Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

Hakuna haja ya kuwagusa kama ina maana ya kuwaondoa
Ila ipo haja ya kutengeneza mfumo mzuri wa wao kuwepo kwa manufaa ya wote

Mfumo mzuri ni ndani ya stand ya basi kuwe na mabasi na ofisi za tiketi za mabasi ndo maana ikaitwa stand ya mabasi. Huduma nyingine ziwe nje ya stand.

Sasa na wachungaji nao wakitaka kuja hapo kutafutwe utaratibu? Mama ntilie? Shoe shinners? Watu wa network marketing? Woote watafutiwe utaratibu?

Huwezi tengeneza kitanda kisha ukatafuta utaratibu mzuri wa kulala na mabeseni yaliyojaa maji, kuna siku utalowa. Wawaache tu ili hatua zikichukuliwa ieleweke.

Kuna mkoa nipo watu wamefunga barabara ya lami kwa nyanya na vitunguu.
 
Umeandika sanaaaaaaa kwanini hawa wamachinga wanakuumiza hivi?

Waache wenzio wapate rizki sababu nao wana mahitaji kama yako japo hawana kazi sawa na yako
Sasa nikuulize, tunajenga lami za nn na barabara kama kipaumbele ni wamachinga wapate riziki?

Sababu wanajaza vitu barabarani hakuna njia.

Au wewe ni wale unasapoti kila kitu kesho wakitolewa utasaisapoti tena serikali kwa maamuzi sahihi?

Halafu hawa wengine usidhani ni wamachinga, wanauza vitu vya matajiri matajiri wao wanayafunga maduka wanawapa wao kidogo kidogo. Mapato yanapotea.
 
Tatizo la Marehemu Jiwe alitaka kutengeza 'cult' (kama kadini kake kenyewe wafuasi wanaomuona masiha). Na ili kulitimiza hili akatarget wale wa kipato cha chini sana na kujitwika utetezi hewa. Kutimiza dhamira yake alikwenda kinyume na mfumo wa kistaarabu ili tu aonekane anajali sana, alifanikiwa kupata wa kumuabudu lakini athari yake inakera wengi zaidi.
Leo hii kupita kariakoo ni tabu maana kumejaa wamachinga kila sehemu, ukija ilala boma barabara imekuwa soko la nyanya na vitunguu. Na hiyo stendi ya mabilioni ishakuwa kama tandika tayari, yote sababu ya kiumbe mmoja tu aliyetaka kuwa mungu na leo hayupo tena.
Kila nchi kuna kumwaga na sehemu kama hizo! Hata London! Wewe ukiona hapa kufai huko chagua sehemu za posta posta, Agakhan, oysterbay na kwingineko penye watu wachache. Watanzania walio wengi maisha ya miksanyiko ndiyo wanapenda!
 
Usihalalishe ujinga kwa vile mwingine anafanya ama kwa vile una kigunia chako pembezoni ya barabara ya mwendokasi ya Msimbazi cha kuuzia sabuni na dawa za meno. Yani nisipite njia kwa vile umeamua kujiita mnyonge na kupanga bidhaa zako barabarani? Mkubali mkatae mfumo wa wamachinga kuvamia maeneo hasa mabarabara ni kero kwa wengine.
 
Mfumo mzuri ni ndani ya stand ya basi kuwe na mabasi na ofisi za tiketi za mabasi ndo maana ikaitwa stand ya mabasi. Huduma nyingine ziwe nje ya stand.

Sasa na wachungaji nao wakitaka kuja hapo kutafutwe utaratibu? Mama ntilie? Shoe shinners? Watu wa network marketing? Woote watafutiwe utaratibu?

Huwezi tengeneza kitanda kisha ukatafuta utaratibu mzuri wa kulala na mabeseni yaliyojaa maji, kuna siku utalowa. Wawaache tu ili hatua zikichukuliwa ieleweke.

Kuna mkoa nipo watu wamefunga barabara ya lami kwa nyanya na vitunguu.
Na wengi ya watetezi hapa ni wale waliochukua watoto wa wajomba zao vijijini na kuwapa meza na bidhaa za kuuza pembezoni mwa barabara. Yenyewe yanakaa baa tu kusubiri hesabu jioni.
 
Hakika inashangaza na Kusikitisha kabisa. SERIKALI inashindwa kuweka na kusimamia Utaratibu Mzuri wa Uendeshaji wa Kituo cha Mabasi cha Magufuli kwa kumwaachia Wafanya biashara kutandaza na kupanga Bidhaa zao kwenye Corridor na Sehemu za Kupumzika Abiria.

Hivi kusimamia hilo mpaka aje Mzungu? Mbona Viongozi wetu wazembe sana kwenye mambo ya Msingi?

Tunawaomba Wahusika wawaondoe wafanya Biashara wanaopanga na kutandaza bidhaa zao kinyume na Utaratibu.
Marehemu hasemwi vibaya lakini kuna baadhi ya mambo mzee alkuwa akifanya maamuzi ya kisiasa na wala sio kitaalamu.

Mana nakumbka wakati anafungua iyo stendi ziko kauli nyingi alizisema kuwafavor wafanya biashara wadogo. Ikitokea wamefukuzwa kuweka biashara zao pale, hii inaleta mpasuko wa hatari...thou kuna muda maamuzi magumu inabidi yafanyike ili kubusuru jambo flani
 
Hakika inashangaza na Kusikitisha kabisa. SERIKALI inashindwa kuweka na kusimamia Utaratibu Mzuri wa Uendeshaji wa Kituo cha Mabasi cha Magufuli kwa kumwachia Wafanya biashara kutandaza na kupanga Bidhaa zao kwenye Corridor na Sehemu za Kupumzika Abiria. Hivi kusimamia hilo mpaka Aje Mzungu? Mbona Viongozi wetu wazembe sana kwenye mambo ya Msingi? Tunawaomba Wahusika wawaondoe wafanya Biashara wanaopanga na kutandaza bidhaa zao kinyume na Utaratibu
Wenye Masi waruhusiwe kichukua abiria kutoka sehemu mbalbili za Jiji. Wajiwekee vituo vyao, kama ilivyokuwa kwa baathi ya kampuni kama Dar express Kilimanjaro nk. Masi yaruhusiwe kufikisha abiria kati kati ya jiji ili kuwaondolea usumbufu maana baada ya flyover kujengwa pamoja na mwendo kasi hakuna foleni tena.

Abiria wakiachwa mbezi wanahangaika sana. Kwa mfano mtu wa Mbagala hata kama kuna mwendokasi kubebana na mabegi ni shida. Ukichukua taxi hharama inakuwa kubwa kuliko nali ya basi uliyotokanayo mkoani. Yani changamoto ni nyingi.

Kwa upande mingine naona Ubungo palikuwa mahali sahihi, kwa ville ni katikati ni rahisi kwenda sehemu nyingine za jiji, kituo cha mabasi sio airport kwamba lazima kiwe nje ya mji. Miji mingine kama Nairobi basi linakufikisha hadi katikati ya jiji, hivyo hupati shida.

Pia kuhamisha vituo kila wakati ni kuua mitaji ya watu ambao wanawekeza vitu kama mahoteli karibu na vituo hivyo. Tufike mahali tuwe na mipango mathubuti na ya kudumu.
 
Umeandika sanaaaaaaa kwanini hawa wamachinga wanakuumiza hivi?

Waache wenzio wapate rizki sababu nao wana mahitaji kama yako japo hawana kazi sawa na yako
Waruhusuni basi wapange bidhaa hadi ikulu..ushen.z kabisa huu.

Mji umekuwa kama wa matahira vile..lazima kuwe na taratibu za kufanya biashara..hii kupanga panga kila sehemu ni ujinga mtupu.
 
Waende wakajifunze hata nchi za jirani
Basi,Waone wanavyoweka mfumo wa wafanyabiashara wadogo wadogo
Waende angalau Lusaka pale kwenye bus terminal yao wakajifunze...
Huwezi kujenga standi ya garama alafu ukaruhusu mambo ya ovyo ovyo, utaratibu zero

Siku zote nasema exposure, exposure, exposure kitu muhimu sana

Ova
Sasa mtu kama Jiwe na yule Waziri wake mwenye maneno mengi kuliko vitendo hiyo exposures wataitolea wapi maisha yao yote walikuwa Dodoma to Chato. Exposure ya Jiwe ilikuwa kutia wake za watu na machangu wa chako to chako.
 
Hakuna anaepinga kutafuta kwao rizki hivyo usipotoshe maudhui. Tatizo linakuja wanaitafuataje hiyo rizki. Ikiwa kila mmoja anatumia kigezo cha kutafuta rizki basi hata vibaka hawana makosa.
Kutafuta kwao rizki kusiwe kero kwa wengine, kama kuna sehemu maalum wanatengewa kufanya biashara na hawazitaki wanaishia kukimbilia pembezoni mwa barabara sasa hapo huoni kuwa wanakuwa wabinafsi kwa kuangalia matakwa yao tu kutokuzingatia mahitaji ya wengine.
Na siku nyingine ukiona mtu kaandika sana potezea mama, usisome kuepuka kukereka.
Machinga Complex imegeuka kiota cha ndege na mateja kulala.
 
Sasa nikuulize, tunajenga lami za nn na barabara kama kipaumbele ni wamachinga wapate riziki?

Sababu wanajaza vitu barabarani hakuna njia.

Au wewe ni wale unasapoti kila kitu kesho wakitolewa utasaisapoti tena serikali kwa maamuzi sahihi?

Halafu hawa wengine usidhani ni wamachinga, wanauza vitu vya matajiri matajiri wao wanayafunga maduka wanawapa wao kidogo kidogo. Mapato yanapotea.

Ukiona wamachinga wanauza vitu barabarani katikati kuna watu wameshindwa kuwajibika.... kila kitu kinakua sawa kama utaratibu upo na unafuatwa

Labda uniambie shida yako ni kwamba hutaki kuwaona binadamu wanaoitwa wamachinga sababu walipewa kipaumbele na JPM

Maana binadamu mkianza ubaya hamkosi sababu
 
Back
Top Bottom