mpinga shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 3,236
- 954
Nimeshangaa sana hivi majuzi nilipofika Dar-es-salaam kwa basi la usiku na kufika kituo kikuu cha Mabasi cha Ubungo ambako nilishuhudia mamia ya watu wakiwa wamerundikana katika jengo la abiria wengi wakiwa wamelala chini sakafuni utadhani spagheti kwenye sufuria.
Nilidhani mambo haya yako India peke yake. Duh! Hivi wote hao huwa ni wasafiri? Usalama jengoni humo ni wa kuaminika?
Pia nilidokezwa kuwa wengine wengi zaidi huwa wanalala kwenye parking za mabasi huko nje na giza lote na ghafla nikagundua kuwa pengine na ile meli ya 'Spice Islander' mambo yalikuwa hivyo.
Sasa ikiwa jengo la Ubungo litaanguka, Kuungua (au hata kuzama kwenye maji he,hee) serikali itadai waliokuwemo ni watu 45 tu abiria wa Coaster iliyokuwa iondoke asubuhi yake.