava iko juu; mfano Mtoto Hidaya, Usiniseme, One love, Shoga ya Shaa (sio ile Fia aliyoirudia), Mbagala, Anatamani, Hatrurudi nyuma kamwe, na moja hivi ya Q Chilla kaimba kidhungu, wanajitahidi watoto. Anyway, nabii hakubaliki kwao.
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Tulia....Msome vizuri Mwanakijiji utaona nini anachozungumza...Kisha Tafakari...Chukua hatua..
   
 10. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nimetumia dakika kumi na tano kusoma tena ile post bwana bendera....ninachoweza kusema ni kwamba bongo flava iko juu, anayeichukia na aichukie. Ukiondoa wimbo wa SMS ambao siwezi kusikiliza mstari wake wa wanza nikamaliza, vijana wanajitahidi na wanapendwa na wengi wa wabongo wanaoishi bongo.
   
 11. paradox

  paradox Senior Member

  #11
  May 8, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bongo Flava sucks in general. [​IMG]
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,729
  Likes Received: 82,665
  Trophy Points: 280
  Nilishasema siku nyingi Bongo Flava na mimi mbali mbali. Napenda sana miziki ya Msongo, nginde ngoma ya ukae, Vijana, Western Jazz, Tabora Jazz, na bendi nyingi nyingine za zamani Tanzania lakini hii bongo flava mmmhhhhhh! Hainigusi kabisaaaaaa huwa naona ni kelele tu ambazo hazina mvuto wowote.
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Lol...mara nishakuwa bwana Bendera(kisa tu natofautiana nawe kimtazamo...hahaaaaaaaa).........Bongo Fleva ni kama Big G,utamu wake haudumu ati....waisha mara tu baada ya kutafunwa kwa dakika kadhaa,kisha yatupwa.............
   
 14. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Jiulize kwa nini asilimia kubwaya wanaBongo Fleva hawawezi kufanya Live performance?....Wengi hawawezi kupiga ala za muziki...wanaenda tu studio wanarekodi sauti(vocals) wanamuachia mzalishaji(producer) kuandaa mapigo(beats) kisha anachanganya muziki Bongo Fleva inaingia sokoni....Ukiwapeleka kufanya live perfomance(kwa kupiga ala za muziki) hawawezi kabisa,na wengi wao hutumia playback kutoka kwa santuri(kwa msaada mkubwa wa maDJ)....Sasa utasema ni wanamuziki hao.....hata waimba kwaya wa kanisani wana nafuu......

  Kuna nyimbo za miaka ya 60,70,80 na mwanzoni mwa 90 zinatamba mpaka kesho,haziishi utamu/hazichuji(ndo maana wengi wa Bongofleva huzirudia kama remix japo huziharibu)....Lakini kuna Bongo Fleva za January 2010 tu zishachuja/zishaisha utamu leo May 2010....

  Kuna baadhi ya nyimbo za Bongofleva ni nzuri(kwa maudhui na hata mdundo).....si kwamba zote ni mbaya
   
 15. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi Asilimia kubwa ya Bongo Flava+Filamu za Kibongo=Sufuri
   
 16. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,739
  Likes Received: 3,173
  Trophy Points: 280
  Hazina mvuto na zaidi hazina maana. Mimi huwa sisikilize hata kwa vipi naona wanapiga makelele tu. Bongo flava imeharibika na mtindo wa kuiga wanataka wafanane na wanamuziki wa kimarekani. Muziki bongo ulikuwa zamani enzi za akina Hemedi Maneti,Nico Zendekaya etc.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  May 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mpenzi mkubwa tu wa muziki.. na nitakuambia nikisikia bongo flava nzuri nitakiri kuwa imenigusa, na hapa natofautisha na muziki wa kizazi kipya ambao hata mtu mzima unaweza kuusikiliza kwani ni wimbo wenye kugusa. Kwa mfano wimbo wa "Cinderella" wa Ali Kiba umefuata mtindo wa utunzi wa nyimbo zetu za dansi za enzi zile wenye kugusa moyo na ukichanganya na sauti ya bwana mdogo na "mpangilio wa vyombo" mpenda muziki mahali popote duniani hata asiyejua maneno atajikuta anatingisha mguu huku anatabasamu. Hicho kinaitwa kipaji na utunzi.

  Ndio maana utaona nyimbo nyingi za bongo flava hazitapita kizazi kingine kwani ni nyimbo za "sasa" tu.. ukiondoa chache mno.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  Asante Mzee Mwanakijiji, sasa angalau naanza kuipata taste yako, pata nafasi sikiliza nyimbo kama za Mr. Paul, Stara Thomas, Prof. J za zamani, Mabaga Fresh, Das Nundas, Lady JD za zamani, Ferouz, Mwana FA za zamani kama 'Alikufa kwa Ngoma', King Crazy G.K-'Sister Sister', M'B Dog, Mr. II, Balozi Dola La Soul, Soggy , Mwasiti, Dataz, Unique Sisters, Afande Sele, Mangwea, Wagosi, etc, etc, the list goes on...

  Nakiri kuna tatizo la mushrooming wasanii wa kizazi kipya kila mmoja akijiona anaweza hivyo kuonekana kama fani imevamiwa mpaka inakuwa kama vurugu tupu. Hali ni sawa na sekta ya habari, pamoja na madudu mengi, bado kuna vyombo vya habari makini na waandishi na watangazaji ambao ni really professionals. Hawa waharibifu wasiichafue sekta nzima kuonekana wote hawafai.

  Kutokana na kuwa mpenzi mkubwa wa muziki, punguza makali ya headline yako ili isiwe Kiujumla, bali ibaki 'Kwa Kiasi Fulani..
   
 19. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,881
  Likes Received: 20,935
  Trophy Points: 280
  kwa muda mrefu nilikuwa na hisia kama hizi kuhusu bongo flava,nikahisi labda UMRI USHAKWENDA HIZO SIO TYPE ZA MUZIKI WANGU,sijui ni umri au ni kuwa BONGO FLAVA ni utumbo??
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  Mmbebabox, sio umri ni taste tuu, kama wewe ukiwa sio mtu wa classics, ni ladha tuu, au jazz music, ndivyo ilivyo, mimi umri umeshapanda, nimeshakata 40, kids wako sekondari, bongo fleva naikubali, tatizo ni kushindwa kutingisha kichwa at the same time my son does that!.

  Kama umepata kuwasikia hawa, Mr. Paul, Stara Thomas, Prof. J za zamani, Mabaga Fresh, Das Nundas, Lady JD za zamani, Ferouz, Mwana FA za zamani kama 'Alikufa kwa Ngoma', King Crazy G.K-'Sister Sister', M'B Dog, Mr. II, Balozi Dola La Soul, Soggy , Mwasiti, Dataz, Unique Sisters, Afande Sele, Mangwea, Wagosi, etc, etc, the list goes on... na bado hujaapreciate bongo fleva kabisa, then achana nazo, siyo ytpe yako..
   
Loading...