Kituo cha Mabasi cha Magufuli kimegeuka soko kwa sababu ya usimamizi mbaya

binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
4,514
2,000
Waende wakajifunze hata nchi za jirani
Basi,Waone wanavyoweka mfumo wa wafanyabiashara wadogo wadogo
Waende angalau Lusaka pale kwenye bus terminal yao wakajifunze...
Huwezi kujenga standi ya garama alafu ukaruhusu mambo ya ovyo ovyo, utaratibu zero

Siku zote nasema exposure, exposure, exposure kitu muhimu sana

Ova
Hata mimi nilitaka kuitaja zambia sababu ndio nchi walau tunaendana kiuchumi, Lungu katuzidi sana, stendi yake biashara zote ziko kwenye fremu kubwa na vifremu vidogo, hakuna bidhaa iliyomwagwa chini wala vimeza meza. Highway yao ya kutokea huku kwetu hakuna banda la turubai utaliona linapepea pembeni mwa barabara, na sehemu za biashara zote highway ziko mita kadhaa kutoka barabarani. Angalau ndicho nilichokiona kwa mwaka huo 2018 nilipokua hapo sijui kwa sasa.

Huku mambo yaliyofanyika kwa miaka mitano mfululizo sidhani kama kuna kiongozi atayekuja kuweza kupambana na machinga wanaopanga biashara zao hadi mabarabarani. Itabidi kutumia mabavu kuwaondoa which sio sahihi au kuwaomba sana na kuwanyeyekea wahame, kitu ambacho nacho hawatatii.
 
atlas copco

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
4,675
2,000
Ukiona wamachinga wanauza vitu barabarani katikati kuna watu wameshindwa kuwajibika.... kila kitu kinakua sawa kama utaratibu upo na unafuatwa

Labda uniambie shida yako ni kwamba hutaki kuwaona binadamu wanaoitwa wamachinga sababu walipewa kipaumbele na JPM

Maana binadamu mkianza ubaya hamkosi sababu
Huna hoja ya msingi unajikan'gatan'gata tuu
 
binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
4,514
2,000
Nchi zingine wana usalama wao wanafanya inside job, kama watawala wanakataa kutekeleza sera fulani kwa masilahi ya wengi wanaingia wao mzigoni.

Anajitokeza mtu na gari lake anajidai limepata shida anasomba biashara za watu kwa mita kadhaa, serikali makini inayopima risk itawaondoa tu hao watu kwa kuwaonesha kuwa kuna siku mtapata madhara hata ya kupoteza uhai. Shida wanaofanya mind games huku bongo yetu nao hawana akili.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
10,904
2,000
Ww si mstaarabu sababu unatumia jina la JPM vibaya kuhalalisha hoja zako za uvuguvugu.

Kwani nikuulize, wamachinga kutolewa barabarani na wakawepo sehemu zao kuna uhusiano gani na chuki au mapenzi kwa JPM?

Sio wewe uliyekubali kuwa sehemu walipojazana wamachinga barabarani viongozi hawawajibiki?

Kwahiyo suluhu pekee uliyoiona wewe ni kuwaondoa?
Kwanini usiwaze kuboresha?
Unatakanwapelekwe sehemu zao zipi?
Ile machinga complex unaijua? Kwanini ilishindikana kufanyia biashara??

Acha unafiki kutafuta kuwatesa wamachinga... na kama huwezi fikiria maboreshochanya heri uache kuhamasisha kuwaumiza wengine
 
Mkuu unapoteza nguvu nyingi kumwelewesha huyo mataga,huyu bado hajarudishiwa akili zake so utakuwa unamuonea bure
 
Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
24,030
2,000
Hakuna kituo kibaya kama cha Magufuli, mara mia turudi ubungo.
Hakuna sehemu ya kula..siku nimewahi asubuhi natafuta sehemu ninywe chai sikupata, wamejaa mama ntilie walioweka vyakula kwenye ndoo.
Kwenda toilet...vyoo vimejaa tumepanga foleni. Nilikereka sana
 
Nilipita pale wiki2 zilizopita nikaambiwa vyakula haviruhusiwi kuingizwa kituoni kwa sasa ila vinapatikana upande wa pili wa kituo
Pia niliambiwa ujenzi unaendelea... na ukikamilika kila kitu kitakua sawa
 
edwayne

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
5,392
2,000
Yani hapo ndio tunakosea.. Kuna vitu vinaitwa uongozi.. Hao wafanya biashara wadogo si wajengewe sehemu yao nje.. Tunaendekeza sana hizi tabia yani kila sehemu wametandaza biashara
 
Mmh haya tusubiri, ila wale machinga mle ndani wapunguzwe
 
Waaai

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,299
2,000
Kwahiyo suluhu pekee uliyoiona wewe ni kuwaondoa?
Kwanini usiwaze kuboresha?
Unatakanwapelekwe sehemu zao zipi?
Ile machinga complex unaijua? Kwanini ilishindikana kufanyia biashara??

Acha unafiki kutafuta kuwatesa wamachinga... na kama huwezi fikiria maboreshochanya heri uache kuhamasisha kuwaumiza wengine
Sasa mtu aliyeweka vitunguu katikati ya barabara unaboresha vipi hayo mazingira? Tutanue barabara. Embu tuishie hapa tu ww nshakuelewa ni binadamu wa aina gani.
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
10,904
2,000
Mmh haya tusubiri, ila wale machinga mle ndani wapunguzwe

Nadhani hakuna kinachoshindikana
Huu ni mradi mpya, ni muda sasa wa uongozi kukaa chini na kufanya tathmini kuona mapungufu na jinsi ya kuboresha.... japo nadhani baadhi ya mapungufu yataondoka pale mradi utakapokamilika kwa asilia 100
 
Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
24,030
2,000
Yani hapo ndio tunakosea.. Kuna vitu vinaitwa uongozi.. Hao wafanya biashara wadogo si wajengewe sehemu yao nje.. Tunaendekeza sana hizi tabia yani kila sehemu wametandaza biashara
Wawepo ndani na nje lakini kwa utaratibu
 
mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
10,904
2,000
Sasa mtu aliyeweka vitunguu katikati ya barabara unaboresha vipi hayo mazingira? Tutanue barabara. Embu tuishie hapa tu ww nshakuelewa ni binadamu wa aina gani.

Hebu weka picha hapa nione vitunguu katikakati ya barabara
Hakuna haja ya kukuza mambo kiasi hiki
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom