Kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Ubungo

mpinga shetani

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
3,237
947
Nimeshangaa sana hivi majuzi nilipofika Dar-es-salaam kwa basi la usiku na kufika kituo kikuu cha Mabasi cha Ubungo ambako nilishuhudia mamia ya watu wakiwa wamerundikana katika jengo la abiria wengi wakiwa wamelala chini sakafuni utadhani spagheti kwenye sufuria.

Nilidhani mambo haya yako India peke yake. Duh! Hivi wote hao huwa ni wasafiri? Usalama jengoni humo ni wa kuaminika?

Pia nilidokezwa kuwa wengine wengi zaidi huwa wanalala kwenye parking za mabasi huko nje na giza lote na ghafla nikagundua kuwa pengine na ile meli ya 'Spice Islander' mambo yalikuwa hivyo.

Sasa ikiwa jengo la Ubungo litaanguka, Kuungua (au hata kuzama kwenye maji he,hee) serikali itadai waliokuwemo ni watu 45 tu abiria wa Coaster iliyokuwa iondoke asubuhi yake.
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,272
4,662
UBT kuna uozo mwingi. Lakini kwa kuwa anaekusanya ushuru hawezi kuguswa basi tufunge domo.
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,288
16,249
WEEE MULE STAND KUNA WAKABAJI,MATAPELI WA MADINI,BIASHARA HARAMU,abiria si salama kabisa,ulilala vbaya unaibiwa mpaka nguo ulizovaa
 

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,974
1,640
WEEE MULE STAND KUNA WAKABAJI,MATAPELI WA MADINI,BIASHARA HARAMU,abiria si salama kabisa,ulilala vbaya unaibiwa mpaka nguo ulizovaa

Tatizo inabidi walale pale ili wasichelewe magari asubuhi. Mkuu kutoka kimanzi chana asubuhi na hayo mafoleni, ni bora ulale tu hapohapo litakalotokea na liwe
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,288
16,249
tatizo inabidi walale pale ili wasichelewe magari asubuhi. Mkuu kutoka kimanzi chana asubuhi na hayo mafoleni, ni bora ulale tu hapohapo litakalotokea na liwe

siwalaum abira,wakusanya kodi wanazifanyia nini?mpaka wananji haohao wanaowalipa huo ushuru wanalala juu ya mikojo!? Ubt kunanuka kuchafu,hii serikali ni kama pango la wezi! Maushuru teeele kisha wanaenda kujaza matumbo yao
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,625
Tumwombe Kingunge afanye marekebisho katika stendi yake inayomwingizia mabilioni.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom